Dawa ya uchovu jamani

drphone

JF-Expert Member
Sep 29, 2009
3,542
281
jamani naomba dawa ya uchovu yani nasumbuliwa na uchovu kwa mda mrefu sana sijui ni ratiba na kazi yangu kwani nashinda kwenye computer mda mwingi alafu nachelewa sana kulala uchovu wenyewe nausikia zaidi kichwani yani kichwa kinakuwa kizito sana nahisi naumwa ukienda hosptal kila k2 kipo normal unaishiwa kupewa vitamin kilo zimepungua kidogo now ni 105 cjui kama ni tatizo najua hapa kuna wataalamu wengi na nitapa ushauri nasaha karibuni wakuu
 
Kg 105???? Hizo ndizo zinazo kumaliza una urefu gani? Anyway inaelekea umepetwa na fatigue pata ushauri wa kitalaamu na badili lifestyle yako.
 
Uchovu si Ugomnjwa bali dalili kuwa kuna kitu hakipo sawa katika mfumo wako wa mwili au kimaisha.
Kwa maelezo yako ya awali kuna mambo mawili, Kwanza inaonekana hupati muda wa kupumzika kwa kuchelewa kulala. Kwa mtu mzima huhitaji 8 Hrs kwa mapunziko. Ni wazi kbaisa kuwa kama hupati muda huo, usingizi unakuwa ''cummulative'' na kusababisha ujisikie mchovu.
Pili, muda unaoshinda kwenye computer nao inaweza kuwa sababu, mwanga wa computer, umbali kutoka katika monitor, position ya keyboard na kiti chako vinaweza kuwa ni sababu pia. Watu wengi wanafanya makosa ya kutofanya mazoezi hasa wanapokaa katika hizo computer kwa muda mrefu. Hakikisha kuwa kila baada ya saa moja au na nusu una ''bend & strech'' ili kuweka mwili sawa.
Uchovu pia unaweza kuwa dalili ya maradhi kama ya moyo, kisukari, figo n.k, kwahiyo uwe una check mara kwa mara vitu kama Blood glucose level, Urinalysis, Heart. Kwa uzito wa KG 105 kwa Mississipi U.S.A huo ni uzito wa kawaida tu wa teenager, lakini kwa maumbile yetu Watanzania si wengi wanaofikia hapo, ingawa pia sijui umbile lako halisi. Mazoezi kurudisha uzito nyuma kidogo ningeshauri.

Nashauri usitumie dawa za kupunguza maumivu kama wengi wanavyofanya kwani unaweza kuwa tegemezi wa hizo dawa na ukawa umejenga tatizo lingine. Angalia utaratibu wako wa maisha kwa ujumla kama nilivyoshauri. Namaliza uchovu si ugonjwa bali dalili kuwa kuna something is wrong ima kimwili[ Physical/organic functions] au kimfumo wa maisha ( Sleeping pattern, Occupation, Leisure etc etc)
 
Kg 105???? Hizo ndizo zinazo kumaliza una urefu gani? Anyway inaelekea umepetwa na fatigue pata ushauri wa kitalaamu na badili lifestyle yako.

hivi uzito mkubwa ni tatizo nilikuwa na 115 ni mrefu ila sio kama hashim
 
Uchovu si Ugomnjwa bali dalili kuwa kuna kitu hakipo sawa katika mfumo wako wa mwili au kimaisha.
Kwa maelezo yako ya awali kuna mambo mawili, Kwanza inaonekana hupati muda wa kupumzika kwa kuchelewa kulala. Kwa mtu mzima huhitaji 8 Hrs kwa mapunziko. Ni wazi kbaisa kuwa kama hupati muda huo, usingizi unakuwa ''cummulative'' na kusababisha ujisikie mchovu.
Pili, muda unaoshinda kwenye computer nao inaweza kuwa sababu, mwanga wa computer, umbali kutoka katika monitor, position ya kthanx mkuu kwa ushauri mzuri nitafanyia kazi nitaleta feedback
 
Dawa ya Uchovu:

Maziwa Fresh, Glass Mbili kabla hujala kitu na Glass Mbili kabla Hujalala. In between, Asali safi.
 
Dawa ya Uchovu:

Maziwa Fresh, Glass Mbili kabla hujala kitu na Glass Mbili kabla Hujalala. In between, Asali safi.

hiyo ni dawa ya kuleta usingizi labda kama umemaanisha uchovu wake utaisha baada ya kulala.
 
Dawa ya Uchovu:

Maziwa Fresh, Glass Mbili kabla hujala kitu na Glass Mbili kabla Hujalala. In between, Asali safi.

maziwa fresh nitapata org ila asali sina uhakika kupata ambayo aijachakachuliwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom