Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,930
- 12,216
TAARIFA KWA UMMA
JITIHADA ZA KUPAMBANA NA UPUNGUFU WA MAJI MTO RUVU
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) inawataarifu wakazi wa Bagamoyo hadi Kigamboni wanaohudumiwa na mtambo wa Ruvu Chini kuwa bado kuna hali ya upungufu wa maji katika mto Ruvu kutokana na kiangazi cha muda mrefu.
Ili kuhakikisha kuwa maji kidogo yaliyopo yanafika katika mitambo ili kuchakatwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu, timu maalum ya wataalamu wa Wizara ya Maji na DAWASA imeendelea kuhakikisha kuwa vibali vya watumiaji wengine ikiwa ni pamoja na vya wakulima vinasitishwa.
Aidha shughuli za kunywesha mifugo katika mto pia zimesitishwa.
Kwa kawaida DAWASA huzalisha lita milioni 520 kwa siku, mabadiliko ya hali ya hewa yameathiri mititririko ya mikondo na mito (hususani Mto Ruvu) na kupelekea uzalishaji maji kupungua kwa asilimia 12 ambapo sasa maji yanayozalishwa kwa siku ni lita milioni 460 kwa siku. Kutokana na hali hiyo, maji yamekuwa yakipatikana kwa msukumo mdogo na katika maeneo mengine huduma itatolewa kwa mgawo.
Ili kupunguza changamoto hii, DAWASA imekuwa ikitekeleza mpango wa kuhamisha maji kutoka katika vyanzo vyake vingine ikiwemo, mtambo wa Ruvu Juu, ili kuhudumia maeneo ambayo awali yalikuwa yakipata huduma kutoka katika mtambo wa Ruvu Chini. Aidha vyanzo vyake vingine vya mtambo wa Mtoni pamoja na visima virefu vinaendelea kutoa huduma katika maeneo mengine ya jiji ili kupunguza changamoto ilioyopo.
Kutokana na ukubwa wa mtandao wa DAWASA, ratiba za migawo zinatolewa kwa wananchi kupitia mifumo ya kimawasiliano ya Mamlaka kupitia mikoa yake ya kihuduma ili kuwafikiwa wananchi husika kwa kwa muda muafaka.
DAWASA inaendelea kuwakumbusha wateja na wananchi kwa ujumla kutunza/kukinga maji ya kutosha wakati wa mgawo na kutumia maji kwa uangalifu.
Tupigie kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 na 0735 202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Jamii - DAWASA