David Kafulila aibwaga serikali

David Kafulila aibwaga serikali

Lisu aliwahi kumtetea Jakobo Zuma na akashinda,Zito na Msando walitegewa bomu na Lisu wakajilipua wenyewe
 
Tundu Lissu ww Ni jembe, Leo nmekuona pia Mwanza ukimtetea Mh. Ester bulaya
 
Neema yanukia jamaa kawekewa sana mapingamizi

Wakina DHAIFU na genge lake la ESCROW wanaogopa kuwa Kafulila akirudi mjengoni atalipua ile kashfa upya na itabidi watajwe wale waliochukua fedha kwenye viroba kutoka Stambic!!
 
wasimpe kwanza yule mama mkopo make hatakaa bungeni hata kwa miezi mitatu
 
Kesi hii kama kafulila angeweka wakili mzuri angeshinda,ila huyu wakili wake ndg Daniel Lumanyila hana uzoefu na anaelea sana kwa wakili wa hasna ndg fungamtama.nayasema haya kwasababu nimeudhuria kesi hii tangu mwanzo,hata jana trh 14/1/2016 nilikuwepo mahakamani.Ni huruma tu ya jaji ndo inayofanyika hata wakili msomi tundu lissu alimwambia jana kafulila kuwa tafuta wakili mzuri.
 
Kesi hii kama kafulila angeweka wakili mzuri angeshinda,ila huyu wakili wake ndg Daniel Lumanyila hana uzoefu na anaelea sana kwa wakili wa hasna ndg fungamtama.nayasema haya kwasababu nimeudhuria kesi hii tangu mwanzo,hata jana trh 14/1/2016 nilikuwepo mahakamani.Ni huruma tu ya jaji ndo inayofanyika hata wakili msomi tundu lissu alimwambia jana kafulila kuwa tafuta wakili mzuri.
Hii ni hatari sana.
Kama hana wakili mzuri atajikuta anashindwa kesi kwa sababu za kipuuzi.
Kafulila anapaswa azingatie sana jambo hili
 
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam Rumanyika leo Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa serikali yalowasilishwa na kujadiliwa Jan11, 2015 katika mahakama hiyo.

Katika mapingamizi ya serikali Wakili wa serikali kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa serikali aliweka mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya Kafulila David kwa madai kwamba;

1. Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii

2. Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani ya uwezo wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi

3. Kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria.

Katika uamuzi wa MAHAKAMA, Jaji Rumanyika amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na utetezi wa Wakili wa Kafulila imeamua kuwa;

1. Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua KESI hii haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida na zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015, kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazima kutaja ukweli ulio hayana.

2. Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya 2015 kifungu112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi alochaguliwa na hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi hilo.

3. Kuhusu pingamizi kuwa ombi la Kafulila la kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, MAHAKAMA imelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo.

Baada ya maelekezo na maelezo hayo, Mahakama haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama ilivyombwa na wakili wa serikali na badala yake Kesi itaendelea January 28, 2015
Haki ya Mtu haipotei, wataiba, wataipora, watadhulumu lakini Mungu akisema NDIYO hakuna wa kusema hapana. Kafulila subira huvuta heri. Waliodhani umepoteza wasubiri waone. Mungu akutangulie Kafulila unahitajika sana kipindi hiki hapa Tanzania
 
au mm sioni vizuri kuna kitu hakipo sawa juu ya taarifa hii kesi kuendelea january 28 2015
 
Back
Top Bottom