Davos, Uswis: Rais wa Marekani Donald Trump ateta na Rais Kagame. Amtuma salamu za upendo barani Afrika

Kila kitu kilichopo Rwanda ni kivutio cha Utalii,
Mkuu utalii siyo lazima kwenda kuangalia vivutio kama mbuga za wanyama na milima,
Historia ya nchi ya Rwanda ni kivutio tosha kwa watu kutoka Barani Ulaya na Marekani.
Elimu, Tamaduni na Dini ni moja ya vivutio vikubwa sana vya utalii......
wale madem zao dah mi lazima nkatalii
 

Rais wa Marekani Donald Trump amemuomba Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kufikisha salamu zake kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.

Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi pambizoni mwa mkutano wa viongozi na watu mashuhuri kuhusu uchumi na biashara duniani.

Mkutano huo wa Kagame na Trump umetokea wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kuyaeleza mataifa ya Afrika kama "machafu" au mataifa ya "mabwege".

Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana.

Bw Trump amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyaelezea mataifa ya Afrika.

Hata hivyo alikiri kwamba alitumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.

Lakini katika mkutano wake na Kagame pambizoni mwa Mkutano wa Uchumi wa Dunia mjini Davos, Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika.

Bw Trump ameeleza mkutano wake wa leo na Kagame kama "wa kufana sana", na kueleza nchi hizo mbili kama washirika wa kibiashara ambao wanajivunia "uhusiano mzuri sana."

Ameongeza: "Ningependa kukupongeza, Bw Rais, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa … najua unaenda kuhudhuria mkutano wa kwanza karibuni. Tafadhali, fikisha salamu zangu."

Rais Kagame alisema wameshauriana kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa Marekani kwa Rwanda katika "operesheni zake kote duniani", pamoja na masuala ya kiuchumi, biashara, uwekezaji na idadi ya watalii wa Marekani wanaozuru Rwanda, ambayo inaongezeka.

Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa AU utafanyika Jumapili na Jumatatu.


Chanzo: BBC
mtu amekuita shithole alafu bado unaenda unajichekesha kwake. Kweli hii ni aibu kubwa. Rais wangu magufuli hawezi kufanya mambo ya kijinga kama hivyo
 
davos napo mzee baba kagoma kwenda,nani kamuwakilisha..???..
mr.slim akirudi atakuja kumpa ronja mzee baba kilichojili...ye si muoga wa kuchanganyika na watu wupe kushare ideas..
 
Kila kitu kilichopo Rwanda ni kivutio cha Utalii,
Mkuu utalii siyo lazima kwenda kuangalia vivutio kama mbuga za wanyama na milima,
Historia ya nchi ya Rwanda ni kivutio tosha kwa watu kutoka Barani Ulaya na Marekani.
Elimu, Tamaduni na Dini ni moja ya vivutio vikubwa sana vya utalii......
Waelimishe, pigs makofi
 
Sichonje yupo busy kuhonga na kuhamisha madiwani wa upinzani wahamie ccm,wakat wenzake wanapata exposer na kutengeneza status,
Hata siku mmja huwezi linganisha mtu anaetembea na aliyekaa ndani
 
Sichonje yupo busy kuhonga na kuhamisha madiwani wa upinzani wahamie ccm,wakat wenzake wanapata exposer na kutengeneza status,
Hata siku mmja huwezi linganisha mtu anaetembea na aliyekaa ndani


True!..it's weird hataki kutembea.
 
Back
Top Bottom