Dawa ya Magufuli imeua kupe wengi

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,771
7,138
Wana JF,

Kila kukicha duniani ukosi headline inayomwongelea Dr. Pombe, huyu kweli ni daktari anayeijua kemia ipasavyo kwani katika mchanganyo wake amefanikiwa kupata dawa sahihi inayoua kupe wengi kwa mpigo, wapo maprofesa wengi walipita wakashindwa, hii dawa ya hapa kazi tu, majungu nyumbani kwenu imeanza kupata mafanikio kwani dunia mzima inataka awatengenezee mfumo nzuri wa kuitumia.

Nchi nyingi za kiafrika hazikuwahi kuitumia dawa hii ya mkemia Dr. John Pombe kwani zinaweka ushikaji mbele, Magufuli pamoja na kupata kikombe cha Babu naona kilimwongezea akili za ubunifu katika kutengeneza dawa ya kutibu dunia na haya magonjwa ya uzembe, unyonyaji, ufisadi, ubadhilifu. Kama kawaida yake anasema usifiche ugonjwa njooni akutibu magonjwa yaliyotajwa.

Utawala wa kutii sheria utawaliza wengi kwani watu walichukulia kila kitu poa, jamaa anakuja na mbegu za nchicha, anachimba sehemu na kuzipanda, mchicha na mboga mboga ukianza kukomaa, anajijengea kabanda akijifanya mlizi wa nchicha wake, baada ya muda anapiga tofari kwa faida ya mchicha ule, baadaye anajenga nyumba ya matoleo, na wengine wanafuata, huyo ajiulizi yeye kaingia jangwani mwaka 2005.

Hivi viwanja miaka yote watu hawakuviona mpaka yeye awe wa kwanza. Ifike hatua tuache kulalamika, viwanja viliachwa makusudi wewe ukafanya kiburi eti ukijidai kuwa kwani wakati unajenga hawakukuona.

Magufuri kwa kumtumia Lukuvi vunja vijumba vyote vya jangwani alafu hamia Kunduchi Changalawe, kwani Mwakyembe aliwaambia wasitishe kuchimba kokoto akuwaambia kujenga baada ya zoezi la kusitisha.

Tunashindwa kukusanya kodi, kuweka miundo mbinu kwa kuendekeza ujinga huu wa kwani hawakuniona, sasa waonwe na kijiko wakati wa kubomolewa.
 
Back
Top Bottom