DAY 2: Updates za mgomo wa madereva wa magari Tanzania - Mei 5, 2015

Kuna haja ya serikali kurudisha mashirika ya umma kwenye sekta ya usafirishaji ili tuindokane na usumbufu wa sekta binafsi ambayo ni ya kibepari na unyama. Kuwe na saccos kama Kenya na ntu binafsi asipewe leseni ya kusafirisha abiria. Ukawa anzeni na hili wazo kwani najua ccm hawawezi.

mkuu hilo nalo neno...yaani ule mfumo wa sacoss za mabasi ya kule kenya uko safi sana. Nakuunga mkono, kwani itatupunguzia hata zile adha za kupigania kuingia kwenye dala dala na kupigwa ndole , kwani mfano ule utaratibu wakupanga mstari abiria wote unaotumika pale Nairobi kenya ,uko poa na hakika unavutia sana.
 
Bila shaka weye itakuwa mutoto ilisaliwa jusijusi tu hata iyo mashirika ya umma weye inayasikia tu haikuyaona eeeehhhh!!!

Hayo mashirika ya umma ndio yaliyotufilisi wakati wa nyerere ingawa alijaribu kuyabeba saaaana kwa pesa za serikali lakini zigo hilo lilimshinda akamtupia mwinyi.

Usinikumbushe ujinga ule, napata kichefuchefu.

Mzee sasa tufanyaje wee na utu uzima wako hautoi fikra chanya au ndio umeishiwa?
 
Leo ni siku ya pili tangu kuanza kwa mgomo wa madereva.
nimepita maeneo ya mbezi,kimara hakuna daladala kabisa, watu wanasafiri kwa kupanda canter na bajaji.
Stand ya mkoa bado hakueleweki abiria wanaonekama kuwa wachache sana. Tofauti na siku ya jana

Mabasi yote yaliyopaki kituo cha Umma pale Ubungo nashauri yapigwe na breakdown kama ambavyo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha aliamuru kuwa basi lolote litakaloonekana kituo cha mabasi lipigwe ban na kupelekwa kituoni na kulipa fine
 
Hahahahaaahhaha mim nimeshindwa kuona tofauti ya serikali ya tanzania na ya somalia au afghanistan ukiacha vita
 
Mwisho wa siku madereva wataumbuka kwani abiria wanaangalia namna yoyote ya kufika waendako. ndio maana leo stendi ya ubungo abiria ni wachache. Hao madereva kama wanayo ajenda ya kisiasa na waizungumze lakini wasilete adha kwa abiria. mimi sijaona mtu kulazimishwa kugoma..kama ni mgomo halali hakuna sababu ya kuwazuia madereva wengine waendelee na shughuli za kuwasafirisha abiria
 
Mw@nza tunapeta tu full daladala,labda wanatoa mgomo kwa mgao wakimaliza dar wana hamia kanda ya ziwa pia kanda ya kati
 
Kuna haja ya serikali kurudisha mashirika ya umma kwenye sekta ya usafirishaji ili tuindokane na usumbufu wa sekta binafsi ambayo ni ya kibepari na unyama. Kuwe na saccos kama Kenya na ntu binafsi asipewe leseni ya kusafirisha abiria. Ukawa anzeni na hili wazo kwani najua ccm hawawezi.

Mkuu unazungumzia Serikali gani hizi za CCM? Ikiwa TRENI imewashinda hadi wananunua Mabehewa chakavu....!! labda tusubiri ya UKAWA lkn kutegemea CCM nikujilisha UPEPO
 
Kama serikali wanadai mgomo ni batili kwa nini wasiende mahakamani kuuzuia? Migomo ya walimu na madaktari huzuiwa kwa nguvu ya mahakama, kwa nini siyo huu mgomo?

Kwani Mahakama Ikiingilia Kati, Kuendesha Gari ni lazima? na wakiwaforce kwa nguvu ya serikali c wanasema tu hatutaki kuendesha kwan hao watumishi wa serikali? waangalie tu nini wanadai wakubaliane
 
Ndugu zangu wa njia ya Ngaramtoni kwenda Mjini Arusha kuna mwenye updates? Mi bado nimevuta shuka, jana wenye Noah walituchaji bei ya taxi wakati wengine mishahara yetu haifikii hata posho ya siku moja ya mbunge wa inji hii!!!
 
Kuna haja ya serikali kurudisha mashirika ya umma kwenye sekta ya usafirishaji ili tuindokane na usumbufu wa sekta binafsi ambayo ni ya kibepari na unyama. Kuwe na saccos kama Kenya na ntu binafsi asipewe leseni ya kusafirisha abiria. Ukawa anzeni na hili wazo kwani najua ccm hawawezi.

kwani madai yao ni yapi ambao wa sekta ya umma hawatoyahitaji?msingi ni madai na sio nani asafirishe
 
Tuwe binadam kidogo.kipi wanachodai kibaya?au mnapenda wakiwa na mawazo watuue njiani?madai yao ni ya msingi sana.sema tatizo transporters wengi wanasiasa ndo maana inakua ngumu.mfanyakazi gani hataki madai kama yao?
 
Back
Top Bottom