David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Posts
4,201
Reaction score
254
Samahanini jamani, nasikitika kuwataarifu kuwa yule aliyekuwa Ofisa
Habari wa Chadema Kafulila kajivua uanachama leo. Chakujiuliza chama
hiki kinaelekea wapi?
 
Samahanini jamani, nasikitika kuwataarifu kuwa yule aliyekuwa Ofisa
Habari wa Chadema Kafulila kajivua uanachama leo. Chakujiuliza chama
hiki kinaelekea wapi?
Kama habari hii ni kweli (maana Shy hueleweki), hakuna shida huo ni utashi wake.
 
Naamini nidhamu katika chama ni muhimu kuliko kitu kingine chochote. Kuhama chama si suluhisho la matatizo. Alihama Mrema CCM na bado CCM ikaendelea, sembuse David Kafulila Chadema!!

Slaa na Mbowe imarisheni nidhamu katika chama ili kuepuka migongano isiyo na tija kama hii inayotokea CCM sasa!!
 
Karibu CCM Kibunango hebu mtafutie kadi huyo kijana wenu!
 
Kama kajivua uanachama, sio kitu kibaya ni utashi wake,Lakini kama angekuwa kafukuzwa nadhani hiyo ndio ingekuwa habari. jJpo, kuondoka kwake inaweza kutafsirika ni kukiri mapungufu yake!
 
Samahanini jamani, nasikitika kuwataarifu kuwa yule aliyekuwa Ofisa
Habari wa Chadema Kafulila kajivua uanachama leo. Chakujiuliza chama
hiki kinaelekea wapi?
Sasa kwanini unaomba msamaha? Au huna uhakika na habari unayotupa? don't be submissive my friend. Kama ni kweli, hiyo ndio demokrasia, hajafungwa miguu mle Chadema!

Hata wale wa CCM, wanaopiga makelele kila siku bila mafanikio, wakijisikia kuondoka waondoke tu!
 
Huu ni muda muafaka wa kila mtu kukaa upande anaotaka. heri wanachama kumi makini kuliko 100 mashaka mashaka
 
Unajua ukubwa wa Pua si wingi wa Makamasi. UNajua wakiwa wengi Ufisadi utakuwa mwingi wakiwa wachache na Jasiri ndo wataijenga Nchi. Tumeona mangapi Wangapi wamekiama cha lakini bado kipo Imara. Mimi nasema unajua kwenye mfereji wa maji yanayoitiririka mabua utayaona yanajitenga pembeni. haya Nenda kachukue kadi yako ya zamani na usije tena Shuwaini!!! mtu mzima atishiwi nyau. kafie mbele.
 
Ujana! The guy is good. Akumbuke "Ujana ni harakati na uzee ni maono" Akikua ataacha. Tumpe Muda.
 
Shy una uhakika? maana habari zako kuziamini huwa inakua ngumu sana
 
Samahanini jamani, nasikitika kuwataarifu kuwa yule aliyekuwa Ofisa
Habari wa Chadema Kafulila kajivua uanachama leo. Chakujiuliza chama
hiki kinaelekea wapi?
Kafulila nenda baba, tangulia tu, upinzani unataka watu makini na waadilifu wasio na mawaa, unatia shaka, umekosa uadilifu, hata CCM hawataki watu rahisi kama wewe, upinzani hauna hofu nawe, huwezi kuboboa CHADEMA, huwezi kamwe. wewe ni sisimizi tu.
 
haya Nenda kachukue kadi yako ya zamani na usije tena Shuwaini!!! mtu mzima atishiwi nyau. kafie mbele.
Mtakie safari njema, siyo mateke na magumi!! Dunia duara, bado ni kijana Taifa linamuhitaji. Jisahihishe kama ulikosea na pia Muombe Mungu atakusaidia mbeleni.
 
Mtakie safari njema, siyo mateke na magumi!! Dunia duara, bado ni kijana Taifa linamuhitaji. Jisahihishe kama ulikosea na pia Muombe Mungu atakusaidia mbeleni.
Bado nashindwa kumjadili Kafulila kwa habari iliyoanzia kwa Shy, kama kuna mtu mwingine wa kututhibitishia habari hii itakuwa jambo la kheri.
 
Huu ni muda muafaka wa kila mtu kukaa upande anaotaka. heri wanachama kumi makini kuliko 100 mashaka mashaka

Shalom, big up man, maake hawa watakuja kutusumbua baadae, anaweza kwenda CCM kama anataka kuchukua chake mapema, make wakina Marando wapo wengi, nafikiri hata ndani ya CHADEMA kuna akina Marando wengi, tunahitaji watu makini kwa kipindi hiki kuelekea 2010 na sio wababaishaji kama huyo jamaa na kundi lake.

halafu kuhama chama sio ndo kutatua matatizo yake, chamuhimu ni kuijenga nidhamu na uzalendo ndani ya nafsi yao.
 
Mtakie safari njema, siyo mateke na magumi!! Dunia duara, bado ni kijana Taifa linamuhitaji. Jisahihishe kama ulikosea na pia Muombe Mungu atakusaidia mbeleni.

Aaa! Hebu sahihisha..
 
Hivi huyu bwana kosa lililomfanya mpaka avuliwe wadhifa wake lilikuwa nini? Tusije tukamhukumu bila kujua kisa hasa ni nini. Isije kuwa alionewa ki kweli na kusababisha yeye kufikia hatua hii.
 
Hivi huyu bwana kosa lililomfanya mpaka avuliwe wadhifa wake lilikuwa nini? Tusije tukamhukumu bila kujua kisa hasa ni nini. Isije kuwa alionewa ki kweli na kusababisha yeye kufikia hatua hii.

Alisema kwenye Majira Nov 8 na Mwananchi Nov 9 kuwa Mbowe na Dr Slaa wamefanya kikao kisicho rasmi cha Gheto huko Dodoma na kufikia maamuzi ya kumvua uanachama. Akaitwa na sekretariati ya chama kuhojiwa akakiri kwamba kweli amesema maneno hayo. Akaambiwa athibitishe kuwa kikao cha Dodoma kilijadili kumfukuza uanachama akasema hana ushahidi wowote ila ameelezwa maneno hayo na waandishi wa habari. Akaambiwa akanushe maneno yake, akakataa. Akaambiwa aombe msamaha, akakataa. Uteuzi wake ukatenguliwa kutokana na kukiuka maadili ya chama kifungu cha 10 kinachokataza viongozi kutoa siri za chama, kuzingatia mipaka ya kimamlaka katika kutoa kauli za chama, kuepuka kuwatuhumu viongozi wengine hadharani bila kupitia vikao halali vya chama na kuacha kutoa tuhuma za uongo

serayamajimbo
 
Source: Shy angalieni msije kuwa mnapoteza muda! Shy uko wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom