• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

David Kafulila: Uzoefu wa IMF kupika takwimu za uchumi inapotofautiana na Serikali husika

Tumbo Tumbo

Tumbo Tumbo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Messages
1,283
Points
2,000
Tumbo Tumbo

Tumbo Tumbo

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2018
1,283 2,000
MAONI YA DAVID KAFULILA KUHUSU UZOEFU WA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF) KUPIKA TAKWIMU ZA UCHUMI INAPOTOFAUTIANA NA SERIKALI HUSIKA.


• Ilipika Takwimu India Mwaka 2013

• Ilipika Takwimu Argentina Na Venezuela Kwa Miaka 7 Mfululizo (1999-2005)

• Atilia Shaka Takwimu Za Tanzania Kuanza Kupikwa

Fuatilia Uchambuzi.

*Ña David Kafulila*

Tangu Shirika la Fedha Kimataifa ( IMF) kutangaza Ripoti yake mwezi Aprili,2019 kuhusu maoteo (projections) ya kushuka kwa uchumi wa Dunia, kumekuwa na mjadala mrefu Kahusu hali na mwenendo wa Uchumi wetu- Tanzania kufuatia maoteo ya IMF kuwa Uchumi wa Tanzania utaporomoka kufikia asilimia 4%.

Pamoja na mabadiliko yote hayo ya maoteo ya IMF yaliyozua mjadala wa kiuchumi duniani, kwa Tanzania mjadala huu umechagizwa zaidi na uamuzi wa Serikali kutoitambua/ kutokubaliana na ripoti hiyo, ambayo imeonesha maoteo ya ukuaji uchumi kushuka kufikia asilimia 4% kutoka makadirio ya Serikali ya ukuaji wa asilimia 7. 3% sanjari na makadirio ya Bank ya dunia (WB) na IMF yenyewe ambayo awali yalikadiria uchumi wa Tanzania ķukua kwa zaidi ya asilimia 6% mwaka 2019.

Wanasayansi wanatushauri kuwa utafiti unapingwa kwa tafiti. Hivyo sio lengo langu kupinga ripoti hiyo ya IMF isipokuwa kuijadili.

Katika kuchangia mawazo yangu binafsi kuhusu mjadala huu ningependa kuanza kwa swali lililobeba uzito mkubwa kwamba ni sahihi au sio sahihi kwa Serikali kupinga maoteo ya IMF? Je maotoeo ya IMF ni lazima yawe sahihi au yanaweza yasiwe sahihi?

Labda nianze kwa kusema kwamba sio kosa wala sio mara moja nchi kupinga makadirio ya maoteo ya ukuaji wa uchumi, Pili na kwa msisitizo niseme kuwa maoteo ya IMF sio lazima yawe sahihi wakati wote kama nitakavyoeleza kilichotokea nchi kadhaa hususani India, Argentina na Venezuela kama nchi za mifano.

Mwaka wa Fedha 2013/ 14, IMF ilikadiria uchumi wa India kushuka kutoka maoteo ya ukuaji wa asilimia 5. 6% mpaka asilimia 3.7%. Hata hivyo kufika mwisho wa mwaka huo, ukuaji halisi wa uchumi wa India ulikua asilimia 6. 6% Sawa na tofauti ya asilimia 2.9%.

Kwa mujibu wa Gazeti maarufu la nchini India, THE HINDU la Oktoba 13, 2013, Waziri wa Fedha wa India, Bwana P.Chidambaram alinukuliwa kupinga takwimu za IMF kwa kusema haelewi IMF wametoa wapi takwimu kufikia hitimisho la anguko hilo kubwa la ukuaji uchumi kwani ilikuwa ni miezi miwili tangu makadirio ya awali kuonesha kuwa uchumi wa India ungekua kwa asilimia 5.6%.

Tatizo la makadirio ya IMF kukosa uhalisia limepata kujitokeza kwa nchi mbalimbali zaidi ya India. Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Utafiti masuala ya Sera na Uchumi cha Center For Economic and Policy Research Chenye makao yake makuu Washington DC Marekani, Aprili 2007 kilipata kuchapisha makala ya kitafiti kuonesha kasoro kubwa katika maoteo ya ukuaji uchumi ya yanaofanywa na IMF, kasoro ambazo kwa namna zilivyo kubwa na namna zilivyojitokeza zilifanya taasisi hiyo kuweka mashaka makubwa kama Shirika la IMF linafanya kazi zake bila msukumo wa kisiasa.

IMF ilikosea makadirio ya ukuaji uchumi kwa nchi ya Argentina kwa miaka saba 7 mfuĺulizo;

Mwaka 1999, IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 1.5% lakini ukuaji halisi ukawa hasi sifuri nukta nane (-0.8%), sawa na tofauti ya asilimia 2.3%.

Mwaka 2000 IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 3.7% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia hasi nne nukta nne ( -4.4%), sawa na tofauti ya asilimia 8.1% na mwaka 2001, IMF ilikadiria ùkuaji uchumi wa asilimia 2.6% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia hasi kumi nukta tisa (-10.9%) sawa na tofauti ya asilimia 13.5%.

Hata mwaka 2002, IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia1% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 8.8% sawa na tofauti ya asilimia hasi saba nukta nane (-7.8%).

Mwaka 2003 IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa asilimia 4% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 9% sawa na tofauti ya asilimia hasi tano (-5%).

Mwaka 2004 IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 4% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 9.2% sawa na tofauti ya asilimia hasi tano nukta mbili ( -5.2%) na hata mwaka 2005 IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa taifa hilo kuwa asilimia 4.2% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 8.5% sawa na tofauti ya asilimia hasi nne nukta tatu ( -4.3%).

Makosa ya IMF katika kukadiria ukuaji uchumi sio kwa Argentina tu bali hata Venezuela, ambapo miaka mitano mfuĺulizo IMF ilikosea pakubwa katika makadirio ya ukuaji uchumi wa Taifa hilo;

Mwaka1999, IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa nchi ya Venezuela wa asilimia 1.6% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 3.6%.

Mwaka 2000 IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa asilimia 3% lakn ukuaji halisi ukawa 3.4%.

Mwaka 2001, IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa asilimia 2.8% lakini ukuaji halisi ukawa hasi nane nukta tisa ( -8.9%).

Mwaka 2002 IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 2.2% lakini ukuaji halisi ukawa hasi saba nukta nane ( -7.8%).

Mwaka 2003, IMF ilikadiria ukuaji wa asilimia 7.7% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 18.3% .

Mwaka 2004, IMF ilikadiria ukuaji wa asilimia 3.5% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 10.3% na Mwaka 2005, IMF ilikadiria ukuaji uchumi kwa Taifa hilo kuwa asilimia 4.5% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia10. 3%.

Tatizo la kukosewa maotoeo ya ukuaji uchumi imekua mjadala kwa wachumi wengi duniani kufuatia shirika hilo kubwa duniani kubadili mara kwa mara takwimu zake katika muda mfupi kama inavyoonekana kwenye Jukwaa la kiuchumi duniani (World Economic Forum 2019) ambapo kuna makala yenye kichwa " IMF has cut its global forecast for the fourth time in nine months" (July 2018, October 2018, January 2019 and April 2019)..

Ikimaanisha kuwa ndani ya miezi 9, IMF imerekebisha takwimu zake mara nne.

Ni kwa msingi huo mwanauchumi wa moja ya Benki kubwa duniani, Australia and New Zealand Banking (ANZ) (ya 32 kwa ukubwa duniani kufikia mwaka 2018), Bwana Manoji Basantial aliandika uchambuzi Oktoba 13, 2015 wenye kichwa "The IMF missed it again- It is indeed frustrating."

ikielezea tatizo hilo na kwenda mbele zaidi kusema kwamba hali ya IMF kurekebisha takwimu za maoteo mara nyingi katika kipindi kifupi kinaweka mashaka kuhusu umakini wa ripoti zake za makadirio ya ukuaji uchumi.

Maoni ya wachumi hao na zaidi kilichotokea ņchi nilizotaja hapo juu hususani Argentina na Venezuela vinanipa mashaka makubwa kuweza kuziamini ripoti za IMF hasa kwa mwenendo wa utawala wa awamu ya tano wa Taifa la Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli ambaye kwa kiasi kikubwa mwelekeo wake wa kudhibiti rasilimali za nchi hii zilizoporwa kwa muda mrefu haujazipendeza sana nchi zilizokuwa zikinufaika na uporaji huo kupitia kampuni za kimataifa.

Huo ndio ukweli mchungu ambao watanzania tunapswa kuujua kwani mbinu kama hizi zilitumiwa na IMF kwenye ñchi nilizotaja hapo juu.

Katika chapisho hilo la uchambuzi kutoka kituo cha utafiti nilichotaja hapo juu kuhusu makadirio ya uchumi wa Argentina na Venezuela, chapisho lilihusu makadirio ya ukuaji uchumi kwa nchi hizo lililobeba kichwa cha " Political Forecast?".
Uchambuzi huo ulibeba kichwa hicho cha" Political Forecast?" ikimaanisha kwamba kwa namna IMF ilivyokosea katika makadirio yake kuhusu ukuaji uchumi ukihusianisha na mwenendo wa mahusiano kati ya IMF na nchi hizo kuna wakati ilitosha ķuthibitisha kuwa makadirio husika yalisukumwa zaidi ya siasa za IMF na mataifa hayo.

Labda kukazia hili ninukuu sehemu ya uchambuzi huo kuhusu Argentina inayosomeka - “The IMF large and repeated errors in projecting GDP growth in Argentina since 1999 strongly suggest that these errors were politically driven. The large over estimations occurred during the country's 1998 -2002 depression, when IMF was lending billions of dollars to support policies that ultimately ended in economic collapse. Similarly, the underestimates took place at a time IMF had an increasingly antagonistic relationship with Argentina government and opposed number of its economic policies. It is worth noting that despite the IMF pessimism about Argentina's recovery from the beginning, Argentina has now completed a five year economic expansion with fastest growth in the western hemisphere"

Kwa kifupi ripoti hiyo inasisitiza namna ambavyo kuna nyakati IMF inatoa makadirio ya kiuchumi kwa msukumo wa kisiasa/ maslahi yake kwa kueleza kwamba kipindi cha miaka kati ya 1999- 2002 ambacho Argentina ilifuata maelekezo ya IMF na kupewa mabilioni ya dola kutekeleza Sera za IMF, ndio kipindi ambacho IMF ilikuwa ikiweka makadirio ya juu ya ùkuaji uchumi kinyume kabisa na hali halisi kwani ndio kipindi ambacho uchumi wa Argentina ulianguka vibaya sana.

Lakin kipindi ambacho Argentina ilianza kuingia mvutano na IMF, ndio kipindi ambacho IMF iliweka makadirio ya chini ya ukuaji uchumi kulinganisha na hali halisi kama takwimu hapo juu kwa miaka ya 2003-2005 zilivyojionesha.


Ni katika msingi huo ninaendelea kuamini kwamba takwimu za maoteo ya IMF za mwezi Aprili 2019 kuhusu ukuaji uchumi Tanzania kuporomoka mpaka asilimia 4% naziona zikiwa takwimu za mashaka kwa kuzingatia; kwanza mifano ya nchi nilizotaja hapo awali, Pili kwa kuzingatia ukweli kuwa takwimu hizo bado zimetofautiana na takwimu za Benki ya Dunia( WB) ambazo makadirio yake ni kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa zaidi ya asilimia 6% na takwimu za Benki ya Afrika( AfDB) zikionesha kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa asilimia 6.6% lakini tatu msimamo mpya wa kisera kuhusu ulinzi wa rasilimali za Tanzania kwa manufaa ya watanzania, mwelekeo ambao umekosolewa sana na IMF na washirika wake wakitaja kuwa ni kutokutabirika kisera!
 
GUSSIE

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Messages
2,852
Points
2,000
GUSSIE

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2014
2,852 2,000
Kwanza kabisa ilibidi aeleze indicators za economic growth?

Uchumi unapimwa kwa vigezo vipi?

Per capital income?
GDP?
Total investment?

Na ni nini exceptions au mapungufu ya nadharia tajwa hapo juu?

IMF wanapima Uchumi kwa vigezo vipi?

Kama kwa kigezo cha per capital income, Mimi binafsi Uchumi wangu wa mfukoni lakini umeongezeka Mara 2 mwaka huu

Kama ni Total investment mimi binafsi mwaka huu ni zero lakini kwenye education investment nimefanikiwa 100%
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,824
Points
2,000
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,824 2,000
Maisha ya Mtanzania mwaka 2015 na mwaka 2018/19 yanatofauti kubwa sana hata motto wako wa miaka 15 anaweza kuziona tofauti hizo. Standard ya maisha imeshuka sana. Sasa iweje uchumi upande na hali ya maisha iwe tete kila mahali?
Kafulila usiwe kama masikini ombaomba aliyekutwa anaokota makombo ili ale akachukuliwa kwenda kufagia jikoni kwa tajiri basi kwa vile jikoni anakula vya kwenye sufuria anawaambia omba omba wenzie kuwa makombo ya jalalani yana magonjwa wasile.
 
Y

ycam

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
875
Points
1,000
Y

ycam

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
875 1,000
Kafulila, jibu hoja moja baada ya nyingine zilizoainishwa na IMF kwenye ripoti yao kuhusu Tanzania; siyo kutaja mifano ya nchi nyingine ambazo mazingira yao ya kiuchumi, kisiasa na kadhalika ni tofauti kabisa na Tanzania, na ripoti zao za kiuchumi hujaziweka hapa tulinganishe. Kama vipi weka ripoti za IMF za uchumi wa hizo nchi ulizotaja hapa kama alivyofanya Zitto tulinganishe na ripoti ya IMF ya mwaka huu kuhusu Tz. Watanzania wa sasahivi siyo Watanzania wa enzi zile.
 
GUSSIE

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Messages
2,852
Points
2,000
GUSSIE

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2014
2,852 2,000
Kafulila hata uje na fact zipi kama hutaweza kukiri kuwa maisha ya sasa yamekuwa magumu, nitaendelea kuamini ripoti ya IMF.
Watueleze Uchumi wanaupima kwa vigezo gani Tanzania?

Measures of economic growth are

Tafadhali tajeni vigezo tujadili sio kelele tu

Macro level _Je serikali imeongeza spending au imepunguza

Tax base iko vipi Tanzania, Uwekezaji unavutia au hauvutii
 
REJESHO HURU

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2014
Messages
2,756
Points
2,000
REJESHO HURU

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Joined Mar 6, 2014
2,756 2,000
Dogo akili zimehamia tumboni hivi hali ya uchumi wa sasa kuna haja IMF watoe takwimu hali ipoje yani hata ukimfuata omba omba asiyejua kusoma na kuandika atakwambia mambo magumu sasa kafurila asitugeuze watu wajinga yeye akae kimya ajilie anavyopewa asituchanganye kabisa wanainchi
 
Oii

Oii

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2017
Messages
3,440
Points
2,000
Oii

Oii

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2017
3,440 2,000
Kafulila hata uje na fact zipi kama hutaweza kukiri kuwa maisha ya sasa yamekuwa magumu, nitaendelea kuamini ripoti ya IMF.
Magumu kiaje, ww unafany kazi? Unalipwa? Sababu ya kutolipwa ni serikali? Nifafanulie tafadhali.
 
xng hua

xng hua

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2016
Messages
1,713
Points
2,000
xng hua

xng hua

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2016
1,713 2,000
makadirio is just a number sidhani wakisha kadiria ushindwe kupambania uchumi wako
kama ni 4 pambaneni ili upande ili muwa prove wrong hao imf

sioni umuhimu kubishana nao wakat hatma ya uchumi wenu mnao nyie
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
11,229
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
11,229 2,000
Kwanza kabisa ilibidi aeleze indicators za economic growth?

Uchumi unapimwa kwa vigezo vipi?

Per capital income?
GDP?
Total investment?

Na ni nini exceptions au mapungufu ya nadharia tajwa hapo juu?

IMF wanapima Uchumi kwa vigezo vipi?

Kama kwa kigezo cha per capital income, Mimi binafsi Uchumi wangu wa mfukoni lakini umeongezeka Mara 2 mwaka huu

Kama ni Total investment mimi binafsi mwaka huu ni zero lakini kwenye education investment nimefanikiwa 100%
Ripoti imewekwa humu JF nenda ukurasa kuanzia 21 wameweka indicators na figures zake.
Nilitegemea kafulila atapinga kutumia hizo data kumbe amekuja na maneno matupu kuhusu inaccuracy kwenye nchi chache bila kusifia kwamba kwa miaka mingi sasa estimations kwenye nchi wanachama zaidi ya 90% hazikosewi anaenda kujengea hoja kwenye kanchi kamoja tu.

Ndio maana yakaitwa makadirio yaani unatumia taarifa zilizopo kubashiri kesho itakuwaje ili uweke sera za kujiandaa mapema sasa wao badala ya kuangalia ushauri uliowekwa kwenye sekta zote wao wanalalamika takwimu hivyo wanasahau lengo kuu la ripoti hizo.

Hata serikali ya Tanzania kila mwaka hupelekea makadirio ya mapato na matumizi ila tokea uhuru ni lini bajeti yetu imewahi kutekelezeka hata kwa 70% hasa bajeti ya Maendeleo?? Ila sijawahi sikia wakikataliwa misaada eti kisa makadirio yao hayaendani na uhalisia!!!

Na ndio maana IMF imerecommend Tanzania itengeneze realistic budgets ili zitekelezeke,isiingilie sana bei za soko,itengeneze spill over effect kwa kuiongezea nguvu private sector,Pesa kukaa BOT huku haizalishi ni hasara kuliko ingewekwa kwenye benki binafsi ziongeze ukwasi n.k hayo kafulila haongelei ila amejikita kwenye MAKADIRIO ambayo tafiti zote duniani huwa zinaweka ''margin of error'' ikimaanisha hata siku moje makadirio hayawezi kuwa 100% sawa hivyo unaweka chumba kwa ajili ya makosa yatakayojitokeza.

Kiufupi kafulila anajibu ili kujikomba na kulinda cheo chake zaidi ya hapo sijaona hoja yoyote ya msingi.
 

Forum statistics

Threads 1,406,194
Members 532,237
Posts 34,508,158
Top