DAWASCO mabomba yenu mengi Tandika yamepasuka wiki sasa mnakuja na kuondoka na kuacha mabwawa

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Mafundi wa DAWASCO Wilaya ya Temeke wamekuwa wakifika maeneo ambayo mambomba yamepasuka na kuondoka bila kuyafunga au kuyaziba mabomba yaliopasuka kwa wiki moja sasa na kuacha mabwawa makubwa mitaani na barabarani.

Mitaa iliyoathirika na huduma hafifu za DAWASCO ni pamoja na mtaa wa Chiwanda ambao kuna bomba limepasuka nje ya nyumba karibu na kituo cha daladala cha Tabata na Segerea kilichopo Tandika na kuweka bwawa kubwa la maji ambalo hata samaki unaweza kufuga.

Pia makutano ya mtaa wa Chiwanda na Mwongozo kuna bomba pia limepasuka wiki moja sasa na kuleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa mtaa wa Mwongozo kwa maji kutapakaa mtaa huo bila suluhu yoyote kutoka DAWASCO pamoja na kupewa taarifa hizo.

Mtaa mwingine ambao kuna mabwawa makubwa ya maji baada ya bomba kupasuka ni mtaa wa Lusaka Tandika Maguruwe karibu na shule ya madrassa DAWASCO wamekuwa wanafika na pikipiki mara na pick up yao na kuondoka bila kuziba hayo mambomba

Kiukweli sijajua tatizo nini kwa hawa DAWASCO kutoyafunga au kuyaziba hayo mambo yaliyopasuka kiasi cha mabwawa kuwepo katika mitaa hiyo na huku wakilalamika kuwa maji yao yanapotea na Waziri wa Maji na umwagiliaji Prof Mbarawa akisisitiza kuangalia chanzo cha DAWASCO kupoteza maji wakatika DAWASCO wenyewe hawawajibi inavyotakiwa katika kuyafunga au kutengeneza mambomba yote yanapopasuka kwa haraka .
 
DAWASCO kimya huku maji yakipotea na kuleta usumbufu kwa wananchi
 
DAWASCO bado maji yanamwagika mitaani...kulikoni je mna mgomo?
 
Back
Top Bottom