Mke wangu ana ujauzito wa mwezi mmoja na siku kama saba, siku mbili zilizopita alikuwa analalamika maumivu ya kichwa na uchovu lakini amepima amekuta hana malaria lakini kwa namna alivyojieleza kwa daktari ameelezwa kuwa huenda ana malaria lakini haijaonekana hivyo akashauriwa atumie dawa MSETO
Alizotakiwa kuanza kumeza palepale hospitalini na Amoxilini kwa sababu ya mkojo mchafu. Sasa mke wangu kagoma kuendelea na dozi kwa madai kuwa alishawahi kusoma vijalida mbalimbali vya wataalamu wa afya wakionya juu ya matumizi ya dawa hizo kwa wajawazito kuwa zina uwezo mkubwa wa kudhuru ukuaji wa kiumbe wakati wa ujauzito au kuharibu kabisa ujauzito. Lakini nafahamu pia kuwa malaria ni mbaya sana hasa kwa kina mama wajawazito isipotibiwa ipasavyo mapema.
Tafadhali naombeni ushaurini wenu, dawa hizo kweli zina madhara kama hayo? Na kama ni kweli, itakuwaje wakati kasha anza dozi? Nimejaribu kuwauliza wataalamu wa afya, nao maelezo yao yanatofautiana. Wengine wana sema hazina madhara lakini wengine wanaishia kusema "Mara nyingi wajawazito wa umri huo hawashauriwi sana kutumia MSETO".... Tuko njia panda hasa ukizingatia SP(dawa inayokubalika kitaalamu kwa wajawazito inashauriwa kuanza kutumika kwa wajawazito wenye mimba ya miezi mitatu tu)
Naombeni ushauri wenu tafadhali.
NB. Hospitali aliyoenda ni ya serikali yenye hadhi ya hospitali ya wilaya na iko mjini
Mzizi mkavu, nakutegemea sana mkuu na wengine wote wenye utaalamu wa mambo haya au uzoefu na mambo ya kina mama wajawazito