Davis Mosha afuturu na watoto yatima

Jul 19, 2020
32
150
Mfanyabiashara Davis Mosha leo amekutana na Watoto wa Kituo cha Watoto yatima cha Sinza na kufuturu nao Nyumbani kwake Mikocheni, Davis leo alipata wasaa huo wa kukaa na watoto hao na kupata futari pamoja huu ukiwa ni utaratibu wake kwa Miaka kumi sasa.

Akizungumza baada ya Futari na Duah iliyosomwa na watoto hao Davis alishukuru kwa watoto hao kuendelea kutunzwa katika maadili mema na kuweza kuwa na furaha wakati wote. "Nimefarijika sana kuwa nanyi leo, Nimekua nikiwatumia Chakula na mahitaji mkiwa kituoni ila leo kwa mara nyingine tumekutana hapa kwa Futari na kupeana Mkono wa Eid, Napenda kuwambia Mwaka huu nimeongeza kituo kingine kama ninyi kilichopo Kibaha Eneo la Misugusugu na juzi tulifuturu nao katika kituo chao. Kwa sasa nina familia kubwa na imeongezeka mkiwa pamoja na watoto zaidi ya mia sita wa kule Moshi Mkoani Kimanjaro ambao nao nimeweza kuwapa futari na kuwapa mkono wa Eid kama kawaida yetu" Alisema Davis Mosha.

Davis Mosha aliendelea kuwatia moyo watoto hao na kuwasihi waongeze juhudi katika Masomo na pia alitoa nafasi za kazi kwa vijana waliomaliza Masomo ambao wamelelewa katika Kituo hicho.

Mimi na familia Yangu tunawapenda sana, na Nitaendelea kuwa nanyi katika Maisha yangu yote na tutaendelea kuhakikisha tunakua sababu ya Tabasamu lenu na daraja la kukamilisha Ndoto zenu." Alimaliza kusema Mfanyabiashara huyo.

IMG-20210512-WA0000.jpg
IMG-20210512-WA0010.jpg
 

Toxic Concotion

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
2,646
2,000
Inasikitisha kwa wanaojiita waislam wanashindwa kufuata kanuni hasa ya kufuturisha, ambayo ni kumlisha yule asiejiweza/mwenye uhitaji.

Unakuta wasanii wanasema wanafuturisha lakini wanajaa mashoga na wakata viuno ilhali kuna watoto yatima wengi wangeridhika na robo ya chakula wanacholishana wao kwa wao wenye uwezo.

Mungu amzidishie Bw. Mosha kwa alichofanya.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,119
2,000
Zilipendwa huyu. Hatawasahau moshi mjini 2015 walivyokula hela zake na ubunge asipate.

Mwizi wa kiboriloni aliibiwa mchana kweupe na wapiga kura. Kula kwa davie mosha ila kura kwa chadema.
Sure ila ni mwana Yanga safi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom