David Kafulila aibwaga serikali

David Kafulila aibwaga serikali

Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam Rumanyika jana Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa serikali yaliyowasilishwa na kujadiliwa Januari 11, 2016 katika mahakama hiyo.

Katika mapingamizi ya serikali Wakili wa serikali kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa serikali aliweka mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya Kafulila David kwa madai kwamba;
  1. Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii
  2. Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani ya uwezo Wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi
  3. Kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria

Katika uamuzi wa Mahakama, Jaji Rumanyika amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na utetezi wa Wakili wa Kafulila imeamua kuwa;
  1. Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua KESI hii haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida na zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015, kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazima kutaja ukweli ulio hayana.
  2. Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya 2015 kifungu112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi alochaguliwa na hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi hilo.
  3. Kuhusu pingamizi kuwa ombi la Kafulila la kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, Mahakama imelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo

Baada ya maelekezo na maelezo hayo, Mahakama haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama ilivyombwa na wakili wa serikali na badala yake Kesi itaendelea Januari 28, 2016.
 
Last edited:
mie naomba mnisaidie sijaelewa vizuri jamani. kwamba kesi kuendelea kusikilizwa January 28/2015? hii ilikuwa kesi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014? na sasa kesi yake tayari ilisikilizwa January 28/2015 kwani Kafulila alikuwa anamtetea mwekiti nani wa serikali za mitaa ambaye ccm walimchakachua, je maamuzi yaliendaje. vinginevyo sijaelewa hiyo January 28/2015 mleta maada anamaanisha nini.
Ni January 28, 2016 Mkuu. Hiyo ni kesi ya Ubunge ktk uchaguzi wa Oktoba 2015.
 
mie naomba mnisaidie sijaelewa vizuri jamani. kwamba kesi kuendelea kusikilizwa January 28/2015? hii ilikuwa kesi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014? na sasa kesi yake tayari ilisikilizwa January 28/2015 kwani Kafulila alikuwa anamtetea mwekiti nani wa serikali za mitaa ambaye ccm walimchakachua, je maamuzi yaliendaje. vinginevyo sijaelewa hiyo January 28/2015 mleta maada anamaanisha nini.
Shauri hilo litaendelea tarehe 28 kipi usichoelewa
 
Hivi ukiwa ukiwa mbunge wa ccm unasimamiwa na mwanasheria kutoka serikalini ila ukiwa upinzani unatafuta mwanasheria wako kwani hii kesi ni juu ya kafulila na tume ya uchaguzi au ni kesi ya kafulila na mgombea wa ccm naomba kusaidiwa wanajamii
Hii ni kesi ya kikatiba
Hapo unakua unaishitaki tume ya uchaguzi kwa maana ya mkurugenzi na pia mwanasheria mkuu wa serikali anakua party to the institution
Umenielewa mkuu
 
Kafulila akishinda hii kesi atanipunguzia machungu ya uchaguzi mkuu kwa 50%
Kila la kheri.
 
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam Rumanyika jana Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa serikali yaliyowasilishwa na kujadiliwa Januari 11, 2016 katika mahakama hiyo.

Katika mapingamizi ya serikali Wakili wa serikali kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa serikali aliweka mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya Kafulila David kwa madai kwamba;
  1. Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii
  2. Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani ya uwezo Wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi
  3. Kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria

Katika uamuzi wa Mahakama, Jaji Rumanyika amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na utetezi wa Wakili wa Kafulila imeamua kuwa;
  1. Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua KESI hii haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida na zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015, kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazima kutaja ukweli ulio hayana.
  2. Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya 2015 kifungu112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi alochaguliwa na hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi hilo.
  3. Kuhusu pingamizi kuwa ombi la Kafulila la kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, Mahakama imelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo

Baada ya maelekezo na maelezo hayo, Mahakama haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama ilivyombwa na wakili wa serikali na badala yake Kesi itaendelea Januari 28, 2016.

Pingamizi la wakili wa serikali limenifanya niwaze kwa sauti kwamba ile ofisi aliyotaka Naibu Speaker ifungwe rasmi.Maana nikisoma sababu za kutaka kesi itupiliwe mbali hata mie niliyesoma St.Kayumba naelewa kwamba Matokeo ya ubunge yanahojiwa na kama yakikutwa yanamakatizo basi aliyeshindwa sababu ya MAKATIZO hupewa ushindi wake na aliyeshinda kwa kutumia nguvu za dola hunyang'anywa.

Sasa huyu mwenzetu sheria hizi amezitoa wapi??

Masikini Tanzanaia yangu ndiyo sababu serikali haijawahi kushinda hata siku moja
 
mie naomba mnisaidie sijaelewa vizuri jamani. kwamba kesi kuendelea kusikilizwa January 28/2015? hii ilikuwa kesi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014? na sasa kesi yake tayari ilisikilizwa January 28/2015 kwani Kafulila alikuwa anamtetea mwekiti nani wa serikali za mitaa ambaye ccm walimchakachua, je maamuzi yaliendaje. vinginevyo sijaelewa hiyo January 28/2015 mleta maada anamaanisha nini.

Tumekuelewa, ni Kesi ya Kafulila walipigana pambano la ngumi featherweight WBO, alishinda ila majaji wakachakachua point na mpinzani wake akashinda unanimously!

Ilikuwa mwaka 2013 mwishoni, Kafulila alipoteza mkanda aliokuwa akiushikilia.
 
Sote tunajua kuwa anachokifanya Kafulila sio kitu rahisi maana anashindana na nguvu kubwa lakini kwa kuwa kasimama katika haki na ukweli, nasi tumwombee kwa ajili ya ustawi wa kizazi hiki na kijacho.
 
Kafulila akishinda hii kesi atanipunguzia machungu ya uchaguzi mkuu kwa 50%
Kila la kheri.

Nifah!
Mambo ya kisiasa ukiyaweka sana moyoni huumiza sana hasa kipini cha uchaguzi ambapo mgombea wako anaposhindwa. Pole kwa machungu anyway.
 
Kwa kweli utu anaoonyesha ndugu Tundu Lissu kwa David Kafulila ni wa kuigwa mfano!

Amekuwa naye bega kwa bega akimsaidia kuhusu sakata lake mahakamani! Hakika unastahili pongezi!

Leo nilikuona ndugu Lissu ukiwa na gari yako Toyota Prado ukiwa siti ya nyuma huku David Kafulila akiwa siti ya mbele maeneo ya Africana! Ulikuwa bize kuchambua mambo mbalimbali huku Kafulila akikupa dondoo za hapa na pale! Nimejaribu kuulizauliza kabla ya kupost nikaambiwa kuwa umekuwa ukimpigania sana! Hongera sana!

Nimependezwa na jinsi mlivyokuwa kwenye gari! Zaidi ya ndugu! Mlikuwa mkijitahidi kupata mambo mbalimbali ili kulikabili hili "JITU CCM" lililokaa kufikiria jinsi ya kupora haki kwa gharama yoyote ile! Nimefarijika sana baada ya kuwaona wewe na Kafulila mkifurahi mara kwa mara mlipokuwa ndani ya gari haijalishi Kafulila alivyotendwa!

Tutafika tu!! Hongera sana! Kafulila tuko pamoja!
 
Hakuna atakayechukia Kafulila akipewa Ubunge wake
 
ndo maana Obama alisema "Lissu is more likely to be th president in the near future '' alipokuwa akiongea na Uhuru Ikulu Nairobi
 
lissu ni muungwana sana. aliwahi kuwatetea kina kigwangallah mahakani bure bila hata kulipwa senti. hongera sana lisu...
 
Napenda sana ushirikiano hasa unapokuwa unalenga katika kutokomeza dhuruma.
 
Back
Top Bottom