DAWASA yaanza kufunga pampu zitakazoimarisha huduma ya maji

DAWASA yaanza kufunga pampu zitakazoimarisha huduma ya maji

DAWASA

Official Account
Joined
Oct 7, 2010
Posts
201
Reaction score
121
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imeanza rasmi zoezi la kufunga Pampu 3 kati ya Pampu 7 zilizowasili mapema Mwezi Mei Mwaka huu zinazotarajia kuimarisha na kupunguza changamoto za kihuduma katika Mikoa ya Dar es salaam na Pwani.

WhatsApp Image 2026-05-27 at 11.09.15.jpeg

Pampu hizo zitakazofungwa katika Mitambo mikubwa ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini zina thaman ya Shilingi Bilioni 16.5 na zimeanza kufungwa kwa awamu kwa kuanzia katika Mtambo wa Ruvu Juu ulioko eneo la Mlandizi Mkoani Pwani.

Akizungumzia zoezi la ufungaji wa Pampu hizo unaoendelea, Meneja wa Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu, Mhandisi Juma Kasekwa amesema jumla ya Pampu tatu mpya zitafungwa mtamboni hapo na tayari wataalamu kutoka China wamefika ili kuhakikisha usimamizi sahihi wa ufungaji pampu hizo.
WhatsApp Image 2026-05-27 at 11.09.15 (1).jpeg

"Pampu zilizofika ni mahususi kwa kuchota maji ghafi kutoka mtoni na kuyasukuma katika mtambo wa kuyachakata/kusafisha maji, huku kuanza kufunga Pampu hizi ni ishara kubwa kwa Mamlaka kuwa sasa tunaenda kupunguza changamoto za kihuduma na kuimarisha huduma kwa kiwango kikubwa, Pampu hizi zitapunguza muda mwingi uliotumika zamani katika matengenezo ya Pampu za awali na zilizochangia kuwakosesha Wananchi huduma,” amesema Mhandisi Kasekwa​
 
Tumewazoea..kinyerez ina mabomba yanaoza
 
Yaani nchi yangu hii ..yaan Kuna sehem nusu kilomita maji yanamwagika mita 300 bomba linaoza. Yaan inafikirisha. Ttumeandika Mkuu Jumaa amekuja, nakumbuka meneja akanunua raia malmluki waje kumshangilia bahat nzur akaambiwa, akamuonya yule jamaa. hadi leo
 
Dawasa miaka yote hamjawahi pata suluhu ya maji.

Hapo August Hadi November tujiandae kukaa nyumba zinanuka uvundo, na rundo nguo chafu, hakuna maji.

Mama ntilie waoshee maji hayo hayo kuanzia asubuhi Hadi Walifunga.
 
Back
Top Bottom