Dawa za kulevya: Watanzania watatu wakamatwa India, mmoja afariki

Hivyo basi, kama mtuhumiwa akipewa chakula na kukataa kula inaweza kuwa ni dalili kuwa amemeza vidonge vya dawa za kulevya.
Which means wanawapa chakula ili wakikubali kula wafe, kwa sababu aliyekubali kula alikufa! Kwa sababu madawa na chakula havichangamani!

Baada ya hapo, Watanzania wote watatu walipelekwa mahakamani
Which means Mtanzania wa tatu ambae umesema hakukamatwa alipekwa mahakamani bila kukamatwa!

Hali ya Mtanzania wa pili ilizidi kuwa mbaya na alipelekwa katika hospitali ya JJ.
Sasa huyu ni Mtanzania wa pili ambae yeye alikataa kula wala kunywa lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya, which means kumbe hakuna haja ya kumjaribu mtu kama atakubali kula kwa sababu kumbe ama ule ama usile, ama unywe ama usinywe, ukibeba madawa hali yako itakuwa mbaya anyway, na tunajua atakaekubali kula atakufa!

Mtanzania wa tatu, ambaye ni mwanamke wa makamo, bado anahojiwa na vyombo husika.
Which means huyu wa tatu alikuwa anahojiwa labda kwenye simu au kwa e-mail au kwa mayowe ya mbali mbali kwa sababu umesema waliokuwa wameshikiliwa kuhojiwa ni wawili, mmoja wao yuko ICU mwingine kafa, wa tatu hakushikiliwa!

Upelelezi bado unaendelea kujua kama alikuwa mmiliki wa hizo dawa za kulevya.
Which means alipelekwa mahakani kusomewa mashitaka labda ya kukaa kiti cha karibu na wabeba madawa! Kwa sababu umesema yeye aliambatana tu, na hawajui kama dawa ni zake ama sio zake, na mahakamani akapekwa vile vile!

I mean haya ndio maelezo na tafsiri za waandishi wetu wa nchi kama Tanzania na India, dunia ya tatu, hata kahabari ka madawa ka nusu ukurasa kanatushinda. Mfumo wa elimu ufumuliwe.
 
Watanzania wengi ni wauzaji wa madawa ya kulevya na mtandao wake ni mrefu sana, sijui kufanyike nini ili kupunguza tatizo hili?
 
Inna Lillahi wa inna Illahi Rajjun!!!. Mola atuepushe na aibu za kufa vifo vyenye fedhea kubwa kwa familia zetu!
Sasa Serikali ya India ilipataje hizo taarifa? Kwanini Serikali ya TZ isishirikiane nao ili wakamatwe huku huku?
Wewe unategemea askari wa TZ,wawakamate "mapunda" wa madawa ya kulevya?!

Si tulimsikia wenyewe Kapuya namna alivyotamba,kuwa watoto.wao ndio wahusika wakuu wa biashara za.kulevya,na hakuna mtu yeyote hapa nchini,mwenye ubavu wa kuwakamata,kwa kuwa wao ndiyo wenye nchi!!

Sasa mleta hii habari,ni vyema akatuletea majina ya hao waliokamatwa,inawezekana likawemo jina la mtoto wa Kapuya.

Kwa kuwa ingawa watoto hao wa vigogo hawakamatiki katika ardhi ya TZ,lakini above law hiyo wanayoenjoy watoto hao wa vigogo,inaapply wakiwa hapa TZ peke yake lakini haiwezi kuapply wakiwa ughaibuni!!
 
wangeweza itwist vizuri wanaweza komaa kuwa jamaa ndio wamemuua, kwa vile walimlazimisha kula na hivyo kumuua.Halafu km CCM hazitodanganya basi waendelee kudai hata hizo dawa nazo pia ni matokeo ya kulazimishwa kula na kumeza ,na hivyo hao polisi waeleze walizipata wapi dawa na chakula.

Hapo kwenye green imekuaje panahusishwa kwenye hii mada?
 
Kua suspect ni very subjective, na sio mbaya mtu akachagua randomly nani atahojiwa na nani asihojiwi. Hawawezi kumfunga mtu kabla ya kua na a minimum evidence kua kahusika katika titu kibaya. The scan was enough evidence, they should have started there.
Ila Kuwalazimisha kula na kunywa wamechemka. Na hapo ni wazi kua matendo yao yamesababisha huyo suspect kufa, na mwenzie kuweka maisha yake hatarini. HApa lazima serikali na familia za marhem wawajibishe hao border police.

mind You kila nchi ina sheria zake,hata kama kuna sheria za kimataifa(international laws) zinakinzana na za ndani(domestic law) za ndani ndo zinasimama,huwezi jua sheria za India zinasemaje
 
Mkuu lakini kisheria huwezi kumlazimisha abiria yoyote kula wala kunywa. Miaka michache iliopita nilikataa kula wala kunywa, tena niliwaambia sitaki kusumbuliwa, na ilikuwa ni flight from AMS - LAX. Hakuna alienilazmisha wala kunishuku. Je ni kwanini hawakudhania mimi ni drug mule? Naomba kuelimishwa, manake isijekuwa wanawanyima hawa vijana haki zao kama abiria

Mleta uzi anasema walipewa tip-off; wewe kama ulipona ni bahati yako usirudie tena lakini!

<Jp Omuga>
 
Mleta uzi anasema walipewa tip-off; wewe kama ulipona ni bahati yako usirudie tena lakini!

<Jp Omuga>
Najua haki zangu na siuzi unga. Ole wake mtu yoyote a-assume mimi ni drug mule kwa kuwa nimekataa kula ama kunywa during the flight.
 
Kulingana na hali ya sasa, Tanzania imekuwa kwenye nchi zinazoshukiwa kuwa na mtandao mkubwa wa wauza unga,kwa hiyo upelelezi makini umekuwa ukifanya na taarifa za yeyote anayehisiwa hufikishwa kwenye vyombo vya usalama. Ndani ya flight kuna huduma ya chakula na vinywaji bure, kwa hiyo abiria anayegomea chakula kwa kisingizio chochote huwa ni ishara kubwa sana kuwa suspected na biashara ya dawa za kulevya. Kwa hiyo ni kazi rahisi kwa flight attendant kumripoti ili achunguzwe zaidi.
 
Najua haki zangu na siuzi unga. Ole wake mtu yoyote a-assume mimi ni drug mule kwa kuwa nimekataa kula ama kunywa during the flight.

Sherrif!
Hawa jamaa walishukiwa wakapitia uchunguzi wa awali na vipimo ikabainika walikuwa drug mules isipokuwa yule mwanamke!
Rai yangu ni kuwa muuza madawa/drug mule yeyote asipewe haki yoyote ile!
 
Sherrif!
Hawa jamaa walishukiwa wakapitia uchunguzi wa awali na vipimo ikabainika walikuwa drug mules isipokuwa yule mwanamke!
Rai yangu ni kuwa muuza madawa/drug mule yeyote asipewe haki yoyote ile!
Ninachopinga ni endapo kigezo cha kumshuku abiria kama ni drug mule eti sababu amekataa kula ama kunywa during the flight. Kama kuna sababu nyingine ni sawa lakini sio eti kukataa kula
 
Back
Top Bottom