David Kafulila akosoa watu kujipa mamlaka ya CAG

yamindinda

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,581
1,318
KAFULILA AKOSOA WATU KUJIPA MAMLAKA YA CAG

1.KUHUSU HATI CHAFU:Awali ACT walisema CAG ametoa hati Chafu kwa hesabu Jumuifu za Serikali( Consolidated Account), walipoulizwa ni ukurasa upi CAG katamka hati chafu kwa hesabu hizo, Kiongozi wao kwenye mtandao wa Jamiiforum akasema ni ukurasa 298, Ilipofahamika hakuna kauli ya CAG kutoa hati Chafu katika ukurasa huo, wamebadili gia, sasa jana wanasema ilitakiwa mtu asome na kutafsiri mwenyewe. ( kujipa mamlaka ya CAG)

2.Narudia kusisitiza kwamba sio kila mwenye kusoma hesabu za ukaguzi ana mamlaka ya kutoa hati kwani hiyo ni Mamlaka ya CAG mwenyewe. Na CAG anatekeleza mamlaka hayo kwa kumujibu wa Viwango vya Kimataifa vya Ukaguzi wa Taasisi za Umma(ISSAIs) na Bodi ya Kimataifa ya Maadili kwa Kanuni za maadili ya wahasibu( Kanuni ya IESBA).

3.Ifahamike zaidi kwamba sio kila kasoro au mapungufu kwenye ukaguzi yanapelekea hati chafu, ndio maana kuna hati za aina NNE , na CAG anatoa hati kwa kuzingatia weledi na mamlaka yake kama nilivyoeleza awali. Nikwamsingj huo hoja ya Hati Chafu kwa hesabu jumuifu za Serikali( Consolidated Account) inabaki kuwa maoni ya ACT( kama walivyosema wenyewe kwamba walichambua) na sio CAG kama walivyotaka kuaminisha Umma hapo mwanzo.

4.KUHUSU TRILIONI 1.5: Awali ACT walitangaza kwamba CAG amebaini ubadhilifu wa trilioni 1.5 kutokana na hesabu zilizokaguliwa kuonesha kwamba Katika makusanyo ya trilioni25.3, Trilioni 23.8 ndizo zilitolewa kwajili ya matumizi.Baada ya kuwabana waseme ni mstari gani kwenye ukurasa huo wa 34 wa ripoti ya CAG ambapo CAG amehoji 1.5trilion na au kusema ni ubadhilifu?wakaona CAG hajasema lolote kuhusu tofauti hiyo ya kiasi kilichotolewa dhidi ya kiasi kilchokusanywa, Sasa Jana nimeona wamebadili gia kutoka kuwa fedha hizo ni ubadhilifu, sasa wanasema fedha hizo ni hazikaguliwa na kutaka kujua kwa nini hazikukaguliwa ,kwanini CAG hakusema lolote kuhusu fedha hizo na zipo wapi?( hili ndio swali ilitakiwa wahoji Awali)

5.Ukisoma mwenendo huo unaona kuna kucheza na akili za watu. Lakini kikubwa na muhimu ni kwamba kama tofauti hiyo ya 1.5trilioni kati ya fedha zilizokusanywa na zilizotolewa ina dosari yoyote ilikuwa lazma CAG aweke neno/hoja kama amevyofanya katika maeneo yote aliyokuta kasoro.

6. CAG kutoweka neno/hoja katika jambo hili(kama linavyosemeka ukurasa34) imetoa mwanya wa kila mtu kutafsiri anavyodhani. Nikwa msingi huo nakubaliana na hoja kwamba CAG aulizwe aliona nini kwenye eneo hilo kwani ndio hasa msingi wa yeye kukagua/kutambua dosari.

7.Aidha inawezekana mpaka hesabu za 2016/17 zilipofungwa, fedha hizo hazikuwa zimetumika, na sio ajabu kwani hata ngazi ya halmshauri kumekuwa na changamoto ya fedha kutotumika na kwisha wakati hesabu zinapofungwa, na CAG ameripoti Mara kadhaa tatizo hilo, ingawa makatibu wakuu na wakurugenzi wamekuwa wakijenga utetezi kuwa sheria ya manunuzi na kipindi pesa zinaingia imekuwa vigumu kuhakikisha fedha zote zinatumika ndani ya mwaka wa fedha husika kwasababu ya hatua za manunuzi zinazopaswa kufuatwa kisheria.

8. Aidha inawezekana ukweli kuna matumizi ambayo CAG hakuweza kuyakagua kwasababu hayakufanyika au kupitia kwenye mfumo wa hesabu za Serikali.kama nilivyosema awali kwamba katika bajeti ya 2016/17, kati ya fedha zaidi ya trilioni3 kutoka washirika wa maendeleo , sehemu ya fedha ya fedha hizo( nasisitiza sehemu), matumizi yake hayakupitia mfumo wa matumizi ya Serikali( Rejea hotuba ya Bajeti 2017/18 kipengele kinachohusu Mapitio ya matumizi kwa mwaka uliokwisha 2016/17 ambao ndio ukaguzi huu unahusika , hotuba ambayo iliyosomwa 2017 kabla hata CAG hajatoa repoti hii).

9.Nikwa msingi huo, kwamba kwakuwa CAG anakagua matumizi yaliyopitia kwenye mfumo wa serikali upo uwezekano wa CAG kwamba hakukutana na matumizi hayo kwakuwa washirika hao wa maendeleo/zamani wahisani walipeleka fedha zao moja kwa moja kwenye miradi bila kufuata mfumo wa matumizi ya Serikali. Nikatika mazingira kama hayo hatuwezi kuhitimisha jumla tu kwamba fedha ambazo hazikutumika mpaka hesabu zilipofungwa kuwa ni ubadhilifu/ufisadi.Hata halmashauri fedha ambazo CAG amekuta zilipokelewa na halmashauri lakini hazikutumika mpaka hesabu za mwaka zilipofungwa, hazijawahi kuitwa ufisadi.

10.Hakuna mahala CAG kasema fedha hizo ambazo hazikutolewa kwa matumizi hazipo, pengine ndio sababu hakufanya jambo hilo kuwa moja ya hoja kwenye ripoti yake.
Kwamba katika mambo ambayo CAG amehoji kwenye ripoti yake hilo halimo, lakini kwakuwa limeibua mjadala kitaifa, bila Shaka Kamati ya PAC italifanya kuwa sehemu ya hoja ili Serikali ijibu rasmi na endapo CAG ataridhika na majibu hayo ataifunga hoja hiyo.Ndio mfumo!

11. KUKOPA NA KUTUMIA NJE YA BAJETI; Mtazamo wangu katika hoja kwamba Serikali imekopa zaidi ya mpango wa bajeti na imelipa madeni ya zamani nje ya mpango wa Bajeti ni kwamba hili ni kasoro kiutaratibu kama CAG mwenyewe alivyohoji,Ingawa nikasoro katika bajeti nyingi tangu bunge la9&10. Hotuba za Kamati za Bunge zimekuwa zikirudia kuhoji hali hiyo kujirudia, na zaidi siku za nyuma ilikuwa pesa imetumika nje ya bajeti kugharamia safari za viongozi nje ya nchi kwa gharama zaidi ya bajeti iliyopitishwa.Sasa zinatumika nje ya bajeti kulipia madeni ya nyuma! sitetei kasoro hiyo iendelee hata kama kulipa madeni ni jambo jema, isipokuwa ifahamike kwamba hali hiyo sio mpya,kwamba imeanza awamu ya 5.Kasoro hii imekuwapo miaka mingi na ikiondolewa itakuwa mafanikio ya bunge la 11 na Serikali ya awamu ya5 dhidi ya mabunge yaliyopita na Serikali zilizotangulia.

David Kafulila
Aprili18,2018.
 
"Katika makusanyo ya trilioni25.3, Trilioni 23.8 ndizo zilitolewa kwajili ya matumizi.Baada ya kuwabana waseme ni mstari gani kwenye ukurasa huo wa 34 wa ripoti ya CAG ambapo CAG amehoji 1.5trilion na au kusema ni ubadhilifu?"
.
NGEDERE KAWA SERIKALI
hata Zitto hakusema CAG kaita ubadhirifu..
ALICHOHOJI NI WAPI ZILIPO TRILIONI 1.5 ?
ambazo hazina maelezo..
POMBE badala ya kusema zilipo analaumu mitandao..
NGEDERE LAZIMA ATETEE MAANA POMBE HAKUHONGA TU MADIWANI HATA NGEDERE walipata
 
Tumbili nafasi za uteuzi zimeshaisha
 
Njaaa ya wanasiasa w tz ni mbaya mno...kafulila ngoja asubir kwanza uteuz
 
Kafulila baada ya kumkosoa Mnafiki Mwenzie Zitto lipaswa sasa atuambue Consolidated Financial report for the year 2016/17 Serikal ilipata hati ipi?
 
Back
Top Bottom