Wasimamizi wa Mwendokasi wameng'oa mifumo ya elektroniki, wameua magari Rundo, madereva wanagongana barabaran, foleni: RC na DC mpo wapi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,124
Ni aibu kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na viongozi wote wa DSM kwa namna mabasi ya mwendo kasi yanavyofanya kazi.

Mradi mkubwa kama huu hakuna kiongozi yeyote anayeuangalia wala kusimamia unajiendesha wenyewe. Magari yawepo au yasiwepo wala hakuna anayeangaika.

Mifumo ya ukataji tiketi imehujumiwa, tiketi zinachanwa kwa mkono, abiria wanakaa vituoni masaa, watu wanajazana kwenye magari kama wanyama and still yupo mkuu wa mkoa na wilaya wapo ofisini wanasubiri mapato.

Magari yanazidi kufa kila siku hakuna Karakana yakufanya ukarabati. Magari yanahongana unajiuliza hawa madereva waliowekewa njia zao maalumu wanashindwa kuwa na akili timamu?

Mradi una Rundo wafanyakazi na maaskari utadhani abiria wapo vitani. Mbona daladala hakuna askari? Askari kwenye vituo wanajazwa wa kazi gani?

NI aibu kwa kweli
 
Mkuu ni mwendo wa kila mtu kula kwa urefu wa kamba yake! Bila mwekezaji hali itazidi kuwa mbaya,tutarudi kule kule!
 
Mode of Operation......
  1. BRT imejinasibu kutozingatia mkataba wa huduma kwa wateja
  2. Uharibifu wa magari unaoendelea ni uhujumu uchumi.
  3. Sehemu kubwa ya madereva tuliambiwa ni wanajeshi hivyo ni dalili ya uasi na kutotimiza wajibu ipasavyo
  4. Serikali inatulazimisha wananchi tupige kelele kwamba hili shirika libinafsishwe....
 
Ni aibu kwa mkuu wa mkoa , mkuu wa wilaya na viongozi wote wa DSM kwa namna mabasi ya mwendo kasi yanavyofanya kazi...
Hakika ni uozo mtupu. Kama ni kweli hakuna karakana ya kuservice na kufanya matengenezo magari, na pia kampuni kama hiyo kama haina bohari kuweka vipuri vya harakakwa bei ya ujumla na pia kutuo chake cha kuweka stock ya mafuta kwa bei ya jumla basi mpango utakua ni ulaji tu kwa kiwango kikubwa. Nina shaka pia taaluma hazijazingatiwa kwenye ajira kila level kuanzia bodi.
 
Na hiyoooi tumpe Azam ? Kuna shuda kubwa sana serikalini waendesha miradi hawWezi kabisa ......kazi sanaaaa Kisena na Juma Maxcom wako jela wamepuga ndefuuuu......sanaaa
 
Ni aibu kwa mkuu wa mkoa , mkuu wa wilaya na viongozi wote wa DSM kwa namna mabasi ya mwendo kasi yanavyofanya kazi....
Toka kaondoka MWAMBA YULE Kwa Sasa ni BORA LIENDE, FREE FOR ALL! Mama kusafiri na kutunikiwa shahada za mbwembwe, bata, kutengeneza masinema, kufumuwa mifumo, kujipangia mida ya kazi, kuonea raia nk nk 👺💢🗯️😠😡😤😾🤬🥹
 
Back
Top Bottom