Davos, Uswis: Rais wa Marekani Donald Trump ateta na Rais Kagame. Amtuma salamu za upendo barani Afrika

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_99760076_8fcb719e-48ce-478f-a632-a8322e234ef4.jpg

Rais wa Marekani Donald Trump amemuomba Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kufikisha salamu zake kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.

Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi pambizoni mwa mkutano wa viongozi na watu mashuhuri kuhusu uchumi na biashara duniani.

Mkutano huo wa Kagame na Trump umetokea wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kuyaeleza mataifa ya Afrika kama "machafu" au mataifa ya "mabwege".

Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana.

Bw Trump amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyaelezea mataifa ya Afrika.

Hata hivyo alikiri kwamba alitumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.

Lakini katika mkutano wake na Kagame pambizoni mwa Mkutano wa Uchumi wa Dunia mjini Davos, Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika.

Bw Trump ameeleza mkutano wake wa leo na Kagame kama "wa kufana sana", na kueleza nchi hizo mbili kama washirika wa kibiashara ambao wanajivunia "uhusiano mzuri sana."

Ameongeza: "Ningependa kukupongeza, Bw Rais, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa … najua unaenda kuhudhuria mkutano wa kwanza karibuni. Tafadhali, fikisha salamu zangu."

Rais Kagame alisema wameshauriana kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa Marekani kwa Rwanda katika "operesheni zake kote duniani", pamoja na masuala ya kiuchumi, biashara, uwekezaji na idadi ya watalii wa Marekani wanaozuru Rwanda, ambayo inaongezeka.

Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa AU utafanyika Jumapili na Jumatatu.

Chanzo: BBC
 
Kwa hiyo atamsaidia katika operesheni ya kujenga BAHIMA empire, maana kasema operesheni zote duniani.TWAFAA.
 
nimeona rockets imepita anga za juu nikadhani inaelekea marekani
 
Hivi Rwanda kuna vivutio gani vya utalii? Nimeshangazwa kuona wamesema “watalii kutoka marekani wameingezeka”

Kila kitu kilichopo Rwanda ni kivutio cha Utalii,
Mkuu utalii siyo lazima kwenda kuangalia vivutio kama mbuga za wanyama na milima,
Historia ya nchi ya Rwanda ni kivutio tosha kwa watu kutoka Barani Ulaya na Marekani.
Elimu, Tamaduni na Dini ni moja ya vivutio vikubwa sana vya utalii......
 
Nafahamu utalii siyo mbuga za wanyama na milima, that was too easy. I don’t like easy stuff.

I just wanted to know what type of tourism in Rwanda there is.

I thought the historic one was a long shot. Hotel Rwanda movie iliwafungua macho kuhusu genocide.

Ujerumani huwa wanaenda kwenye holocaust memories. Hata places like Bagamoyo na huko Zenji.

Yote hayo bado nashangazwa kidogo na watalii wengi kuongezeka huko.
 
Rwanda kuna Dark Tourism
 
Hivi kulikuwa hakuna njia nyingine ya kuonyesha Rais ametoa msaada kwa ndugu yetu Wastara bila kutuonyesha yale mabunda ya pesa ?

Au ndio ushamba aliosema zitto?
 
Nafahamu utalii siyo mbuga za wanyama na milima, that was too easy. I don’t like easy stuff.

I just wanted to know what type of tourism in Rwanda there is.

Hapana hukuuliza hivi,
Uliuliza kuhusu vivutio vya Utalii na siyo aina ya Utalii.
Ulisema hivi "Hivi Rwanda kuna vivutio gani vya utalii?" (Umeona tofauti Mkuu??)
Na mimi nikakujibu kwamba kila kitu kilichopo Rwanda ni kivutio cha utalii....

NB: Tukirudi kwenye swali lako sasa.
"I just wanted to know what types of Tourism in Rwanda there is"
Hapa jibu ni moja tu: All three types of tourism are prevalent in Rwanda....
 
Mauwaji ya kimbali Rwanda ni chanzo kikubwa cha utalii, vitu vingi vimehifadhiwa na watu hutembelea kushuhudia hivyo vitu
 
Maongezi ya ushirikiano wa Nchi hizo mbili.
Biashara, Uchumi na, RWANDA
Uwekezaji na, RWANDA
Utalii na, RWANDA

The rest of African Reps wamepewa Hi.
Nikafikiri ni mkutano na Kagame as AU Chair.
Ndio maana ya shithole leaders from shithole countries yamejaa ubinafsi na udikteta
 
Hapana hukuuliza hivi,
Uliuliza kuhusu vivutio vya Utalii na siyo aina ya Utalii.
Ulisema hivi "Hivi Rwanda kuna vivutio gani vya utalii?" (Umeona tofauti Mkuu??)
Na mimi nikakujibu kwamba kila kitu kilichopo Rwanda ni kivutio cha utalii....

NB: Tukirudi kwenye swali lako sasa.
"I just wanted to know what types of Tourism in Rwanda there is"
Hapa jibu ni moja tu: All three types of tourism are prevalent in Rwanda....
Sasa kama swali lilikuwa rahisi hivyo mbona umelicomplicate jibu lake? Pengine ukajibu ambacho hakikuulizwa?

Ungetaja tu hivyo vituo vya utalii kama unavifahamu.

Kusema “kila kitu kilichopo Rwanda ni kivutio cha utalii”, hilo nalo siyo sahihi.u

Ebu ziainishe hizo “three types of tourism” zilizopo Rwanda na mifano yake.
 
Mafuvu ya binadamu wa genocide
I still don’t buy it. There gotta be something more than that behind the scenes.

Hayo mafuvu ndo yamefanya watalii waongezeke?

Kumbuka kwenye statement hiyo hiyo, “wawekezaji kutoka marekani nao wameongezeka”
 
Back
Top Bottom