David Kafulila aibwaga serikali

Mzee Mchopu

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
1,031
268
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam Rumanyika leo Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa serikali yalowasilishwa na kujadiliwa Jan11, 2015 katika mahakama hiyo.

Katika mapingamizi ya serikali Wakili wa serikali kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa serikali aliweka mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya Kafulila David kwa madai kwamba;

1. Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii

2. Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani ya uwezo wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi

3. Kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria.

Katika uamuzi wa MAHAKAMA, Jaji Rumanyika amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na utetezi wa Wakili wa Kafulila imeamua kuwa;

1. Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua KESI hii haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida na zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015, kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazima kutaja ukweli ulio hayana.

2. Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya 2015 kifungu112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi alochaguliwa na hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi hilo.

3. Kuhusu pingamizi kuwa ombi la Kafulila la kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, MAHAKAMA imelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo.

Baada ya maelekezo na maelezo hayo, Mahakama haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama ilivyombwa na wakili wa serikali na badala yake Kesi itaendelea January 28, 2015
 
Last edited by a moderator:
Mungu yupo pamoja nawe kafulila na Tanzania inakuhitaji utashinda uongo hauwezi shinda ukweli Bali unachelewesha tu ukweli kujulikana
 
TE="imamuAbasi, post: 15096990, member: 291924"]akishinda kafulila haki imetendeka lakn ikishinda serikali hakuna haki nchi hii ni vituko[/QUOTE]
Haki inashinda dhulma
 
Mara nyingine serikali inakuwa na usumbufu kwa baadhi ya watu hasa wapinzani pasipo sababu ya msingi. Kwani hawakujua kuwa kesi hiyo ilikuwa batili/invalid kwa kukosa vigezo hivyo? Au ni usumbufu tu usio na maana na upotezaji muda. Hizo ndio sababu za malimbikizo ya kesi mahakamani alizokataa Mh. Magufuli
 
mie naomba mnisaidie sijaelewa vizuri jamani. kwamba kesi kuendelea kusikilizwa January 28/2015? hii ilikuwa kesi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014? na sasa kesi yake tayari ilisikilizwa January 28/2015 kwani Kafulila alikuwa anamtetea mwekiti nani wa serikali za mitaa ambaye ccm walimchakachua, je maamuzi yaliendaje. vinginevyo sijaelewa hiyo January 28/2015 mleta maada anamaanisha nini.
 
Mara nyingine serikali inakuwa na usumbufu kwa baadhi ya watu hasa wapinzani pasipo sababu ya msingi. Kwani hawakujua kuwa kesi hiyo ilikuwa batili/invalid kwa kukosa vigezo hivyo? Au ni usumbufu tu usio na maana na upotezaji muda. Hizo ndio sababu za malimbikizo ya kesi mahakamani alizokataa Mh. Magufuli

Wana JF,

Kuhusu hili la kesi ya Kafulila kuna kila pingamizi kutoka serikali ya Magufuli ili kesi hii ifutwe kabisa ili Kafulila apoteze haki yake ya kutaka kurudishiwa Ubunge alioshinda lakini akanyang'anywa na manyang'au wa CCM.

Tunajua kabisa Serikali ya CCM kwa sasa chini ya Magufuli hawataki kusikia kabisa jina la David Kafulila likirudi Bungeni. Hii ni mikakati ilisukwa hata kabla ya Uchaguzi ili kumkomesha Kafulila kwa kuidhalilisha serikali ya CCM chini ya Jakaya Kiwete alipoibua sekeseke la Akaunti ya Tegeta Escrow.

Kashfa ya Escrow bado mbichi lakini kwa maksudi Serikali ya CCM wameamua kuipotezea ili isiendelee kuwasumbua. Kitendo cha kumrudisha Prof. Muhongo kwenye Wizara hiyo hiyo iliyomfanya ajiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow ni dalili tosha kuwa CCM wanataka kuendeleza ubabe wa kulinda maslahi yao.Hivo wanataka kuhakikisha David Kafulila harudi Bungeni.

Tusubiri.
 
Hongera Kafulila na Mungu atakupigania na tuko nawe kushinda udhalimu, BORA KUFA UKIWA UMESIMAMA KULIKO KUISHI UKIWA UMEPIGA MAGOTI.
 
Hivi ukiwa ukiwa mbunge wa ccm unasimamiwa na mwanasheria kutoka serikalini ila ukiwa upinzani unatafuta mwanasheria wako kwani hii kesi ni juu ya kafulila na tume ya uchaguzi au ni kesi ya kafulila na mgombea wa ccm naomba kusaidiwa wanajamii
 
Back
Top Bottom