Davis Mosha aliwahi sana kutangaza kustaafu siasa

mezakuu

Senior Member
Apr 19, 2016
156
131
Ni wazi kwa jinsi hali ilivyo na hii kasi ya jpm na wana Moshi walivyokuwa maopportunist mbunge wetu mpendwa bwana Jafary Michael hatakuwa na chake wakazi wa Moshi ifikapo 2020.

Wanamoshi watahitaji mtu makini mwenye ukaribu na chama tawala ili watatuliwe shida zao na itakuwa muda muafaka kwa CCM kuchukua lile jimbo lililoporwa muda mrefu hivyo bwana Davis Mosha (the tycoon) kijana mwenye mapenzi mema na Moshi angekuwa ndio chaguo sahihi kwani alikuwa radhi kutumia pesa yote ipatikanayo na malipo ya ubunge kuendeleza jimbo.

Ingekuwa busara kama wakuu wengemwendea na kumuomba akagombee upya 2020.
 
Wakuu ni maoni tu sijawahi kula hata shs 100 ya mosha ila jamaa alikuwa na mipango mizuri na lile jimbo basi tu watanzania waga tunaendeshwa na uchama zaidi sio sera
 
Ni wazi kwa jinsi hali ilivyo na hii kasi ya jpm na wana moshi walivyokuwa maopportunist mbunge wetu mpendwa bwana Jafary michael hatakuwa na chake wakazi wa moshi ifikapo 2020 wana moshi watahitaji mtu makini mwenye ukaribu na chama tawala ili watatuliwe shida zao na itakuwa muda muafaka kwa ccm kuchukua lile jimbo lililoporwa muda mrefu hivyo bwana david mosha (the tycoon) kijana mwenye mapenzi mema na moshi angekuwa ndo chaguo sahihi kwani alikuwa radhi kutumia pesa yote ipatikanayo na malipo ya ubunge kuendleza jimbo.ingekuwa busara kama wakuu wengemwendea na kumuomba akagombee upya 2020.
wewe unachekesha 2020 unaongelea leo!!! na pia sio kazi ya mbunge kutumia pesa zake binafsi kwa ajili ya jamii, nini maana ya kodi zinazotozwa, wewe umetumwa humu....
 
Mkuu manny pacquiao alivyojenga nyumba kwa ajili ya raia wake alitumia pesa za jimbo ni mapenzi yake tu na jimbo watu wapo committed na kubadilisha maisha ya wananchi wao
 
Wakuu ni maoni tu sijawahi kula hata shs 100 ya mosha ila jamaa alikuwa na mipango mizuri na lile jimbo basi tu watanzania waga tunaendeshwa na uchama zaidi sio sera
subiri 2019 ndio uanze ushawishi,jimbo lina watu wengi sana wanaweza kugombea, hata mbunge mpya bado hatujaanza kumpima maana bunge ni la juzi tu.
 
Wakuu ni maoni tu sijawahi kula hata shs 100 ya mosha ila jamaa alikuwa na mipango mizuri na lile jimbo basi tu watanzania waga tunaendeshwa na uchama zaidi sio sera
hahahaha! hata JK alikuwa na mipango mizuri sana kwa tz, na akapewa nchi! ila mpaka leo Kigoma haifanani hata kidogo na Dubai, Kagera hakuna uwanja wa ndege wa kimataifa, ziwa Victoria hakuna meli mpya kubwa, umeme bado unasumbua, sio kila mtanzania ana maisha bora......! hahahaha!! siasa bwana!
 
Mkuu manny pacquiao alivyojenga nyumba kwa ajili ya raia wake alitumia pesa za jimbo ni mapenzi yake tu na jimbo watu wapo committed na kubadilisha maisha ya wananchi wao
ah!! kumbe umekuja kafananisha ya bondia wa nje na wabunge wa tz!!
 
Hii mentality ya kwamba ni lazima uwe karibu na chama tawala ndio maendeleo yapatikane sijui itakufa lini ,Kaskazini washashtuka zamani sana na ni mwendo wa maendeleo kwa speed 120 ,vipi Dodoma na Shinyanga kwenye ngome yenu kuna maendeleo gani ??
 
ah!! kumbe umekuja kafananisha ya bondia wa nje na wabunge wa tz!!
Ni mfano tu huo mkuu kukuonyesha maendeleo hayapaswi kusubiri pesa za jimbo kama mbunge una uwezo unaweza saidia jimbo lako hela yenyewe ya jimbo haitoshi kutatua matatizo yote ya jimbo
 
bondia kasaidia kabla ya kuwa mwanasiasa! hapa wanasaidia wakitaka kura, mosha alitaka kura, sasa umemuona tena?
 
Huyu mleta mada naye mlevi tu.
Kuwapulizia akina mama lishe pilipili machoni ndiyo kuwa na malengo?
Mosha hafai na hatakiwi hata sura yake ionekane huku Moshi hana radhi ya wazazi.
Kilimanjaro watu tunaelewa tunachokifanya wewe kamwambie huyu aliyekutuma aendelee kuuza pilipili hapa sio
mahali pake...MOSHI INA WENYEWE.
 
Wakuu ni maoni tu sijawahi kula hata shs 100 ya mosha ila jamaa alikuwa na mipango mizuri na lile jimbo basi tu watanzania waga tunaendeshwa na uchama zaidi sio sera
Angekuwa na mipango mizuri basi angepita awe mbunge but wananchi waliamua kumchagua yule wa chadema kwa vile anafaa kwa wakati huu.
 
Davis Mosha (the tycoon) kijana mwenye mapenzi mema na Moshi angekuwa ndio chaguo sahihi kwani alikuwa radhi kutumia pesa yote ipatikanayo na malipo ya ubunge kuendeleza jimbo.

Tumeona mara nyingi kuwa hizi ahadi huwa hazitimizwi baada ya hawa waheshimiwa kuchaguliwa!! Chezea siasa ww!!
 
Ni wazi kwa jinsi hali ilivyo na hii kasi ya jpm na wana Moshi walivyokuwa maopportunist mbunge wetu mpendwa bwana Jafary Michael hatakuwa na chake wakazi wa Moshi ifikapo 2020.

Wanamoshi watahitaji mtu makini mwenye ukaribu na chama tawala ili watatuliwe shida zao na itakuwa muda muafaka kwa CCM kuchukua lile jimbo lililoporwa muda mrefu hivyo bwana Davis Mosha (the tycoon) kijana mwenye mapenzi mema na Moshi angekuwa ndio chaguo sahihi kwani alikuwa radhi kutumia pesa yote ipatikanayo na malipo ya ubunge kuendeleza jimbo.

Ingekuwa busara kama wakuu wengemwendea na kumuomba akagombee upya 2020.

nilimshusha sana Mosha pale alipotumia mamilioni ya pesa kuhakikisha anakutana na Suge knight mtu mwenye kashfa kibao za kuuza unga na mauaji
 
Attachments

  • mosha.JPG
    mosha.JPG
    99.1 KB · Views: 148
Back
Top Bottom