Umenifurahisha sana kwa hii conclusionSisi ni wamoja, zaidi ya JF hatuna pakusemea. Hongera JF. Heri akina Kafulila wanauwezo wa kuwakusanya waandishi wa habari kibao na kusema watakavyo, nasi tukaamini.
Idumu JF!!!!
Nashangaa, hivi ni wangapi wabovu huko?well said, He was supposed to step down even before he was fired
So, next is Zitto? how come is one of the top leaders?
No hapa anaongelewa - Kolimba, Kabeho, Kibona, Mama Mbatia, Kombe, mkemia mkuu wa serikali, Stan Katabalo, na wengine wengi waliopitia chinja chinja ya ccm.
Hapo hujaweka wale waandamanaji wa pemba au mauaji ya Jan 2001.
1) Alianguka kutoka ghorafani..kwahiyo inawezekana ana matatizo ya akili..swali mbona sasa hivi? mbona chadema ilimfanya kiongozi muda wote?
2) Hajamaliza shule ame-disco..gosh? mbona sasa hivi? mbona alikuwa kiongozi wenu muda wote?
Akiondoka ndio mnapekua historia yake na siyo kabla ya kumpa nafasi hiyo kwa muda wote huo ni unafiki na sizitaki mbichi hizi lol.
Kinachofanyika sasa na vyama vya upinzani ni sensitization na advocacy u kutokana na size ya vyama hivyo!!
Upinzani wa kweli uko ndani ya CCM na kuna siku utajitokeza
Hii si tu ni test of time, bali ni mapinduzi kamili ndani ya chama yenye mwelekeo wa kufungua milango ya uwazi na uadilifu.Dhahabu safi hupita katika moto mkali. Lets see if Chadema will survive the test of time!!
Tetesi za kufukuzwa uanachama, bwana Kafulila zilijitokeza toka kwa wana Paparazi siku nyingi tu kabla hata ya yeye mwenyewe kukutana na waandishi wa habari.
Habari zilivuma huku wasomaji wakidai vyanzo vya habari hizo bila mafanikio. Leo hii kuna chanzo maalum ikwa ni yeye mwenyewe akithibitisha kufukuzwa uanachama. Kinachonisikitisha mimi ni pale anapoonyesha kuukubali uamuzi huo kwa shingo upande, pale asemapo: "Ninaondoka CHADEMA kwa uchungu mkubwa kwasababu ya lengo thabiti kwamba lazima niitumikie nchi yangu katika harakati za siasa, na. Nitaikumbuka sana CHADEMA kwakuwa nilimwaga damu katika ujenzi wa chama hiki, ninalazimika kukaa pembeni."
Huwezi kuitumikia nchi yako ipasavyo ukiwa ndani ya chama ambacho kinamapungufu mengi kama aliyoyaeleza Kafulila katika pres conf. Aidha anaendelea kusema kuwa " ".......ninawaheshimu sana viongozi wa CHADEMA." Huwezi hata kidogo ukawaheshimu viongozi wasiojua kazi yao au wanaotaka kuendeleza ufisadi ndani ya CHAMA. Kwa maneno mengine wanakiandaa chama kushika nchi ili kuendeleza ufisadi. Ni kosa kabisa kuwaheshimu viongozi kama hao. Kwanza kazi, ndio baadae heshima. Ukichemsha katika kazi hakuna heshima. Kwa upande mwingine nahisi kama vile Kafulila anajilaumu, kuwa kwanini alianzisha kuhoji utawala katika chama, kwani asingefanya hivyo bado angekuwa anakula kuku.
Katika pres conf yake, kulijaa tuhuma zifuatazo zikiwaendea viongozi wajuu wa CHADEMA wakiwemo, M/Kiti, Freema Mbowe, Dr Slaa n.k
1. Matumizi mabaya ya Ruzuku
2.Taratibu za fedha ndani ya Chama
3.Ufinyu wa Demokrasia (Mbowe vs Zitto/uchaguzi M/Kiti. Uchaguzi M/kiti vijana, yeye mwenyewe akiwa mgombea)
Kifupi yote hayo hapo juu ni mambo ya FWEZA, kazi ipo. Sasa chama kisichokuwa wazi katika mambo ya fedha, tutadiriki vipi kukipa nchi. Matatizo haya niliyajadili siku za nyuma, si mara moja bali mara nyingi tu. Lakini kwa bahati mbaya kama alivyoeleza Kafulila, kuwa wana CHADEMA ni wagumu sana kujirekebisha. NA MBISHI HAFAIDI MPAKA SIKU YA IDD.
Kafulilo ameendelea kwa kutoa ujumbe muhimu sana kama ninavyounukuu hapa chini:
"Taifa linapita katika kipindi kigumu sana chenye misukosuko ambayo msingi wake ni siasa duni ambazo msingi wake ni upinzani dhaifu kwa upande mmoja na Chama tawala kilicho choka kwa upande wa pili"
Yote hayo ni tisa, lakini kumi kama anajihisi kuwa kafulia bila kukusudia basi aombe msamaha kwa CHADEMA na arudi madarakani.
Haya tuseme huyu Kafulila ni mjinga, na Zitto je? Maana kwa muujibu wa wapambe, naye anatia maji kichwa chake baada ya mwenzie kunyolewa.Kafulila nilimsikiliza kwenye taarifa ya habari TCB1. Huyu kijana ni mpuuzi sana. Hata maelezo yake ni ya kitoto. Kifupi anataka sifa asizostahili, kifupi hajai hata kwenye kiganja.
Kafulila nilimsikiliza kwenye taarifa ya habari TCB1. Huyu kijana ni mpuuzi sana. Hata maelezo yake ni ya kitoto. Kifupi anataka sifa asizostahili, kifupi hajai hata kwenye kiganja.
Zitto ni ngangari hafuati mkumbo. ataendelea kuwapo CHADEMA na utashangaa!!Haya tuseme huyu Kafulila ni mjinga, na Zitto je? Maana kwa muujibu wa wapambe, naye anatia maji kichwa chake baada ya mwenzie kunyolewa.
Vizuri, na hilo ndio tunaloombea, maana kuhama chama si ufumbuzi wa matatizo.Zitto ni ngangari hafuati mkumbo. ataendelea kuwapo CHADEMA na utashangaa!!
Vizuri, na hilo ndio tunaloombea, maana kuhama chama si ufumbuzi wa matatizo.
Wangapi wamehama vyama kwa kizingizio eti wanatafuta chama makini, pale ambapo wao watawatumikia wananchi zaidi kwa uwezo wao wote. Hayo hayajatoke, kwani Tambwe Hiza na wenye mawazo kama yake, hawawezi kutueleza kuwa leo baada ya miaka eti wanatumikia wananchi zaidi kuliko alivyokuwa CUF.
Tunachoona ni kinyume, kuwa wote hawa wahama vyama, imani ya wananchi kwao inapungua kwa kiasi kikubwa sana. Leo hii Tambe ndani ya CCM hana mchango hata kidogo. Na hali kama hiyo tumeiona kwa Mrema.
Hivyo maombi yamgu ni kuona wanasiasa wanakuwa na malengo ya muda mrefu yatayowawezesha kujua toka awali kuwa katiba na muelekeo wa chama gani wapo tayari kuutumikia maishani mwao mwote. Malengo ya muda mfupi, kama kupata cheo chamani kamwe hayatamnufaisha yeyote, si watanzania, chama wala muhusika.
Siasa za Tanzania ni tofauti sana na Kenya, sitaingia kiundani.Sifikiri mtu kuhama chama ni tatizo mbali ni pengine mbinu mahili kabisa zakuweza kuwatumikia wananchi vizuri.
Mfano . Hakuna mwasiasa Afrika mashariki ambaye amebadirisha vyama vingi kama Raila Kalamanjogi Odinga.
Kama mtu ana nia ya kweli na sababu za msingi ,kuhama chama sio tatizo na wananchi wataendelea kuunga mkono tu hata ukihama mara ngapi.
Tatizo naloliona hapa watu tunajaribu ku reference kusiko. Kama mtu alihama chama kwa nia yake mbaya hakumzuii mtu mwingine kuhama chama kwa nia yake nzuri.
Watu mnaowaliference ni watu ambao wamehama kwa nia zao binafsi wenda za kinafiki ama wao wajuavyo.Na kinachowamaliza ni kwa sababu ya unafiki wao na si kuhama chama , kwa sababu kamwe Shetani huwa havumilii kukufichia siri yeye atajitahidi kukufichia siri kwa mda usio mwafaka na kuitoboa siri kwa mda muafaka.
Mimi ninachojaribu kusema hapa Kama kafulila kahama kwa unafiki basi shetani atamfichia siri hiyo kwa mda tu kwa wakati usio mwafaka, na ikifika wakati mwafaka shetani ataitoa hiyo siri na kujamaliza mwenyewe. Lakini kama hakuhama kwa kinafiki shetani hana siri ya kutoboa na Mungu hata mhukumu kwa lolote.
Kama CHADEMA ndo wanafiki basi watambue unafiki wao unafichwa kwa mda tu usio mwafaka na mda muafaka utapotimua shetani atatoboa siri na ktk mda mwafaka na sahihi na hatimaye kitawamaliza kabisa.