Diesel generator
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 706
- 663
Habarini mnaosoma ukulasa huu.
Dawasco shida mnayotupatia ni kubwa sana. Maji yanatoka siku moja tu kwa mwezi! Eneo la Kinyerezi Zimbili kuna barabara ya lami inayotokea Kinyerezi darajani kwenda Gongo la Mboto.
Inakuwaje maji yakitoka upande mmoja na upande wa pili haupati maji? Nina miezi mitatu tangu niishi hapa. Na maji kwa miezi mitatu yametoka mara tatu pekee, tena kwa masaa. Sasa tuilaumu Serikali kwa kukosa maji au Dawasco kwa uzembe?
Mnapaswa kutambua kuwa mna dhamana kubwa sana toka serekalini upande wa maji kuhakikisha kuwa, maendeleo ya huduma ya maji yaliotekelezwa na serikali yanadhihirika na jamii kunufaika nayo.
Inakuwa inaleta ukakasi kiongozi wa serekali kusema tumefikisha maji huku nyie mmetulia na mkitambua maji hayatoki baadhi ya sehemu. Hadi mnatufanya tuwaze huenda mnafanya makusudi?
Maana kwa huduma inavyofanyika tukiwaza mnaigombanisha au kuihujumu serekali tutakuwa tunakosea?
Hakikisheni maji yanatoka japo kwa zamu. Yani miezi mitatu maji yametoka mara tatu?
Tunataka maji.
Sent using Jamii Forums mobile app