DC aagiza kituo kinachowafundisha watoto mambo ya kijinsia kufungwa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash ameagiza kufungwa kwa Taasisi ya Mango Kinder iliyopo Kata ya Dunda Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani baada ya kituo hicho kukiuka utaratibu wa leseni yake ya kutoa haki kwa Watoto na badala yake kuwakusanya Watoto zaidi ya 200 na kuwapa elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo yaliyo kinyume na maadili ya Mtanzania chini ya ufadhili wa Raia wa Ujerumani.

Kituo hicho huwakusanya Wanafunzi kuanzia saa nane mchana hadi saa 12 jioni na kuwapikia chakula kisha kuwafundisha masuala mbalimbali bila ya kibali ambapo DC Halima ameagiza pia kusitishwa kwa kibali cha Taasisi hiyo na leseni na ameitaka Kamati ya Usalama kuondoka na Mmiliki wa Taasisi hiyo Mtanzania Franky Silvester Neumann na Timu yake akiwemo Mke wa Franky ambaye ni Raia wa Ujerumani ili wakahojiwe zaidi.

Awali wakati wa mahojiani yake na DC, Franky amesema “Mimi nilikuwa Ujerumani nikawaambia Tanzania nina Watoto hali yao sio nzuri, wakanipa ufadhili Euro 1000 kila mwezi tuwe tunawapikia Watoto chakula, wakimaliza wanasoma msomo mbalimbali”

DC Halima amesema “Tumekuta zana mbalimbali ambazo inatupeleka kugundua Watoto hawafundishwi maadili mema na mengi ya mambo wanayofundishwa ni mambo ya kijinsia ambayo yanakiuka taratibu na mila na desturi zetu”

“Nimeelekeza tutasitisha kibali na leseni ya Taasisi hii na wote wanaohusika na Taasisi tutaondoka nao kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi lakini hili eneo halitotumika tena, hawa Watoto tangu November mwaka jana wanakuja hapa na Watu hawatoi taarifa kwa wakati, utamaduni wa kwetu wanaenda kuubadilisha”

Source-MillardAyo
 
Njaa yaani ukiwa na njaa mtihani ila nchi kama ilivyo tanzania ile kuomba ufadhili nje sababu ya chakula sio tu aibu bali ni fedheha na ndio maana yanatikea haya
Busara naona sirikali uwafukuze wazungu wote watatuharibia vijana wetu hawa viumbe
Wao washaridhia kupeana baraka wanataka nasi tufate ujinga ujinga kama wao kenge hawa!!!
 
walikuwa wanawafyndisha mambo yao ya kikameruni huko, nchi imekua ngumu sana yani mtu kabisa anapewa msaada ili akafundishe watoto umaaluni , anatakiwa apewe PA kabisa ya saa 24 awe yuko kwao huko Ujerumani.
 
Back
Top Bottom