Dawa ya mdomo...!

Dawa ya mdomo...!

Ahaha akilala wewe unakuwa macho ukifanyaje!???????:heh:
 
Habarini wakuu naombeni msaada kwahili..
Nina mchumba wangu kiukweli yupo vizur na nampenda sana...lakini tatizo linakuja pale anapo lala mdomo huwa anapenda kuuacha wazi, kiufupi anapenda kulala mdomo ukiwa wazi,kitu ambacho mm cpendezwi nacho...swali kwa wataalam kuna dawa yyte anaweza kutumia kubadilisha hali hii?

Kwa baadhi ya watu ni vigumu kujicontrol kwa kulala ukiwa umefumba mdomo kama una tatizo la kulala kinywa kikiwa wazi. Ila kuna baadhi ya vitu vinaweza kusaidia kupunguza au kuondoa kabisa tatizo hilo kama
  • kulala kiubavu ubavu au kulalia tumbo kama alivyosema Kaunga
  • Anaweza kujaribu kutumia 'nasal spray' au decongestant
  • Au pia anaweza kutumia 'nasal strips' ambayo humasaidia mtu kupumua kutumia pua na siyo mdomo
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuwa mtu akilala usingizi anakuwa hajitambui, huenda na wewe unatatizo kama hilo ila yeye anakuvumilia. Si ukimwambia unaweza kushtuka atakpokuonyesha picha aliyokupiga ukiwa umelala mdomo wazi zaidi yake. Usahuri, vumilia tu achana na vitu vidogo vidogo kama hivyo ilmradi tabia na "reception" yake ni nzuri.
 
Mleta mada naomba utambue ,maisha ya mapenzi ni kubebeana mizigo,yaani ishu ya kuacha mdomo wazi tu nayo unaona kero hadi kuileta hapa jamvini ?
We potezea tu, kwanza we badala ya kulala unaanza kumkagua mwenza wako,je na yeye akisema asilale akukague unafikiri yatakosekana mapungufu kweli? Kesho utakuja hapa kutujuza kwamba kaanza kupiga mashuti !!
 
Shukuru wako anaachama tu mdomo mi mbona wangu anaruka sarakasi usiku kucha na nimejizoelea hiyo hali
 
Habarini wakuu naombeni msaada kwahili..
Nina mchumba wangu kiukweli yupo vizur na nampenda sana...lakini tatizo linakuja pale anapo lala mdomo huwa anapenda kuuacha wazi, kiufupi anapenda kulala mdomo ukiwa wazi,kitu ambacho mm cpendezwi nacho...swali kwa wataalam kuna dawa yyte anaweza kutumia kubadilisha hali hii?

Uwe unampaka super glue mnapo enda kulala
 
Mwambie mpenzi wako apende kulala kitumbo tumbo, hii itasaidia kufumba mdomo, pia inasaidia pia kwa wanaokoroma wasikorome, maana inaonyesha huyo mpenzio analala chali.
 
Mkuu,mimi nina swali, Hivi mtu ukiwa unampenda lazima kila kitu chake ukipende? na chochote usichokipenda lazima ukirekebishe?

Binafsi naona,labda uumbe wa kwako kwa ku'customize specifications uzitakazo ndio utapenda kila kilicho chake!
Mengine unatakiwa kuyapotezea na kuvumilia ama kuachana nae kama unadhani huwezi kuendana nayo!

Umenikumbusha JKT wakati wa chakula,unamwambia afande mbona umeniwekea mifupa tupu,anakujibu kama unataka nyama ya ng'ombe hisiyokuwa na mifupa mchole ng'ombe wako.
 
Ahaha akilala wewe unakuwa macho ukifanyaje!???????:heh:

Ni vizuri kumuangalia mpenzi wako akiwa amelala, sura yake ikoje, mimi mwenyewe napenda kumuangalia Mr wangu na huwa nafurahi sana.Naona nimepata Mume bora.
 
Shukuru wako anaachama tu mdomo mi mbona wangu anaruka sarakasi usiku kucha na nimejizoelea hiyo hali

Haahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!! Loh!! ukiwa mgeni si utasema mnapigana humo ndani kumbe mtu anageuka.
 
Habarini wakuu naombeni msaada kwahili..
Nina mchumba wangu kiukweli yupo vizur na nampenda sana...lakini tatizo linakuja pale anapo lala mdomo huwa anapenda kuuacha wazi, kiufupi anapenda kulala mdomo ukiwa wazi,kitu ambacho mm cpendezwi nacho...swali kwa wataalam kuna dawa yyte anaweza kutumia kubadilisha hali hii?
wewe ni jinsia gani?
 
Sidhani kama kuna dawa nijuavyo mimi kuna watu wako hivyo ie ni maumbile. Chaa msingi na wewe usikae macho usiku uwe unalala jamani.
 
Ni vizuri kumuangalia mpenzi wako akiwa amelala, sura yake ikoje, mimi mwenyewe napenda kumuangalia Mr wangu na huwa nafurahi sana.Naona nimepata Mume bora.

Mambo ya aerosmith - don't wanna miss a thing ( BAK ) sio! hata hutamani kulala...eheheh... basi inabidi kila akiwa anamuangalia amfunge mdomo!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom