David Kafulila amfurahisha Kikwete

David Kafulila amfurahisha Kikwete

tamimusalim

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2014
Posts
1,822
Reaction score
499
Imethibitika kuwa jimbo la Kigoma Kusini ambalo linaongozwa na mbunge David Kafulila ndio jimbo pekee Tanzania ambalo shule zake zote za sekondari zimefanikiwa kuwa na maabara(laboratory) tena zenye vifaa vya kujifunzia kwa vitendo,

Jimbo hilo lenye shule 17 zenye maabara kati ya shule hizo, shule 3 zina mfumo wa kisasa kabisa kama simu, fax, na kompyuta. Akizungumza jana na ITV katika kipindi cha dakika 45 kafulila aliongeza kwa kipindi chake kilichosalia anataka kuakikisha shule zilizobakia zinapata, simu fax, na kompyuta,

Hali hiyo imemfurahisha sana JK kwani ameona ni mbunge pekee alieonyesha kwa 100% kwa vitendo kampeni yake kuakikisha kila shule inakuwa na maabara za sayansi katika mashule ya sekondari hapa nchini
 
Sasa hapo suala la kumfurahisha Rais ndio lilikuwa manifest au kuhudumia jamii???!!!
chukulia mfano wewe mkuu kama boss mfanyakazi wako katekeleza agizo lako tena ni mfanyakazi pekee uwezi kufulahi mkuu
 
chukulia mfano wewe mkuu kama boss mfanyakazi wako katekeleza agizo lako tena ni mfanyakazi pekee uwezi kufulahi mkuu

Boss wa mbunge ni mpiga kura wake ! Ndio maana kioengele sahihi ilikuwa asipofanya "yanayohitajika" na wananchi basi na afurushwe na walimchagua.

Hawakitaki hicho unajua ni kwa nini??!!
 
Naona na ww unataka mabishano basi hata wananchi wake wamempongeza sana maana kafanikisha malengo na katimiza sera
 
Sidhani kama kuna ukweli katika hili,mimi ninapafahamu huko asilimia kubwa ya jimbo hilo hakuna hata umeme
hizo kompyuta na fax zinatumikaje?
 
Nimemsikia Kafulila akihojiwa na ITV kipindi cha Dakika 45 usiku wa tarehe 17/11/2014 akisema kuwa mikataba ya gesi ina kipengele kinachosema kuwa itakuwa ruksa kuonwa ikihitajika na chombo cha dola kikiihitaji.Akasema bunge ni sehemu ya dola kwa hiyo mikataba inaruhusu waione lakini serikali haitaki kuwapa.
Je bunge ni kweli ni sehemu ya dola?
 
Atwambie mchango wake kwenye huo ujenzi ni kiasi gani au shilingi ngapi.
 
tamimusalim

Mh.Kafulila kwa sasa yuko kitaifa zaidi hadi majizi ya ESCROW yanyooshe mikono, hii mbinu yako ni kumbembelezA KAFULILA ALEGEZE KAMBA,
Tumbiri yuko imara lazima majizi yaswekwe rumande
 
Last edited by a moderator:
Na pia Mheshimiwa raisi amechukizwa na kitendo cha Kafulila kuendelea kupigia debe suala la ESCRO na IPTL !
 
Sidhani kama kuna ukweli katika hili,mimi ninapafahamu huko asilimia kubwa ya jimbo hilo hakuna hata umeme
hizo kompyuta na fax zinatumikaje?

Mkuu,

Kwanza sikubaliana na hicho kinachoitwa eti kumfurahisha rais, nafikiri hiyo sio kazi ya mbunge kumpima kama kwa analofanya linamfurhisha au vinginevyo, yeye anapaswa kuwafurahisha wapiga kura wake.

Vinginenvyo nakubaliana nna wewe kuwa maneno mengine yaliyotamkwa sio sahihi kuna changamoto nyingi zaidi kuliko kujisifia kwa ujenzi wa maabara, hata kama unaweza kuweka nishati ya umeme kwa njia mbadala lakini na kuzidisha chumvi kwa majigambo hayo

sana sana kuna baadhi ya maeneo ambako hawajhawahi kumwona mbunge wao tangu alivyoingia madarakani 2010 na hilo sijui kama linaweza kuingia katika orodha ya kumfurahisha rais mwenye sifa ya kufanya ziara mara kwa mara.
 
Atwambie mchango wake kwenye huo ujenzi ni kiasi gani au shilingi ngapi.

Siyo kazi ya mbunge kuchangia ujenzi. Chama cha mabusha ndio wabunge hawajui wajibu wao.

Kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia serikali kama kwenye hili la Escrow.
 
Back
Top Bottom