Dawa ya kumdhibiti mwanaume asiyeeleweka

Salaam.

Kuna wakati mwanamke unaona mwanaume wako unayempenda na kumuheshimu hakupendi wala kukuthamini kama ilivyokua mwanzo/kabadilika.Na hali hii inawaletea stress wanawake wengi.

Wapo wanawake wakiona tu kidume hakieleweki anasepa zake,which is good for peace of mind ila kama wewe ni kama mimi ambao hatu give up on our men kirahisi au kama umeolewa basi nakushauri ufanye hivii;

1)Kwanza kabisa kama bado unampenda mwanaume wako hata kama anafanya vitendo vinavyokuumiza roho KAMWE USIACHE KUMUHESHIMU,kumuonyesha Upendo na kuwa mnyenyekevu kwake.Ukifanya hivi Mungu hawezi kukuacha uteseke milele maana (Kwa wakristo) neno lake linaagiza kuwa WANAWAKE WATIINI WAUME ZENU.Halijasema akichepuka au akipunguza kukupenda usimtii.Tii hii amri ya Kumtii mwanaume wako nakuhakikishia mwanamke mwenzangu iko siku Mungu atayafuta machozi yako.Hata kama ni jilevi,au stress za kukosa hela au za kuachwa na mcheps wake anakutolea wewe MTII TU,kamwe usimpandishie sauti,kamwe usijibizane nae,kamwe usimuoneshe dharau kwa namna yeyote ile na MARUFUKU KUAHINDANA NAE..Usiache kumuomba msamaha hata kama.umekosa mara moja na yeye kakukosea mara mia moja na hakuomba msamahaAkiharibu hela kwenye pombe na micheps usilipize kwa kuziharibu kwenye vijora au akichepuka na wewe ulipize kwa kugawa kwa mabodaboda, nop.

2)Mwnaume anapopunguza mapenzi na wewe ukilalamikia mabadiliko yake anakuona kero tu.Ukishinda unamuwaza sijui unalia unakonda, unapauka,unazeeka na ndio anazidi kukuona nyanya mbichi.

Dawa ya mwanaume wa hivi ni moja tu shoga angu.TAFUTA MCHEPUKO ANAYEITWA HELA/PESA.

Acha kushinda kumuwaza binadamu asiyekuwaza instead waza na kuwazua jinsi ya kuboresha maisha yako.

Kila akikufanyia kitu cha kukuumiza kifute moyoni mwako kwa kuwaza Idea ya kukuongezea kipato.Akisema atakuja asipokuja,kalala nje,umefuma sms ya mcheps umia kidogo sbb unampenda ila usijilize wala kumlalamikia bali hamisha mawazo yako kwenye kujiboresha kiuchumi.
Hakikisha humuwazi kabisa bali akili na mawazo yako hamishia ktk kujiboresha kiuchumi.Na hizi Hela tukizipata zisifanye tuote mapembe na kumdharau,hapana.Kumbuka biblia inasema tuwatii hata ukiwa na hela mtii, kumtii mwanaume wako ni kumtii Mungu.Hizi hela tunazitafuta sbb mwanamke ni muhimu uwe na kipato chako na mwanamke asiye busy ndo anawaza mapenzi mapenz kila saa.Kila saa unataka upigiwe,kila saa utumiwe text za ailavyuu aimisyuu,umekula nin.Yes wote tunapenda attention hizo ila ukiwa busy hu notice sana kama katext au hajatext.

Ukifanya hivi hata ikitokea siku umechoka kumvumilia utatoka kwenye hayo mahusiano ukiwa umekua kiuchumi na namna nyingine nyingi.Yes kuvumilia kuna kikomo.Hata kama umeolewa kuna stage inafika inabidi utoke ila hakikisha hata ifikie unatoka uwe hujawahi KUMTUKANA,KUMPANDISHIA SAUTI WALA KUMUONESHA DHARAU KWA NAMNA YEYOTE ILE.

PS:Uzi huu hauwahusu wadangaji.
Mnh!
 
Hii haiwahusu wale wanaooa kwa sababu umri umeenda au nae anataka tu awe na mke ila sio kwamba alikupenda!
Ukiolewa na mwanaume wa hivi alafu ufanye kama mleta mada anachosema nakuhakikishia depression will kill you!
Ni kweli do mana nikasema uvumilivu uwe na kikomo mkuu.
 
Back
Top Bottom