Sikonge, nimeshawahi kusema kuwa sioni mantiki ya kuwa na Wakuu wa Mikoa (RCs) na Wakuu wa Wilaya (DCs), hivyo vilikuwa vyeo vya kikoloni na vilitumiwa na wakoloni na si ajabu huyo DC kuamuru Waalimu wachapwe viboko! Vyeo vya RCs na DCs huwa ni vyeo vya kuwasaidia 'wenzetu' ambao hawana pa kwenda na ndo maana utakuta sehemu kubwa ya RCs na DCs ni Wabunge waliopoteza Ubunge, walioondolewa kazini bila sababu za msingi na ili kuficha ukweli au kuepusha kesi anateuliwa kuwa RC au DC (Mfano Col. Simbakalia-RC wa Kigoma alikuwa DG wa NDC, akaondolewa baada ya kukataa matakwa ya Wakubwa kuhusu Mgodi wa Mchuchuma au Liganga).
Kuna DC wa Wilaya ya Hai- Husna Mwilima, huyu alikuwa Katibu wa Tawi moja la CCM Arusha Mjini, baada ya Muungwana na kundi lake kushika hatamu sasa ni Dc wa Hai tena ni bomu kweli! Mkuu wa Wilaya ya Tabora-Moshi Chang'a ulizia elimu yake, utachoka. Lakini alikuwa ni Mkereketwa huko Iringa na Mshereshaji kwenye matukio ya CCM! wako wengi na ni vituko vitupu na wote wamekabidhiwa Mashangingi!
Ingekuwa vema vyeo vya RC na DC vikafutwa wakabaki Maafisa Tawala (RAS na DAS) ambao ndio professionals na si hawa wanasihasa.
Sawa sawa MK, ili kila mmoja ahukumiwe kufuatana na cheo, nafasi yake pamoja na matendo yake!
Lakini kama walimu wamepewa nyenzo zote na mitoto ina feli inapaswa walimu wale mboko.Lakini kama walimu hawana nyenzo zote zinazo takiwa kufundishiwa huyu mkuu wa wilaya inabidi naye ale mboko kwa nini hajapeleka mahitaji ya msingi katika shule husika?
Walimu huenda wakawacha kazi ikiwa adhabu ni bakora.
Kama kuna jina ambalo ungestahili kwa kigeugeu hiki cha hoja basi ni MALAYA ni kipi haswa unachosimamia ndugu yetu? mara kuchapwa sio sawa mara iwe sawa? au analysis yako isiyo poor haina principles inazo zisimamia? im out here, my grade three daughter will respond to your next st*p*d post.
huyo nae anapaswa kuadhibiwa si uliona ya mwaka jana hapo Mbeya rais alikoswa koswa na mawe...asichezee watu kama ameshindwa kazi si anaaachia ngazi tuna watu kibao wanaweza kufanya hivyo.Angalia kule Thailand kiongozi akileta za kuleta nchi nzima watu wanachachamaa.Na kama Rais amepewa nchi yenye kila kitu mf. maji, madini, watu, ardhi nzuri sana n.k; na anashindwa kuwaletea wananchi wake maendeleo tumfanyeje?
Watu kama hawa kwa wenzetu wavimba macho Wachina wangekuwa long time wamenyongwa au wanaoza tu gerezani mtu mmoja anakwiba kiujanja ujanja mabilioni ya pesa bado mnamchekea chekea eti tukimshitaki nchi haita tawalika nani kakwambia????nadhani hawa wakulu walioshindwa karibu kila kitu watahitaji adhabu kubwa zaidi.
Kitu cha ajabu kabisa katika mjadala huu ni kwamba kuna watu wanaunga mkono kitendo hiki. Sawa, lakini je mkuu wa wilaya naye achapwe viboko kwa kuchelewesha mishahara yao? kwa sababu katika waliochapwa kuna walimu hawajalipwa mishahara kwa miezi sita? Waziri wa elimu achapwe viboko kwa kuvuja mitihani ? Kama ndiyo hivyo hata Muungwana naye anastahili viboko kwa kujenga shule bila walimu na maabara !! Masha atachapwa sana kwa kuingilia mchakato wa vitambulisho !!
The primary teachers were caned by a police officer after an inquiry into poor exam results at three schools.
The deputy education minister has condemned the caning but asked the teachers not to take action until the case has been investigated.
The union is thinking of taking action against District Commissioner (DC) Albert Mnali, who ordered the caning in the northern region of Bukoba.
Deputy Education Minister Mwantumu Bakari Mahiza told the Tanzanian Broadcasting Corporation that the DC's action was "abnormal".
She said the DC and the police commissioner should "have their heads examined" and called for a commission to investigate the case.
Soma hapa
Tatizo kubwa nilililo liona viongozi na wafanyakazi au watumishi wengi wa serikalini wamezoea kujifanyia kazi kwa kusua sua na kusukumwa mtu anafanya kazi anavyo taka.Punda haendi bila viboko.
Lakini tusimlaumu pekee huyu mkuu wa wilaya, hata hawa walimu kukubali kwanza kulala chini kupigwa bakora nadhani ni ishara ya mambo mengi kutoka kwa hawa walimu,
1. Hawajiamini
2. Hawajui taratibu zao za kazi
3. Hawawezi hata kujitetea na kuhoji
Kwa hayo tu machache hapo juu inaonyesha ni jinsi gani aina ya wanafunzi watakaotoka chini ya usimamizi au mafunzo toka kwa walimu wa aina hii. Na hili ndio tatizo letu kubwa watanzania, tunarithishana kwa kiasi kikubwa upumbazi, ulegelege n.k. iwe kutoka kwa wazazi au mashuleni.
Haswa!!! hata mimi swali la kwanza nilijiuliza- ivi? hao walimu waliokubali kulala chini na kutandikwa mboko, akili zao zikoje????