Dawa ya malaria kwa mama mjamzito

delusions

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2013
Posts
5,001
Reaction score
1,292
Naomba msaada nimepima malaria ninembiwa nina Malaria 2. Nina ujauzito wa miezi mitatu.

Je, naweza tumia dawa gani kutibu malaria nimepima kwenye maabara Hakuna daktari.
=========

Michango:

 
Naomba msaada nimepima malaria ninembiwa Nina Nina Malaria 2 nina ujauzito wa miezi mitatu naweza tumia Dawa gani kutibu malaria nimepima kwny maabara Hakuna daktari

Dada...kipindi cha uja-uzito ni kipindi kinachohitaji umakini sana na kujali afya yako, linapokuja suala la matibabu hasa kwa ugonjwa kama Malaria ambao umo kati ya magonjwa yanayoua wajawazito, kusababisha mimba kutoka, kusababisha upungufu wa damu, na pia hata kudumaza ukuaji wa mimba na mtoto tumboni (kusababisha low birth weight, ambayo huongeza risk ya mtoto kutosurvive)...usifanye utani!

Nenda hospitali kaonane na daktari...kama utagoma kwenda, basi angalau ufahamu tu..kwa mimba hiyo ya miezi mi3...si salama kutumia dawa ya mseto ya Malaria.

NB: Nenda hospitali...na ni kipindi muhafaka kuanza kliniki ya wajawazito.
 
halafu ni vizuri zaidi nenda kachukue clinic zipo SP special kwa wajawazito na zinatolewa kuanzia wk ya 20 lakini wenyewe wanaelewa zaidi jinsi ya kukusaidia usijeenda dispensary au pharmacy watakupa SP za kawaida.

Katika hali ya ujauzito usipende kuuliza ni dawa gani nitumie bali muone dr.tena specialist wa wanawake kuna mtu alipewa kwinini na alimwambia dr.nina ujauzito wa miezi 2 akamwambia hiyo ndo inafaa mimba ikatoka kuwa makini.
 
Hata hivyo sidhan kama huyo mhudumu wa afya ana ujuzi wa afya ya mama mjamzito,mwone tabibu upesi
 
MSAADA WA HARAKA TOKA JF Doctor

Habari wakuu?
Naomba kuuliza dawa ya mwanamke mjamzito wa mwezi mmoja na nusu, je ni dawa gani ya malaria utumia, kwani nimeambiwa mpaka mimba ya miezi 4 nakuendelea unywa dawa hizi za kawaida

Na chini ya miezi 4 ukinywa hizi, eti mimba inatoka..... ?

MSAADA TAFADHARI!!!!
DAWA YA MALARIA MIMBA YA MWEZI 1 1/2.

asanteni.
 
frema 120,

Nenda hospitali umuone dr wa kinamama (gynecology), upate vipimo vyote na utashauriwa ni dawa gani yakutumia kama kweli una malaria, once u find out unamimba nivizuri kwenda kwa Dr (gynecology) kuconfirm the pregnancy napia kushauliwa way forward, mdu huu hutakiwi kunywa dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Nihayo tu.
 
Kawaida katika first trimister first line drug ni quinine japo ckushauri kunywa dawa yoyote hadi ushauriwe na daktari...
 
first trimester ni mimba ndg na ukikosea tu tiba inatoka coz dawa za maralia ni kali..kamuone dokta kwa ushaur zaidi..
 
Ni vizuri kama una-access na hospitali na dr mzuri-ukamwone haraka na ufanye -vipimo kwa uhakika na kupata appropriate medics...
 
Mke wangu ana mimba ya miezi 3 ambapo juzi ameenda hospitali amegundulika ana malaria (wadudu 2).

Sababu kubwa ya kuandika huu uzi ni kuwa amepewa dawa za quinine ambazo zimekuwa zikimsumbua sana,dozi hii kaanza kutumia jana na usiku wa jana hatujalala kabisa maana amekuwa akilalamika tumbo na mwili kiujumla vinamuuma.

Wadau naomba mnisaidie ikiwa kuna dozi nzuri au tiba yoyote mbadala ambayo itaweza mponesha...msaada wenu ni muhimu sana maana nakosa raha kwa jinsi anavyolalamika!!!
 
Hospitali au dispensary hapo mtaani???!!

Mrudishe hospitali akawe reviewed na mtu mwenye uelewa, huyo daktari wako??????!!!!

Malaria 2, ujauzito na dose ya quinine inaacha mengi kufikirika????!!!
 
Malaria ni mbaya kwa mjamzito mrudishe hosp haraka sana..halafu Tafuta Dr specialist wa akina mama amuhudumie wakati wote wa ujauzito wake.
 
Hospitali au dispensary hapo mtaani???!!

Mrudishe hospitali akawe reviewed na mtu mwenye uelewa, huyo daktari wako??????!!!!

Malaria 2, ujauzito na dose ya quinine inaacha mengi kufikirika????!!!

Ni dispensary kaka...halafu huku ambako nipo hakuna specialists, nashindwa nifanyaje kwa wakati husika!!!
 
Malaria ni mbaya kwa mjamzito mrudishe hosp haraka sana..halafu Tafuta Dr specialist wa akina mama amuhudumie wakati wote wa ujauzito wake.

maana nimejishauri sana...halafu hata wakazi wa huku nilipo kwa sasa (kilwa) wao wanona ni jambo sahihi tu!!!
 
Quinine sio nzuri zinatia uziwi na upofu. Huyo Dr kakuandikia izo coz inaonesha ndo walokua wanazo apo dispensary kwao.

Mpeleke hosp nyengine. Au huna hata namba ya simu ya Dr yyt umpigie akushauri? Mjamzito hapewi midawa tu ovyo ovyo
 
Ponjoro,

Pole sana kaka!

Quinine ni moja kati ya dawa za malaria ambazo zimethibitishwa kuwa salama wakati wa ujauzito. Ila jambo moja ambalo nimeliliona katika uzi huu ni kuwa mkeo anapata usumbufu iwapo anatumia Quinine, hivyo basi ulipaswa kumweleza mtoa huduma/daktari juu ya madhara anayopata mkeo anapotumia Quinine, hii imgemwezesha kufikiria dawa nyingine ambayo ingemfaa pia. Kuna thread moja ipo kule JF doctor inaelekeza jinsi ya kujieleza kwa dakatrari-ipitie

Dawa nyingi haishauriwi kutolewa kwa wanawake wenye ujauzito wenye umri wa chini ya wiki 12 (Miezi mitatu)au kitaalam tunasemema first trimester hapa inahusisha dawa nyingi za malaria (Isipokuwa Quinine) na antibaiotiki pia.

Kwa maelezo yako, mkeo ana ujauzito wa miezi mitatu au zaidi (Ameingia second trimester) hivyo anaweza kupata dawa Mbadala wa Quinine

Ushauri wangu

1. Rudi hospitali kwa mtoa huduma/daktari eleza shida anayopata mkeo baada ya kutumia quinine-anaweza kukubadilishia dawa.
2. Kwa uzoefu wangu kwa hali kama hii sindano za artemether zinaweza kufaa (Maana risk ya kutapika haipo na inachomwa mara moja kwa siku na kwa siku 4 tu)
3. Kama hatapiki anaweza kumeza dawa kama ALU, ARCO, Duo-cotexin au artequin-hizi zote zinztaka ushauri wa daktari, hivyo nasisitiza umuhimu wa kwenda tena kwa daktari aone ni dawa ipi inaweza ikamfaa mama kijacho wako!

CC Dr. Preta
 
Last edited by a moderator:
Quinine sio nzuri zinatia uziwi na upofu. Huyo Dr kakuandikia izo coz inaonesha ndo walokua wanazo apo dispensary kwao. Mpeleke hosp nyengine. Au huna hata namba ya simu ya Dr yyt umpigie akushauri? Mjamzito hapewi midawa tu ovyo ovyo

Hapana ndugu

Usipotoshe, maneno ya mitaani yasiyo na scientific proof yasitumike kutoa ushauri. Nimependa ushauri wa kumpeleka mgonjwa hospitali, ila kuhusu Quinine na kuwa ndo dawa pekee waliyokuwa nayo, naomba kupingana nawe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…