Nani aliyegundua dawa ya binadamu inayoitwa Indomethacin? Ni hatari kwa panya

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
477
1,244
Hii dawa ya vidonge kwa binadamu kutibu maumivu inashangaza sana kwa namna inavyoua panya bila kubakiza hata mmoja.

Siku za karibuni nilijikuta nimevamiwa na panya zaidi ya 20 na kuzaliana ndani mwangu na kuniharibia mazao, nguo na kuwa kero ndani, nikaanza kutafuta dawa ya kuua, nikaenda dukani kununua rat and rat nikaweka nikaambulia sifuri, hakufa hata mmoja.

Nikauliza watu nifanyeje panya wananisumbua hatari wakanambia nenda duka la dawa nunua dawa inaitwa Indocini changanya na unga halafu leta taarifa baada ya wiki, aisee kweli hakuna panya hata mmoja ndani.

Nimejaribu kuulizia nani aliyegundua hii dawa kwa panya ni funga kazi na wenyewe wamesema waliambiwa na wengine.

Je, ni nani hasa aliyegundua hii na kufanyia majaribio kwa panya na kugundua ni hatari, kwa nini asijitokeze apewe cheti?
 
nenda duka la dawa nunua dawa inaitwa Indocin changanya na unga halafu leta taarifa
Ukute Kuna mtu alitunza dawa zake panya wakadokoa kama kawaida yao, halafu wakakata moto.
1686894627539.png
 
Hii dawa ya vidonge kwa binadamu kutibu maumivu inashangaza sana kwa namna inavyoua panya bila kubakiza hata mmoja.

Siku za karibuni nilijikuta nimevamiwa na panya zaidi ya 20 na kuzaliana ndani mwangu na kuniharibia mazao, nguo na kuwa kero ndani, nikaanza kutafuta dawa ya kuua, nikaenda dukani kununua rat and rat nikaweka nikaambulia sifuri, hakufa hata mmoja.

Nikauliza watu nifanyeje panya wananisumbua hatari wakanambia nenda duka la dawa nunua dawa inaitwa Indocini changanya na unga halafu leta taarifa baada ya wiki, aisee kweli hakuna panya hata mmoja ndani.

Nimejaribu kuulizia nani aliyegundua hii dawa kwa panya ni funga kazi na wenyewe wamesema waliambiwa na wengine.

Je, ni nani hasa aliyegundua hii na kufanyia majaribio kwa panya na kugundua ni hatari, kwa nini asijitokeze apewe cheti?

Yaani dawa ya binadamu iwe ni sumu kwa panya anapoila ??!--- binadamu akiimeza sio sumu ila panya akimeza/akila ni sumu?!!😏

Acheni masikhara.
 
Dawa nyingine hatari ni cement ukitaka kuua panya wengi maeneo makubwa mfano shambani.
Chukua simenti changanya na nafaka kavu walayo panya kisha weka kwenye eneo la panya weka maji karibu,panya atakula nafaka yenye vumbi la simenti,simenti inaleta kiu atakimbilia kunywa maji,simenti tumboni itaganda ikiganda itaharibu digestive system ya panya kisha panya watakufa
 
Yaani dawa ya binadamu iwe ni sumu kwa panya anapoila ??!--- binadamu akiimeza sio sumu ila panya akimeza/akila ni sumu?!!

Acheni masikhara.
Ni kweli inaua panya kikamilifu. Ilishapigwa marufuku kutumiwa na binadamu. Na hata kwenye maduka ya dawa inauzwa kimagendo kwa sababu ya kuulia panya na siyo kwa matumizi ya binadamu, mbona hata hao wafamasia wanalijua hilo!

Ukienda famasi ukamkuta muuzaji mkongwe ni lazima akuulize, unataja kwa ajili ya matumizi gani? Ukimwabia unataka unywe wewe hakupi. Wanajua ni kwa ajili ya panya

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
katika kutengeneza madawa yoyote mnyama wanaomjaribishia kuhusu pharmacokinetics, bioavailability, pharmacodynamics huwa wanamtumia panya mkuu
 
Back
Top Bottom