1, ASALI NA LIMAU
Asali na limau ni kinywaji bora kuliko vyote katika tiba hii. Ili kupata ahueni, kunywa mchanganyiko huo mara kadhaa kwa siku.
2. NDIZI MBIVU
Unapozidiwa na kilevi, kiasi kikubwa cha madini ya potassium hupotea, hivyo kwa kula ndizi mbivu kutakusaidia kupunguza makali ya hang-over.
3, TANGAWIZI
Andaa juisi ya tangawizi mbichi na kunywa kama ilivyo, au unaweza kuandaa kwa kukata vipande na uchanganye na maji. Chemsha kwa dakika 10, epua na chuja.
4,HEWA SAFI
Kiasi kikubwa cha oksijeni ingeweza kurahisisha hali ya mgonjwa na kupunguza sumu, kuwa na uhakika wa kushauri kukaa muda mrefu katika viwanja vya wazi, lakini si katika mionzi ya jua.
5, JUISI
Juisi, hasa fresh ya machungwa, husaidia kupandisha kiwango cha sukari kilichopotea na husaidia kuondoa dalili za uchovu mwilini.