hakika amejenga hoja, labda tu kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kufuatilia niwape baadhi ya hoja alizojenga
1: kama kuna watu (ccm) ambao wanadai maoni ya watu 17000 juu ya kuwa na serikali 3 ni idadi ndogo sana ambayoyo haiakisi matakwa ya watanzania 46ml, je hawa wabunge 600 wanapata wapi nguvu ya kuwa na uwakilishi wa wananchi ili hali wao ni wachache zaidi kuliko hata hao waliotoa maoni juu ya kuwa na serikali 3?
2: Amehoji kama ishu ni kumtii mwl nyere ambae hakuta kuvunjika kwa muungano,wamesahau kuwa mwl alikuwa anabadilika kulingana na wakati. Mf mwaka 1965 mwl alifuta vyama vingivlakini kulingana na mabadiliko yaliyohitaji mageuzi mwaka 1992 ni mwl uyohuyo aliweze kuwa na vyama vingi ambavyo alivifuta hapo mwanzo. Akauliza je mwl angekufa kabla ya kuanzishwa vyama vingi inamaana mpaka sasa kungekuwa na chama kimoja tu?
3: Viongozi waliopo madarakani leo wafanikishe kuwa na muungano mzuri zaidi wa serikali 3 kwakuwa hii nafasi walionayo hawatakuwa nayo tena miaka ijayo kwani ni dhahir wingi wao (ccm) utapungua hivyo watalazimika kukubali mabadiliko kwa shinikizo kubwa kitu ambacho kitazalisha muundo mbovu zaidi . Hili alitoa kama ushauri kwa viongozi waliopo madarakani kutumia hii nafasi kufanya mabadiliko mazuri tena kwa busara kuliko kusubiri presha hapo baadae.