Dawa au mafuta ya kuondoa nywele kichwani.

Arch Barrel

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2024
Posts
533
Reaction score
1,225
Habari za jioni wanajamvi, naomba niende moja kwa moja kwenye maada.
Nina miaka 32, jinsia yang n Me, nimekumbana na changamoto ya kuota kipara mapema sana kuanzia kwenye komwe mpaka kisogoni, kwa bahati mbaya zaidi nywele za pembezoni mwa kichwa zinaota na kustawi haraka sana kila ninaponyoa.
Nimekuwa mtumwa wa kwenda saloon kila baada ya siku tatu tafauti na hapo kichwa kinakuwa kwenye muonekano wa ajabu sana.
Wakuu naomba kama kuna mdau anajua dawa au mafuta ya kuondoa nywele zote moja kwa moja zisiote tena naomba anisaidie. Naomba sana wakuu.
Ahsanten
 
Mkuu usikate tamaa mapema, dawa imepatikana
 
Dah, mkuu hiki ni kitendo ambacho sijawahi hata kukiwaza akilini mwangu na sijawahi hata kujaribu kufanya hivyo.
Nisaidie dawa kama ipo mkuu
Wakuu
 
Attachments

  • 17453385049541559159308966176411.jpg
    17453385049541559159308966176411.jpg
    435.6 KB · Views: 23
Naomba sana wakuu.
Ahsanten

Tumia dawa hii iliyofanyiwa utafiti kisayansi utupe mrejesho :

TAWIRI YAGUNDUA DAWA YA ASILI YA KUOTESHA NYWELE NA KUZUIA NYWELE KUKATIKA​

Aprili 22, 2025

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania(TAWIRI) imegundua dawa ya kuotesha nywele au kuzuia nywele kutoka kwa binadamu kutokana na mimea inayotumika kama tiba asili ugunduzi huo ulianza mwaka 2013 na kukamilika mwaka huu katika mimea inayotumika kwa tiba asili katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania katika wilaya za Ngorongoro, Mbulu na Hanang kwa watu jamii ya Masai, Hadzabe, Datoga na Iraqw.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Arusha 21 Aprili 2025 kuhusu ugunduzi wa dawa ya kuotesha nywele au kuzuia nywele kutoka kwa kutumia mmea uitwao Mporojo, Mkurugenzi wa Utafiti kutoka TAWIRI, Dkt, Julius Keyyu amesema taasisi hiyo imefanya utafiti kwa kipindi cha miaka 12 na hatimaye imepata dawa hiyo ya watu wenye changamoto za vipara pamoja na nywele kutokuota
Dk, Keyyu alisema mmea huo kwa kiingereza unaitwa wormwood albizia, bitter false thorn, jina la kisayansi unaitwa Albiziaanthelmintica na kwa Kimasai unaitwa Ormuktan ambapo wamasai wanatumia magome na mizizi yake kutibu minyoo, malaria na maumivu ya miguu, mgongo na misuli.

Alisema Utafiti huu ulikwenda zaidi ya matumizi haya na kugundua uwezo wa mmea huu kuotesha nywele au kuzuia nywele kutoka na tayari umepata hati miliki (Hataza) hii inaitwa ‘Composition for Hair Growth Stimulation or Hair Loss Prevention Using an Extract of Albizia anthelmintica’.

Alisema Tawiri ni taasisi ya wanyamapori lakini pia inapofanya tafiti hizo inakwenda sanjari na mimea na ndio maana wamebaini mmea huo wa Mporojo unasaidia nywele kuota na kukua zaidi kwa wale wenye changamoto za kutokuota nywele kwa wanawake na wanaume.

Alisema gharama yake ni kwa shampoo ni shs. 31,000 na shs. 75,000 mafuta sawa na dola 12 kwa shampoo na dola 24 kwa mafuta kwa jumla na upande wa rejareja ni shs. 76,000 kwa shampoo na shs. 152,000 kwa mafuta endapo wakipata mawakala wa ndani na nje ya nchi baada kusaini mkataba wa makubaliano kati ya TAWIRI na mawakala.

Alisema teknolojia ya Hataza hii imetolewa (patent transfer) kwa kampuni ya Winwik Enterprise co. ltd ya Korea Kusini ambayo ni watengenezaji wa Kimataifa wa dawa na vipodozi.

"Tayari kampuni hii imeshatengeneza dawa ya kuotesha nywele (Albizia Hair Loss Care) katika mfumo wa Shampoo (shampuu ya wanawake na wanaume), Dawa(Treatment), na Mafuta (Hair Essence Tonic),Dawa/ vipodozi hivi vitaanza kupatikana kwa bei ya jumla kwa mawakala na pia rejareja hivi karibuni."

Alisema utafiti wa jinsi ya kuotesha Mporojo (propagation) kwa ajili ya kilimo umeanza ili kuzuia mmea huu kutoweka kutokana na uvunaji wa magome kutoka mimea iliyopo porini
Alisema lengo la utafiti huo lilikuwa kufanya ugunduzi wa dawa na vipodozi kutokana na bioanuwai ya mimea inayotumika kwa tiba asili na pia kubaini mimea inayotumika kwa tiba asili ambayo iko katika hatari ya kutoweka ili kuihifadhi katika bustani za mimea au ‘botanical garden’.

Alisema kutokana na utafiti wa bioanuwai ya mimea inayotumika kwa tiba asili, watafiti wa Tawiri wamepata Hataza tatu za ugunduzi wa dawa au vipodozi asili ambazo ni dawa hiyo ya kuotesha nywele au kuzuia nywele kutoka kwa kutumia mmea uitwao Mporojo Alisema dawa ya ya kuotesha nywele (Albizia Hair Loss Care) imetengenezwa katika mfumo wa shampoo (shampuu ya wanawake na wanaume), dawa (Treatment), na Mafuta (Hair Essence Tonic).

Alisema dawa na vipodozi hivyo vitaanza kupatikana kw bei ya jumla kwa mawakala na pia rejareja hivi karibuni kwanni dawa au vipodozi hivi vinatumika kuotesha nywele, kuboresha, kuimarisha nywele (zisikatike, kuwa nyingi), kuzuia nywele kutoka (kuzuia kipara), au kuondoa kipara.

Aidha, kutokana na utafiti huo, taasisi hiyo pia imepata hataza nyingine mbili kutokana na bioanuwai ya mimea inayotumika kwa tiba asili ambazo ni ugunduzi wa kipodozi cha kung’arisha ngozi na kuondoa makunyanzi kwa kutumia mmea wa Mugufe.

Alisema Mmea huo kwa kiingereza unaitwa Evergreen shrub,blue bush cherry, na kwa jina la jina la kisayansi la mmea huu unaitwa Maerua edulis ambapo mmea huu kwa Kidatoga unaitwa Ekwida na jamii hii inatumia majani yake kutibu minyoo, tumbo na ngiri

Alisema utafiti huo ulikwenda zaidi ya matumizi haya na kugundua uwezo wa mmea huu katika kung’arisha ngozi na kuondoa makunyanzi na kuongeza kuwa Teknolojia ya hataza hii bado haijanunuliwa au kupewa kampuni yoyote, hivyo bado taasisi na washirika wake wanaendelea kuitangaza ili kupata atakayeihitaji ili kutengeneza kipodozi cha kung’arisha ngozi na kuondoa makunyanzi.

Pia wamegundua dawa nyingine ya tatu ambayo ni dawa ya kuotesha nywele au kuzuia nywele kutoka kwa kutumia mmea uitwao Chimbulei (Kigwala, Mphata na kuongeza kuwa mmea huo kwa kiingereza unaitwa Apple leat, broadlance-pod na kwa jina la kisayansi unaitwa Lonchocarpus eriocalyx.

Alisema mmea huo kwa Kisonjo unaitwa Ekurehe ambapo Wasonjo wanatumia magome na mizizi yake kutibu kikohozi na mafua kwani utafiti huu ulikwenda zaidi ya matumizi hayo na kugundua uwezo wa mmea huu kuotesha nywele au kuzuia nywele kutoka.

Kwamujibu wa Dk, Keyyu alisema teknolojia hiyo bado haijapewa kampuni yoyote, hivyo bado taasisi na washirika wake wanaendelea kuitangaza ili kupata atakayeihitaji ili kutengeneza dawa ya kuotesha nywele au kuzuia nywele kutoka.

Wakati huo huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri, Rogastian Msafiri alisisitiza utafiti huo ni nyota njema kwa nchi ya Tanzania katika kuhakikisha ataza mbalimbali zinalindwa ili kuhakikisha mimea asil8 inatunzwa na watafiti kufanya tafiti mbalimbali na kuja na matumaini mengine kwa jamii na wanyamapori
 
Hii dawa inapatikana duka gani mpaka sasa?
 
Tanzania wameshindwa kabisa kupromoti na kuzalisha kwa wingi bidhaa hii sokoni ndani na nje kupata utajiri. Watu wengi wenye matatizo ya nywele kuto kukua kwa wingi au vipara ni soko kubwa sana duniani ikiwemo ndani ya Tanzania
 
Ni kweli aise, hii dawa wala hawakuhitaji kutumia nguvu, ilikuwa ni kuitangaza tu ijulikane basi
 
Back
Top Bottom