GE2025 David Kafulila: Ni vizuri aliyeiandaa dira ya 2050 apewe nafasi ya kuiwekea misingi walau hadi 2030

GE2025 David Kafulila: Ni vizuri aliyeiandaa dira ya 2050 apewe nafasi ya kuiwekea misingi walau hadi 2030

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
3,579
Reaction score
2,906

KAULI HII YA KAFULILA INAFUNGA MJADALA

Na Mwandishi Wetu,

Dar es Salaam,
Katika mahojiano ya moja kwa moja kupitia kipindi maarufu cha DK45 kinachorushwa na runinga ya ITV kila Jumatatu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia (PPP Centre), Bw. David Kafulila, ametoa taswira pana kuhusu ndoto ya Tanzania kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.
Bw. Kafulila alisisitiza kuwa ili taifa lifikie dira hiyo, kasi ya ukuaji wa uchumi inapaswa kuongezeka maradufu. Kwa sasa, uchumi wa Tanzania unakua kwa wastani wa takribani asilimia 5 hadi 6 kwa mwaka. Hata hivyo, dira ya 2050 inalenga ukuaji wa asilimia 11 kila mwaka – hatua ambayo, kwa mtazamo wake, siyo jambo lisilowezekana.

Mfano Kutoka Korea Kusini

Akitumia rejea ya kihistoria, Kafulila aliibua mfano wa Korea Kusini kama kielelezo cha mafanikio. “Korea Kusini walianza safari wakiwa na uchumi mdogo, sawa na wa Tanzania wa sasa wenye ukubwa wa takribani dola bilioni 85. Lakini katika kipindi cha miaka 25 pekee, walijipandisha hadhi na kuingia kwenye ligi ya mataifa yenye uchumi wa zaidi ya dola trilioni moja,” alisema.

Kwa mujibu wake, mafanikio hayo hayakutokana na miujiza, bali mabadiliko ya kifikra, mwelekeo mpya wa taasisi na nidhamu ya kitaifa katika utekelezaji wa sera.

Pato la Kila Mwananchi (Percapita income)

Mbali na ukuaji wa uchumi jumla, Kafulila aligusia kipimo muhimu kinachoonyesha hali halisi ya maisha ya wananchi – pato la mtu mmoja mmoja (per capita income). Hivi sasa, wastani wa pato la kila Mtanzania ni mdogo ikilinganishwa na nchi zilizoendelea. Lakini Kafulila alisema matarajio ya taifa ni makubwa.

“Ifikapo mwaka 2050, tunatarajia pato la mtu mmoja mmoja kufikia dola za Marekani 7,000. Hii ni wastani, na inamaanisha kuwa wengi wetu tutakuwa tunazalisha ama kiwango hicho au zaidi ya hapo,” alifafanua.

Hata hivyo, alitoa angalizo kwamba wastani huo haumaanishi kila mwananchi kufikia kiwango hicho sawasawa, bali huenda baadhi wakabaki chini ya mstari huo huku wengi wakinufaika zaidi.

Mabadiliko ya Taasisi na Nidhamu katika kazi.

Akihitimisha, Kafulila alisisitiza kwamba ndoto ya Dira ya 2050 si ndoto ya kufikirika bali ni ajenda ya utekelezaji inayowezekana. “Mabadiliko haya yatawezekana tu endapo tutabadilika sisi pamoja na taasisi zetu. Hii ni safari ya nidhamu, sera madhubuti na mshikamano wa kitaifa,” alisema kwa msisitizo huku akimpongeza Rais Samia kwa kuiandaa na kuizindua Dira2050.



 
Back
Top Bottom