DC Hapi atoa masaa 8, walio ktk Hatari ya maafa maporomoko Ukwamani kupatiwa makazi

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Salum Hapi leo ikiwa siku yake ya 6 tangu Kuteuliwa na Rais, lakini pia ni siku ya Pili (2) Tangu Kuapishwa kwake.

Mkuu wa Wilaya ametembelea eneo la Kawe Ukwamani ambalo ni Hatalishi sana kwa Kuwa na Bonde la mapolomoko ambalo Siku Chache zilizopita kuna Udongo ulikatika nakuponda Nyumba ambayo Ndani kulikuwa na Watu Watano ambao walipoteza Uhai wao.

DC wa Kinondoni Mh Ally Salum Hapi akiwa ameambatana na watendani wa manispaa ya Kinondoni akiwamo Injinia wa Manispaa, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Mkuu wa Police (OCD Kawe) wa Kinondoni na Maafisa wengine. Majira ya Saa Tano aliwasili kawe ukwamani kufanya ukaguzi wa eneo la Maafa.

Mkuu wa wilaya alipofika eneo hilo alishitushwa na mazingira yale ambapo Wakazi wa maeneo hayo wanaishi na Vifusi vikiwa vinaning'inia pembeni ya Nyumba zao jambo ambalo ni hatarishi sana kwa Uhai wa maisha yao ukizingatia kuna watu 5 walopoteza maisha siku chache zilizopita.

DC Hapi Ametoa Masaa 8 kwa Watendani wa Mtaa, Kata, Injinia wa Manispaa na Ofisi ya Mkurugenzi Kuhakikisha Ifikapo Saa mbili usiku wawe wamewapatia Mahala pakulala wakazi wanaoishi ktk Eneo hilo Hatarishi.

DC amewaagiza Watendaji Kuhakikisha Waliopo ktk Eneo hilo Hatarishi wanaondolewa Mara Moja Leo wasilale pale kwani ni Hatari sana hasa kipindi hiki ambacho kuna Mvua zinaendelea Jijini Dar es salaam.

Amewambia wahakikishe Wanakaa na Wananchi hao kuhakikisha wanapata Mahala Pakulala, Mwisho Saa Mbili usiku wa leo wampatie Taarifa ya Utekelezaji wa Maagizo hayo na yeye atakuwa ofisini kwake kungoja taarifa hiyo.

"Sisi watendaji tulopewa dhamana hatuwezi kukaa kimya bila kuchukua hatua huku wananchi wetu wako ktk Hatari kubwa ya maafa, na wapa Muda ifikapo saa mbili usiku nipate Taarifa ya hatua mlizokubaliana na utekelezaji wake, mkishindwa kufanya hivo mtawajibika"

Alisema DC Hapi.

DC amesema Kama Watafeli ktk hilo basi Adhabu stahiki zitachukuliwa Dhidi yao.

Mkuu wa Wilaya Huyu ambae amekuja baada RC Paul C. Makonda inaonekana kuwa atakuwa na Speed Kali kama ya Boss wake alomtangukia ambae leo hii ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
 
Duh...Kwa hiyo wawapeleke mabwepande wakawape viwanja na mahema au wawapeleke madarasani wakafungue makambi ya wahanga?...just thinking aloud
 
Wawapeleke ofisi za Mkuu wa wilaya wakae kwa muda,haina maana wafanyakazi wakae kwenye kiyoyozi wakati wananchi wanaumia,waweke meza na viti nje Kazi iendelee wawaachie jengo wana kawe ukwamani
 
mmmmmh wagawane tu kila ofisa achukue raia kadhaa aende nao nyumbani kwake mkuu wa wilaya akionyesha mfano!!
 
Safi sana, ni mwendo wa kupeana Muda na madakika kadhaa kutatua matatizo ya miaka karne nzima...safi , viongozi thabiti....
Tunasubiri matokeo.
 
Back
Top Bottom