Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 2,167
- 1,923
===
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia nchi Tanzània PPPC Mhe David Kafulila amewaeleza Watanzania lazima wafahamu kesho ya Tanzània yao ni bora kama tu hali ya Umoja na mshikamamo iliyopo Sasa itaendelea kuwa ilivyo leo.
David Kafulila anasema, Tanzania kwa kushirikiana na sekta binafsi ( PPP) toka ndani au nje ya Tanzania wataipeleka kwa Kasi Tanzania kwenye Uchumi wa viwango vya juu kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo kwa miaka 25 ijayo ( 2025-2050 )
Mtakumbuka, David Kafulila amekuwa ni Mtendaji na mwanasiasa anayejikita zaidi kwenye kutetea hoja za Serikali yake kwa namba|takwimu na "fact" zenye kueleweka na watu wa Kada zote kitu kinachomfanya awe ni Mtendaji wa Serikali anayefuatiliwa zaidi mitandaoni na. Wananchi kwa sasa.
Mkurugenzi Mtendaji huyu anasema Tanzània mpaka kufikia mwaka 2050 kwa kushirikiana na PPP inatarajia kujenga Uchumi mkubwa zaidi wa $700bn ambazo ni zaidi ya TZS 1,750 Trilioni ambao ni karibu mara mbili ya Uchumi wote wa Africa ya Kusini ya leo ambao unafikia i karibu $380bn.
Kafulila anasema si kazi rahisi kujenga Uchumi wa $700bn kutoka Uchumi wa sasa wa Tanzania wa $85bn kwani ni kazi ambayo kamwe haiwezi ikatekelezwa kwa Kodi na Mikopo pekee hivyo sekta binafsi haiepukiki kwenye safari hii ya ujenzi wa Uchumi mkubwa kwa kipindi kifupi cha miaka 25.
Mkurugenzi Mtendaji huyu anaendelea kwa kusema jambo hili linawezekana bila mashaka yoyote kwani hata nchi ya Vietnam mwaka 1990 ilikuwa na Uchumi wa $6.4bn lakini leo Vietnam wana Uchumi wa zaidi ya $460bn sawa na ukuaji wa karibu mara themanini (X 80) zaidi.
HITIMISHO, Kama hivyo ndivyo ilivyo kwanini Tanzania tusiweze wakati Vietnam wao wameweza kwani wao Wana nini?
====