David Kafulila: Uzoefu wa IMF kupika takwimu za uchumi inapotofautiana na Serikali husika

Mkuu mie nadhani ungeandika kuhusu Ripoti ya CAG ningekupongeza sana kwani Mafisadi ndani ya Serikali Uliyomo wanapiga sana kodi za walalahoi

Na alisema alikuwa upinzani sababu ya ajenda kuu ya ufisadi hivo kaunga juhudi sababu ufisadi unashughulikiwa hadi kuna mahakama ya mafisadi sasa kulikoni yeye kuwa kimya kuhusu ripoti ya CAG ya Miaka miwili.
 
Sijasoma nitasoma baadae, ngoja nimeze kwanza mate ya akili.. Mie jambo likishaongelewa na mwanasiasa uwezekano wa kuamini huwa mdogo mnooo
 
Maisha ya Mtanzania mwaka 2015 na mwaka 2018/19 yanatofauti kubwa sana hata motto wako wa miaka 15 anaweza kuziona tofauti hizo. Standard ya maisha imeshuka sana. Sasa iweje uchumi upande na hali ya maisha iwe tete kila mahali?
Kafulila usiwe kama masikini ombaomba aliyekutwa anaokota makombo ili ale akachukuliwa kwenda kufagia jikoni kwa tajiri basi kwa vile jikoni anakula vya kwenye sufuria anawaambia omba omba wenzie kuwa makombo ya jalalani yana magonjwa wasile.

Yana utofauti gani mazee, mmeachishwa kazi? Vyeti feki labda. Lakini kama mtu una kazi yako halali, unalipwa, maisha yamekuwaje worse.

Licha ya kwamba hata bei ya vitu 2015 ni juu kushinda bei ya vitu hivyohivyo 2013.

Nyie mnaosema maisha magumu, hamna kazi inayowapa hela au.

Mngekuwa mnaelezea maisha yanakuwaje magumu, wengine it doesnt make sense tunaona bars/ clubs kunajaa. Uwanja wa taifa unajaa. Construction activities zimejaa awamu hii kushinda zote, watu jobless 2015 wanalipwa huko saa hii. FDI tunaongoza EA, watu wanalipwa hapo.

Sasa honestly mngekuwa na figures za ku support huo ugumu wa maisha mngesaidia watu wengi sana, with all due respect boss.
 
Lakini hali halisi tunaiona maana maduka mengi yamefungwa, watu hawana pesa , wafanyakazi hawapandishwi mishahara, etc....

Huu utafiti wa IMF ungekuja tofauti ndio ingeshangaza..
 
Huu ndio uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu ??

Yaàni badala ya kujibu hoja , yeye anaandika historia ??

This is rubbish ..!!
 
UZOEFU WA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF) KUPIKA TAKWIMU ZA UCHUMI INAPOTOFAUTIANA NA SERIKALI HUSIKA

• Ilipika Takwimu India Mwaka 2013

• Ilipika Takwimu Argentina Na Venezuela Kwa Miaka 7 Mfululizo (1999-2005)

Takwimu Za Tanzania Kuanza Kupikwa

Tangu Shirika la Fedha Kimataifa ( IMF) kutangaza Ripoti yake mwezi Aprili,2019 kuhusu maoteo (projections) ya kushuka kwa uchumi wa Dunia, kumekuwa na mjadala mrefu Kahusu hali na mwenendo wa Uchumi wetu- Tanzania kufuatia maoteo ya IMF kuwa Uchumi wa Tanzania utaporomoka kufikia asilimia 4%.

Pamoja na mabadiliko yote hayo ya maoteo ya IMF yaliyozua mjadala wa kiuchumi duniani, kwa Tanzania mjadala huu umechagizwa zaidi na uamuzi wa Serikali kutoitambua/ kutokubaliana na ripoti hiyo, ambayo imeonesha maoteo ya ukuaji uchumi kushuka kufikia asilimia 4% kutoka makadirio ya Serikali ya ukuaji wa asilimia 7.3% sanjari na makadirio ya Bank ya dunia (WB) na IMF yenyewe ambayo awali yalikadiria uchumi wa Tanzania ķukua kwa zaidi ya asilimia 6% mwaka 2019.

Wanasayansi wanatushauri kuwa utafiti unapingwa kwa tafiti. Hivyo sio lengo langu kupinga ripoti hiyo ya IMF isipokuwa kuijadili.

Katika kuchangia mawazo yangu binafsi kuhusu mjadala huu ningependa kuanza kwa swali lililobeba uzito mkubwa kwamba ni sahihi au sio sahihi kwa Serikali kupinga maoteo ya IMF? Je maotoeo ya IMF ni lazima yawe sahihi au yanaweza yasiwe sahihi?

Labda nianze kwa kusema kwamba sio kosa wala sio mara moja nchi kupinga makadirio ya maoteo ya ukuaji wa uchumi, Pili na kwa msisitizo niseme kuwa maoteo ya IMF sio lazima yawe sahihi wakati wote kama nitakavyoeleza kilichotokea nchi kadhaa hususani India, Argentina na Venezuela kama nchi za mifano.

Mwaka wa Fedha 2013/ 14, IMF ilikadiria uchumi wa India kushuka kutoka maoteo ya ukuaji wa asilimia 5. 6% mpaka asilimia 3.7%. Hata hivyo kufika mwisho wa mwaka huo, ukuaji halisi wa uchumi wa India ulikua asilimia 6.6% Sawa na tofauti ya asilimia 2.9%.

Kwa mujibu wa Gazeti maarufu la nchini India, THE HINDU la Oktoba 13, 2013, Waziri wa Fedha wa India, Bwana P.Chidambaram alinukuliwa kupinga takwimu za IMF kwa kusema haelewi IMF wametoa wapi takwimu kufikia hitimisho la anguko hilo kubwa la ukuaji uchumi kwani ilikuwa ni miezi miwili tangu makadirio ya awali kuonesha kuwa uchumi wa India ungekua kwa asilimia 5.6%.

Tatizo la makadirio ya IMF kukosa uhalisia limepata kujitokeza kwa nchi mbalimbali zaidi ya India. Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Utafiti masuala ya Sera na Uchumi cha Center For Economic and Policy Research Chenye makao yake makuu Washington DC Marekani, Aprili 2007 kilipata kuchapisha makala ya kitafiti kuonesha kasoro kubwa katika maoteo ya ukuaji uchumi ya yanaofanywa na IMF, kasoro ambazo kwa namna zilivyo kubwa na namna zilivyojitokeza zilifanya taasisi hiyo kuweka mashaka makubwa kama Shirika la IMF linafanya kazi zake bila msukumo wa kisiasa.

IMF ilikosea makadirio ya ukuaji uchumi kwa nchi ya Argentina kwa miaka saba 7 mfuĺulizo;

Mwaka 1999, IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 1.5% lakini ukuaji halisi ukawa hasi sifuri nukta nane (-0.8%), sawa na tofauti ya asilimia 2.3%.

Mwaka 2000 IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 3.7% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia hasi nne nukta nne ( -4.4%), sawa na tofauti ya asilimia 8.1% na mwaka 2001, IMF ilikadiria ùkuaji uchumi wa asilimia 2.6% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia hasi kumi nukta tisa (-10.9%) sawa na tofauti ya asilimia 13.5%.

Hata mwaka 2002, IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia1% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 8.8% sawa na tofauti ya asilimia hasi saba nukta nane (-7.8%).

Mwaka 2003 IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa asilimia 4% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 9% sawa na tofauti ya asilimia hasi tano (-5%).

Mwaka 2004 IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 4% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 9.2% sawa na tofauti ya asilimia hasi tano nukta mbili ( -5.2%) na hata mwaka 2005 IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa taifa hilo kuwa asilimia 4.2% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 8.5% sawa na tofauti ya asilimia hasi nne nukta tatu ( -4.3%).

Makosa ya IMF katika kukadiria ukuaji uchumi sio kwa Argentina tu bali hata Venezuela, ambapo miaka mitano mfuĺulizo IMF ilikosea pakubwa katika makadirio ya ukuaji uchumi wa Taifa hilo;

Mwaka1999, IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa nchi ya Venezuela wa asilimia 1.6% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 3.6%.

Mwaka 2000 IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa asilimia 3% lakn ukuaji halisi ukawa 3.4%.

Mwaka 2001, IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa asilimia 2.8% lakini ukuaji halisi ukawa hasi nane nukta tisa ( -8.9%).

Mwaka 2002 IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 2.2% lakini ukuaji halisi ukawa hasi saba nukta nane ( -7.8%).

Mwaka 2003, IMF ilikadiria ukuaji wa asilimia 7.7% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 18.3% .

Mwaka 2004, IMF ilikadiria ukuaji wa asilimia 3.5% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 10.3% na Mwaka 2005, IMF ilikadiria ukuaji uchumi kwa Taifa hilo kuwa asilimia 4.5% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 10.3%.

Tatizo la kukosewa maotoeo ya ukuaji uchumi imekua mjadala kwa wachumi wengi duniani kufuatia shirika hilo kubwa duniani kubadili mara kwa mara takwimu zake katika muda mfupi kama inavyoonekana kwenye Jukwaa la kiuchumi duniani (World Economic Forum 2019) ambapo kuna makala yenye kichwa " IMF has cut its global forecast for the fourth time in nine months" (July 2018, October 2018, January 2019 and April 2019)..

Ikimaanisha kuwa ndani ya miezi 9, IMF imerekebisha takwimu zake mara nne.

Ni kwa msingi huo mwanauchumi wa moja ya Benki kubwa duniani, Australia and New Zealand Banking (ANZ) (ya 32 kwa ukubwa duniani kufikia mwaka 2018), Bwana Manoji Basantial aliandika uchambuzi Oktoba 13, 2015 wenye kichwa "The IMF missed it again- It is indeed frustrating."

ikielezea tatizo hilo na kwenda mbele zaidi kusema kwamba hali ya IMF kurekebisha takwimu za maoteo mara nyingi katika kipindi kifupi kinaweka mashaka kuhusu umakini wa ripoti zake za makadirio ya ukuaji uchumi.

Maoni ya wachumi hao na zaidi kilichotokea ņchi nilizotaja hapo juu hususani Argentina na Venezuela vinanipa mashaka makubwa kuweza kuziamini ripoti za IMF hasa kwa mwenendo wa utawala wa awamu ya tano wa Taifa la Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli ambaye kwa kiasi kikubwa mwelekeo wake wa kudhibiti rasilimali za nchi hii zilizoporwa kwa muda mrefu haujazipendeza sana nchi zilizokuwa zikinufaika na uporaji huo kupitia kampuni za kimataifa.

Huo ndio ukweli mchungu ambao watanzania tunapswa kuujua kwani mbinu kama hizi zilitumiwa na IMF kwenye ñchi nilizotaja hapo juu.

Katika chapisho hilo la uchambuzi kutoka kituo cha utafiti nilichotaja hapo juu kuhusu makadirio ya uchumi wa Argentina na Venezuela, chapisho lilihusu makadirio ya ukuaji uchumi kwa nchi hizo lililobeba kichwa cha " Political Forecast?".
Uchambuzi huo ulibeba kichwa hicho cha" Political Forecast?" ikimaanisha kwamba kwa namna IMF ilivyokosea katika makadirio yake kuhusu ukuaji uchumi ukihusianisha na mwenendo wa mahusiano kati ya IMF na nchi hizo kuna wakati ilitosha ķuthibitisha kuwa makadirio husika yalisukumwa zaidi na siasa za IMF na mataifa hayo.

Labda kukazia hili ninukuu sehemu ya uchambuzi huo kuhusu Argentina inayosomeka - “The IMF large and repeated errors in projecting GDP growth in Argentina since 1999 strongly suggest that these errors were politically driven. The large over estimations occurred during the country's 1998 -2002 depression, when IMF was lending billions of dollars to support policies that ultimately ended in economic collapse. Similarly, the underestimates took place at a time IMF had an increasingly antagonistic relationship with Argentina government and opposed number of its economic policies. It is worth noting that despite the IMF pessimism about Argentina's recovery from the beginning, Argentina has now completed a five year economic expansion with fastest growth in the western hemisphere"

Kwa kifupi ripoti hiyo inasisitiza namna ambavyo kuna nyakati IMF inatoa makadirio ya kiuchumi kwa msukumo wa kisiasa/ maslahi yake kwa kueleza kwamba kipindi cha miaka kati ya 1999- 2002 ambacho Argentina ilifuata maelekezo ya IMF na kupewa mabilioni ya dola kutekeleza Sera za IMF, ndio kipindi ambacho IMF ilikuwa ikiweka makadirio ya juu ya ùkuaji uchumi kinyume kabisa na hali halisi kwani ndio kipindi ambacho uchumi wa Argentina ulianguka vibaya sana.

Lakin kipindi ambacho Argentina ilianza kuingia mvutano na IMF, ndio kipindi ambacho IMF iliweka makadirio ya chini ya ukuaji uchumi kulinganisha na hali halisi kama takwimu hapo juu kwa miaka ya 2003-2005 zilivyojionesha.

Ni katika msingi huo ninaendelea kuamini kwamba takwimu za maoteo ya IMF za mwezi Aprili 2019 kuhusu ukuaji uchumi Tanzania kuporomoka mpaka asilimia 4% naziona zikiwa takwimu za mashaka kwa kuzingatia; kwanza mifano ya nchi nilizotaja hapo awali, Pili kwa kuzingatia ukweli kuwa takwimu hizo bado zimetofautiana na takwimu za Benki ya Dunia( WB) ambazo makadirio yake ni kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa zaidi ya asilimia 6% na takwimu za Benki ya Afrika( AfDB) zikionesha kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa asilimia 6.6% lakini tatu msimamo mpya wa kisera kuhusu ulinzi wa rasilimali za Tanzania kwa manufaa ya watanzania, mwelekeo ambao umekosolewa sana na IMF na washirika wake wakitaja kuwa ni kutokutabirika kisera!

Imeandikwa na David Kafulila
 
Watueleze Uchumi wanaupima kwa vigezo gani Tanzania?

Measures of economic growth are

Tafadhali tajeni vigezo tujadili sio kelele tu

Macro level _Je serikali imeongeza spending au imepunguza

Tax base iko vipi Tanzania, Uwekezaji unavutia au hauvutii

Ila kuna watu sijui wanawezaje kuishi kwa amani na unafiki wa aina hii. Ila Tumbili hata ukimwangalia usoni ni mtu mwenye njaa sana. Njaa mbaya jamani acheni tu.
 
MAONI YA DAVID KAFULILA KUHUSU UZOEFU WA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF) KUPIKA TAKWIMU ZA UCHUMI INAPOTOFAUTIANA NA SERIKALI HUSIKA.

• Ilipika Takwimu India Mwaka 2013

• Ilipika Takwimu Argentina Na Venezuela Kwa Miaka 7 Mfululizo (1999-2005)

• Atilia Shaka Takwimu Za Tanzania Kuanza Kupikwa

Fuatilia Uchambuzi.

*Ña David Kafulila*

Tangu Shirika la Fedha Kimataifa ( IMF) kutangaza Ripoti yake mwezi Aprili,2019 kuhusu maoteo (projections) ya kushuka kwa uchumi wa Dunia, kumekuwa na mjadala mrefu Kahusu hali na mwenendo wa Uchumi wetu- Tanzania kufuatia maoteo ya IMF kuwa Uchumi wa Tanzania utaporomoka kufikia asilimia 4%.

Pamoja na mabadiliko yote hayo ya maoteo ya IMF yaliyozua mjadala wa kiuchumi duniani, kwa Tanzania mjadala huu umechagizwa zaidi na uamuzi wa Serikali kutoitambua/ kutokubaliana na ripoti hiyo, ambayo imeonesha maoteo ya ukuaji uchumi kushuka kufikia asilimia 4% kutoka makadirio ya Serikali ya ukuaji wa asilimia 7. 3% sanjari na makadirio ya Bank ya dunia (WB) na IMF yenyewe ambayo awali yalikadiria uchumi wa Tanzania ķukua kwa zaidi ya asilimia 6% mwaka 2019.

Wanasayansi wanatushauri kuwa utafiti unapingwa kwa tafiti. Hivyo sio lengo langu kupinga ripoti hiyo ya IMF isipokuwa kuijadili.

Katika kuchangia mawazo yangu binafsi kuhusu mjadala huu ningependa kuanza kwa swali lililobeba uzito mkubwa kwamba ni sahihi au sio sahihi kwa Serikali kupinga maoteo ya IMF? Je maotoeo ya IMF ni lazima yawe sahihi au yanaweza yasiwe sahihi?

Labda nianze kwa kusema kwamba sio kosa wala sio mara moja nchi kupinga makadirio ya maoteo ya ukuaji wa uchumi, Pili na kwa msisitizo niseme kuwa maoteo ya IMF sio lazima yawe sahihi wakati wote kama nitakavyoeleza kilichotokea nchi kadhaa hususani India, Argentina na Venezuela kama nchi za mifano.

Mwaka wa Fedha 2013/ 14, IMF ilikadiria uchumi wa India kushuka kutoka maoteo ya ukuaji wa asilimia 5. 6% mpaka asilimia 3.7%. Hata hivyo kufika mwisho wa mwaka huo, ukuaji halisi wa uchumi wa India ulikua asilimia 6. 6% Sawa na tofauti ya asilimia 2.9%.

Kwa mujibu wa Gazeti maarufu la nchini India, THE HINDU la Oktoba 13, 2013, Waziri wa Fedha wa India, Bwana P.Chidambaram alinukuliwa kupinga takwimu za IMF kwa kusema haelewi IMF wametoa wapi takwimu kufikia hitimisho la anguko hilo kubwa la ukuaji uchumi kwani ilikuwa ni miezi miwili tangu makadirio ya awali kuonesha kuwa uchumi wa India ungekua kwa asilimia 5.6%.

Tatizo la makadirio ya IMF kukosa uhalisia limepata kujitokeza kwa nchi mbalimbali zaidi ya India. Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Utafiti masuala ya Sera na Uchumi cha Center For Economic and Policy Research Chenye makao yake makuu Washington DC Marekani, Aprili 2007 kilipata kuchapisha makala ya kitafiti kuonesha kasoro kubwa katika maoteo ya ukuaji uchumi ya yanaofanywa na IMF, kasoro ambazo kwa namna zilivyo kubwa na namna zilivyojitokeza zilifanya taasisi hiyo kuweka mashaka makubwa kama Shirika la IMF linafanya kazi zake bila msukumo wa kisiasa.

IMF ilikosea makadirio ya ukuaji uchumi kwa nchi ya Argentina kwa miaka saba 7 mfuĺulizo;

Mwaka 1999, IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 1.5% lakini ukuaji halisi ukawa hasi sifuri nukta nane (-0.8%), sawa na tofauti ya asilimia 2.3%.

Mwaka 2000 IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 3.7% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia hasi nne nukta nne ( -4.4%), sawa na tofauti ya asilimia 8.1% na mwaka 2001, IMF ilikadiria ùkuaji uchumi wa asilimia 2.6% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia hasi kumi nukta tisa (-10.9%) sawa na tofauti ya asilimia 13.5%.

Hata mwaka 2002, IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia1% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 8.8% sawa na tofauti ya asilimia hasi saba nukta nane (-7.8%).

Mwaka 2003 IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa asilimia 4% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 9% sawa na tofauti ya asilimia hasi tano (-5%).

Mwaka 2004 IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 4% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 9.2% sawa na tofauti ya asilimia hasi tano nukta mbili ( -5.2%) na hata mwaka 2005 IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa taifa hilo kuwa asilimia 4.2% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 8.5% sawa na tofauti ya asilimia hasi nne nukta tatu ( -4.3%).

Makosa ya IMF katika kukadiria ukuaji uchumi sio kwa Argentina tu bali hata Venezuela, ambapo miaka mitano mfuĺulizo IMF ilikosea pakubwa katika makadirio ya ukuaji uchumi wa Taifa hilo;

Mwaka1999, IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa nchi ya Venezuela wa asilimia 1.6% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 3.6%.

Mwaka 2000 IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa asilimia 3% lakn ukuaji halisi ukawa 3.4%.

Mwaka 2001, IMF ilikadiria ukuaji uchumi wa asilimia 2.8% lakini ukuaji halisi ukawa hasi nane nukta tisa ( -8.9%).

Mwaka 2002 IMF ilikadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 2.2% lakini ukuaji halisi ukawa hasi saba nukta nane ( -7.8%).

Mwaka 2003, IMF ilikadiria ukuaji wa asilimia 7.7% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 18.3% .

Mwaka 2004, IMF ilikadiria ukuaji wa asilimia 3.5% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia 10.3% na Mwaka 2005, IMF ilikadiria ukuaji uchumi kwa Taifa hilo kuwa asilimia 4.5% lakini ukuaji halisi ukawa asilimia10. 3%.

Tatizo la kukosewa maotoeo ya ukuaji uchumi imekua mjadala kwa wachumi wengi duniani kufuatia shirika hilo kubwa duniani kubadili mara kwa mara takwimu zake katika muda mfupi kama inavyoonekana kwenye Jukwaa la kiuchumi duniani (World Economic Forum 2019) ambapo kuna makala yenye kichwa " IMF has cut its global forecast for the fourth time in nine months" (July 2018, October 2018, January 2019 and April 2019)..

Ikimaanisha kuwa ndani ya miezi 9, IMF imerekebisha takwimu zake mara nne.

Ni kwa msingi huo mwanauchumi wa moja ya Benki kubwa duniani, Australia and New Zealand Banking (ANZ) (ya 32 kwa ukubwa duniani kufikia mwaka 2018), Bwana Manoji Basantial aliandika uchambuzi Oktoba 13, 2015 wenye kichwa "The IMF missed it again- It is indeed frustrating."

ikielezea tatizo hilo na kwenda mbele zaidi kusema kwamba hali ya IMF kurekebisha takwimu za maoteo mara nyingi katika kipindi kifupi kinaweka mashaka kuhusu umakini wa ripoti zake za makadirio ya ukuaji uchumi.

Maoni ya wachumi hao na zaidi kilichotokea ņchi nilizotaja hapo juu hususani Argentina na Venezuela vinanipa mashaka makubwa kuweza kuziamini ripoti za IMF hasa kwa mwenendo wa utawala wa awamu ya tano wa Taifa la Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli ambaye kwa kiasi kikubwa mwelekeo wake wa kudhibiti rasilimali za nchi hii zilizoporwa kwa muda mrefu haujazipendeza sana nchi zilizokuwa zikinufaika na uporaji huo kupitia kampuni za kimataifa.

Huo ndio ukweli mchungu ambao watanzania tunapswa kuujua kwani mbinu kama hizi zilitumiwa na IMF kwenye ñchi nilizotaja hapo juu.

Katika chapisho hilo la uchambuzi kutoka kituo cha utafiti nilichotaja hapo juu kuhusu makadirio ya uchumi wa Argentina na Venezuela, chapisho lilihusu makadirio ya ukuaji uchumi kwa nchi hizo lililobeba kichwa cha " Political Forecast?".
Uchambuzi huo ulibeba kichwa hicho cha" Political Forecast?" ikimaanisha kwamba kwa namna IMF ilivyokosea katika makadirio yake kuhusu ukuaji uchumi ukihusianisha na mwenendo wa mahusiano kati ya IMF na nchi hizo kuna wakati ilitosha ķuthibitisha kuwa makadirio husika yalisukumwa zaidi ya siasa za IMF na mataifa hayo.

Labda kukazia hili ninukuu sehemu ya uchambuzi huo kuhusu Argentina inayosomeka - “The IMF large and repeated errors in projecting GDP growth in Argentina since 1999 strongly suggest that these errors were politically driven. The large over estimations occurred during the country's 1998 -2002 depression, when IMF was lending billions of dollars to support policies that ultimately ended in economic collapse. Similarly, the underestimates took place at a time IMF had an increasingly antagonistic relationship with Argentina government and opposed number of its economic policies. It is worth noting that despite the IMF pessimism about Argentina's recovery from the beginning, Argentina has now completed a five year economic expansion with fastest growth in the western hemisphere"

Kwa kifupi ripoti hiyo inasisitiza namna ambavyo kuna nyakati IMF inatoa makadirio ya kiuchumi kwa msukumo wa kisiasa/ maslahi yake kwa kueleza kwamba kipindi cha miaka kati ya 1999- 2002 ambacho Argentina ilifuata maelekezo ya IMF na kupewa mabilioni ya dola kutekeleza Sera za IMF, ndio kipindi ambacho IMF ilikuwa ikiweka makadirio ya juu ya ùkuaji uchumi kinyume kabisa na hali halisi kwani ndio kipindi ambacho uchumi wa Argentina ulianguka vibaya sana.

Lakin kipindi ambacho Argentina ilianza kuingia mvutano na IMF, ndio kipindi ambacho IMF iliweka makadirio ya chini ya ukuaji uchumi kulinganisha na hali halisi kama takwimu hapo juu kwa miaka ya 2003-2005 zilivyojionesha.

Ni katika msingi huo ninaendelea kuamini kwamba takwimu za maoteo ya IMF za mwezi Aprili 2019 kuhusu ukuaji uchumi Tanzania kuporomoka mpaka asilimia 4% naziona zikiwa takwimu za mashaka kwa kuzingatia; kwanza mifano ya nchi nilizotaja hapo awali, Pili kwa kuzingatia ukweli kuwa takwimu hizo bado zimetofautiana na takwimu za Benki ya Dunia( WB) ambazo makadirio yake ni kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa zaidi ya asilimia 6% na takwimu za Benki ya Afrika( AfDB) zikionesha kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa asilimia 6.6% lakini tatu msimamo mpya wa kisera kuhusu ulinzi wa rasilimali za Tanzania kwa manufaa ya watanzania, mwelekeo ambao umekosolewa sana na IMF na washirika wake wakitaja kuwa ni kutokutabirika kisera!
Mkuu niliwahi leta uzi wenye mashaka na shirika hili.

(IMF)ni instrument inayotumika kisiasa na mabeberu kwa upikaji wa data kufikia malengo waliokusudia(unyonyaji)

Nakubaliana na wewe zengwe ni baada ya serikali kudhibiti raslimali zake ikiwemo (migodi)
Ukiona data zinakubeba ujue kuna sehemu unapigwa,na ukiona data hazikubebi basi ujue umewabania,
Tukubali tusikubali,maoteo ya IMF kuhusu uchumi wa tanzania yanamsukumo wa kisiasa,piga ua.
Naunga mkono hoja yako
 
Haka kafulila kabasaka mkate wake na mkewe anasaka akiwa chadema. Wanaishi vizuri,somesha watoto shule bora,tembelea gari nzuri nk. Kafulia wewe tetea serikali uwezavyo maana wengi tunajua kwakweli njaa ni mbaya hatamimi ningetetea iwapo ningekuwa nafasi uliyopo
 
Hivi huyu Kafulila anajua kuwa sekta binafsi nchini Tanzania imedhoofika mithili ya mgonjwa aliyepo ICU?
Hivi huyu Kafulila anajua kuwa "Unemployment rate" inazidi kukua kwa kasi?

Au huyu ndugu yetu kesharidhika kisha kapata ujiko kwenye serikali ya awamu hii..??
Anyway; wenye shibe na nafasi zao hawawezi kuielewa ile ripoti ya IMF.
 
Kafulila Literally means "kajambia"

Ushuzi unanukaje!!!!!
 
Kama wewe ni muimini wa dini hizi mbili Islam na Christian tambua tu dini zote zinakataza unafiki na mwisho wasiku kwa kila ulitendalo tambua kuna moto na pepo..Duniani tunapita tu na Mungu anaona na kujua kila kitu mpaka nafsini kwako..
 
Mkuu mie nadhani ungeandika kuhusu Ripoti ya CAG ningekupongeza sana kwani Mafisadi ndani ya Serikali Uliyomo wanapiga sana kodi za walalahoi
Siku zote maoteo, kama ilivyo utabiri wa kisayansi, unaangalia vigezo. Kama ilivyo kwa utabiri, maoteo yanaweza yakasibu au yakaja vingine. Ni kawaida pia maoteo, ili yawe ni maoteo, lazima kuwe na uwezekano wa mtu mwingine kupinga kwa hoja (falsification). Kwa muktadha huo Kafulila, kama ilivyo kwa IMF, uko sahihi kwa mantiki ya hapo juu. Wacha tuone matokeo, kwani pande zote hizi mbili ziko sahihi kwa vigezo walivyotumia.
Z
 
Back
Top Bottom