DAWASA yaanza fufua visima kupunguza nakisi ya maji Dar es salaam

DAWASA yaanza fufua visima kupunguza nakisi ya maji Dar es salaam

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza kufufua na kuhuisha visima virefu vya maji ili kupunguza nakisi ya maji ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire ameyasema hayo siku Ijumaa Desemba 12, 2025 katika mkutano wa DAWASA na mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika mkoani Dar es Salaam.

Soma pia: Hii ni Dar na hawa ni wananchi wa Ubungo wakichota maji katika chemchem ya mto Gide



"Kwasasa hivi tunafanya kazi kubwa ya kuendelea kuongeza uzalishaji kupitia visima vya Kimbiji. Katika hali ya kawaida tulikuwa tunaweza kuzalisha karibu lita milioni 17 hadi 20, sasa hivi tunaweka pampu kubwa ambazo zinaweza kuchukua maji mengi kwenye visima vile, kusudi tuongeze ule uzalishaji wa maji kutoka kwenye vile visima", ameeleza Mhandisi Bwire.
 
Hawana lolote zaidi ya kufuga viliba tumbo vyao walivyovibatiza jina takatifu kwamba ni vitambi.
 
Ukanda wa Goba week inaenda ya pili hakuna maji wananchi wanateseka mnoo
 
Back
Top Bottom