Dawa ya CHADEMA yapatikana

Rais alionyesha kwa vitendo akiwa amepiga picha na 50Cent na kuvaa jezi ya Real Madrid

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Ahaa! Kumbe ndo maana sasa kuna kausemi kapya mujini: Ze big result now now.
 

Haitoshi kuonyesha na kuzungumzia mafanikio tu, afterall ndio kazi waliyotumwa kufanya, tatizo ni kwamba haitoshi, kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa zaidi katika dhuluma, kunyonga demokrasia na haki za binadamu, rushwa na ufisadi kuliko huduma za wananchi! Kama wako tayari kubadilika kupambana na maovu Kwa. Dhati then wananchi watwaelewa na kuwa na imani nao na kwa njia hiyo nguvu ya upinzani Na CDM itafifia naturally. Kinachoipaisha CDM ni kukithiri kwa maovu na CCM Kuonekana haiko tayari kuyakomesha sababu kubwa ikiwa ni kwamba viongozi wote wa CCM na serikali yake wote wamekuwa embedded; they are not squeck clean na kwa hiyo hawana moral authority ya kukemea maovu. Dawa ni kuimarisha mapambano towards a new republic
 
Leo wameonyesha mafanikio kwa kuwakamata viongozi wa Chadema wakiwa Iringa!
 
Hawa ccm mbona wanajitesa tu, si wamtumie prof maji marefu???????
 
WAZEE tuliambiwa wanasubiri ''Kufa'' au wameahirisha. Maendeleo tuliambiwa yapo na mfano mzuri na wa wazi ni ''mama lishe'' kumiliki simu au wameongeza zile barabara za wachina zilizo chini ya kiwango.
 

Tupatupa umeniacha hoi hakika .CCM kuachana na vyombo vya dola hawawezi ni sawa na kusema Mugabe asema anaachia madaraka awe Rais mstaafu .CCM bila dola haipo .
 
Matokeo makubwa sasa-Big results now... Na bado watabashir hadi nje ya uwanja, na itakuwa mwisho wao kurudi uwanjani.
 
Na mbona tayari wameishatuonyesha kwa vitendo kwenye ufisadi, kufilisi makampuni na viwanda, madawa ya kulevya, ujangili wa wanyamapori, kuficha mapesa nje ya nchi, na mengine mengi ya jinsi hiyo. Na tumekwisha amua kweli kuwapa kura kama wanavyofikiri wasubiri mwaka 2015 watayaona matokeomazuri ya kuvutia.
 
We wa Sumbawanga hata hapo kwa Aishi hamyaoni mafanikio ya CCM? Tehe....tehe.....sisi huku Mpanda Tunayaona mafaniko ya Said Arf....wala hata hatuhitaji kuoneshwa....yanaonekana yenyewe.....Posuta....!
Tataitu kalesa ...wakata uli? Huyo mbunge wa swanga alisoma na dada yangu pale mazwi sec. kabla hajakimbia shule akiwa fomu 2, akisimulia huyo bwana mambo yake by then hana tofati na leo . Hivi mkoa wa Rukwa tuna wabunge wa aina gani kama vile hatupo watu wa maana ngoja haki ya nani 2015 tuje tupambane atadead mtu hapo
 
Ujangili,kukithiri kwa biashara ya dawa za kulevya,ugaidi,kuporomoka kwa elimu yetu na mengine mengi yanayofanana na hayo ndiyo mafanikio ya magamba. LAANA!!!!!!!!!!!!!
 
Kuonyesha kwa vitendo ni kukomesha madawa ya kulevya, kukomesha ufisadi, kuonyesha uwajibikaji, kuonyesha elimu ya Tz inapaa, madini yetu yameinufaishaje Tz na Watz, misitu, milima, mbuga za wanyama zimeongeza pato gani kwa Taifa na hilo pato limechangia kwa kiasi gani ahueni ya yake "maisha bora as opposed o bora maisha" aliyoahidi baba Rz1.
Kama kweli wanaweza kufanya hayo basi watatuthibitishia Watz kwa matendo the so called "mafanikio" ya Chama cha majambazi aka magamba
 

Shwar mkuu, wafu waachwe wazike wafu wao
 
Huo mradi wakuonyesha mafanikio walishauanza tangu mwaka jana lakini naona ulifeli,

Walijikuta wanaingia gharama kubwa sana kulipia matangazo yao kwenye vyombo vya habari huku wananchi wanazidi kuwakataa,

Tunawasubiri tena karibuni!

Mwenyekiti ambaye ndiye mkuu wa nchi alichagua baadhi ya watu na kuwaweka mwezi mzima sehemu waje na mbinu ya kuleta maendeleo haraka. Kitu kimoja alichoshindwa kukielewa ni kuwa wakati yy akifikiria kuinusuru chama chake hao aliowachagua walikuwa na mawazo yao ya kufuta umasikini wao......matokeo ya haya yote ni kuishia kulaumiana baadaye.

Bibilia inasema wawezaje wawili kutembea pamoja wasipokubaliana? Bila kuwa na msukumo na matamanio y kuwia mamoja hakuna kitakachotoke! Mwenyekiti ajiandaye kupokea matokeo yale yale kama ya kilimo kwanza, mabilioni ya Rais etc!

Kansa ya ufisadi iliyozaa mtoto wa umimi isipotibiwa there would be big failure now badala ya big results now!
 

Tatizo sio kuwaonyesha mafanikio,tatizo ni mafanikio gani ya kuwaonyesha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…