Yoyo na wengine,
Naona nyie wote ni wakuja tu kwenye maswala ya Pombe na athari zake. Si muache tu hiyo kazi ya watu? Kunyweni tu Bia na Kibunango walau zitawafanya muwe mnaongea Kiingereza zaidi na Kisukuma (Masanilo).
Yoyo, Warusi siku hizi wana hela bwana. Nilipata habari hivi juzijuzi maana kuna jamaa yangu Mwanza kaowa Mrusi. Akaniambia kuwa wakati sasa hivi Tanzania tunatamba kwa kuonyesha una gari gani? Warusi wanatamba kwa kuvaa shati lenye nembo inayoonyesha wewe ni Pilot na story ni kuwa ndege yako iko wapi, umesharuka masaa mangapi nk nk. Hivyo wale akina Ibrahimovic achana nao.
Dawa ya Hang-over ni rahisi sana. Ukitaka hata unaweza kufanya majaribio nyumbani. Chukua Pombe kali kama Konyagi na changanya na Acid na utaona palepale hiyo pombe imekuwa diluted na kuwa maji.
Kwa maana hiyo dawa ya Pombe yoyote ili kupunguza makali yake ni LIMAO/NDIMU. Kama huna hivyo vitu basi ni kama walivyosema wengine yaani Apple, maji baridi nk.
Dawa kali kupita zote ni kutokunywa kabisa au kunywa kwa kiasi na siyo kama Wajeruman kwenye October first ambao kabla ya kuanza kunywa hizo Jags za bia, basi wanafunga kabisa suruali chini kwenye viatu ili vitu vyao vibaki ndani ya suruali.