David Kafulila ahamia NCCR Mageuzi akitokea CHADEMA

David Kafulila kuhamia NCCR



Kuna nyepesinyepesi kuwa yule sisimizi wa CHADEMA kuhamia NCCR MAGEUZi kama alivyodai yeye kuwa anahitaji kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini.

ebu edit hilo neno mkuu, huyu ni mtu kama wewe, ana maamuzi yake na yeye sio wa kwanza, kwa lolote lile anabaki na utu wake kama mtu. unless kama una definition nyingine

Mods hii imakaaje?
 
ebu edit hilo neno mkuu, huyu ni mtu kama wewe, ana maamuzi yake na yeye sio wa kwanza, kwa lolote lile anabaki na utu wake kama mtu. unless kama una definition nyingine

Mods hii imakaaje?

Ala wewe hujui Slaa akisema inakua imehalalishwa??
 
Mwacheni kijana apige siasa. Mambo ya kupeana mikosi haya ya nini kama sio fitina. Mtu unasafiri hata kabla ya kupanda chombo watu wameshaanza nafikiri hiki chombo kitapinduka ama kuwaka moto kabla hakijafika. Huu ni u roho ya korosho. Kumuombea mwezako madudu

Hapa umenena mkuu, yaani kuna watu wana roho za korosho na fitna hadi wanaombea wenzao madudu. Ukiwasoma washabiki wa Mwakalinga hapa JF, utakubaliana nami kuwa wanamuombea mabaya Mwakyembe.
 
Mbona tunamsema sana kafulila peke yake, Vipi viongozi wa CHADEMA kama walkuwa hawampendi na kumbagua,hapa namaanisha pale alipotaka kugombea na kwa dhahir wakamkatalia asigombee na kumtaka mtu wao. Ingekua wewe je ungefanya na watu kazi ambao hawakujali na kukuthamini. Wangemwacha kura ndo zimtoe na si mtu binafsi.
Hata mcheza mpira akiona kocha hampendi lazma ajikate zake, hata ningekua mimi ningeondoka tu.

Si hata wewe una haki ya kusema hayo (kama ulivyoanza hapa kusema). Sio lazima mass ikufuate nyuma mkuu Semenya. Sema (andika) tu utasikika.
 
Zitto alirudi nyumbani ccm muda mrefu uliopita?
I beg to correct you, si kweli kwamba Zitto yuko sisi m hapana! hizi ni siasa nyingine za kupakana matope tu.
Hata hivyo nashangaa kwamba Kafulila kwa nini hakuamia sisi m kama wapinzani wengi wafanyavyo wakidhani wanakomoa upinzani huku wakijikomba kwa wezi wa rasilimali zetu.
 
Wakuu
DAVID Kafulila yule jamaa aliyejivua uanachama CHADEMA na kuhamia NCCR amekataa kukabidhi kadi ya CHADEMA na kudai kwamba ni mali yake. Pamoja na kuktaa kukabidhi kadi hizo pia Kafulila alionekana amevaa sare ya CHADEMA kwa jina maarufu la kombati katika kikao na waandishi wa habari alipokuwa akikabidhiwa kadi ya NCCR.Alipohojiwa kwanini amevaa vazi la CAHDEMA alidai kwamba lile sio vazi la CADEMA bali ni mali yake.Kwa hali hii nina mashaka na kijana huyu huenda akawa ana siri nyuma ya pazia na bado anaipenda sana CHADEMA.
 
unataka kutuambia kuwa nikivaa shati la kijani nitakuwa mwana CCM? yeye ndie aliyevaa na bahati nzuri kaulizwa na katoa jibu kuwa ni mali yake so nini cha kujadili?
 
unataka kutuambia kuwa nikivaa shati la kijani nitakuwa mwana CCM? yeye ndie aliyevaa na bahati nzuri kaulizwa na katoa jibu kuwa ni mali yake so nini cha kujadili?

Kuvaa shati la kijani hakumaanishi ni CCM ila kuna aina ya mashati ya kijani ukivaa basi wewe ni CCM,Ukivaa shati lenye maandishi CCM,CCM ni vazi la CCM. Kombati ni vazi la CHADEMA weither you like or not.
 
Kuvaa shati la kijani hakumaanishi ni CCM ila kuna aina ya mashati ya kijani ukivaa basi wewe ni CCM,Ukivaa shati lenye maandishi CCM,CCM ni vazi la CCM. Kombati ni vazi la CHADEMA weither you like or not.

sijakuelewa unapolazimisha kuwa kombati ni vazi la CHADEMA!!
 
Kombati si vazi la Chadema kama ilivyo green siyo rangi ya CCM. Green and Kombati was there before vyama hivyo. hoja ya msingi hapa ni aina gani ya green na kombati ndivyo tunaweza tukavilink na chama. Lakini mnatakiwa kukumbuka kwamba vazi la Kombati siyo la Chadema bali ni vazi ambalo linatokana na mapenzi binafsi ya mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambaye alicopy kutoka kwa mwanasiasa maarufu wa Italia Benito Belcos Mussolin na baadae likavaliwa sana na Fidel Castro. Hata Hitler naye alikuwa mara chache akiacha kuvaa nguo zake za kijeshi alikuwa ana vaa kombati. Kifupi ni vazi la mafishisti na madikteta wa kipindi hicho. Kama kombati ni vazi la chadema je wale makamanda wa UVCCM ambao huvaa kombati za kijani na ufito wa njano mtasema wamevaa vazi la chadema? kwa sababu makamanda hao walikuwepo kabla ya chadema na bado wapo. Kwa hiyo kulink kombati ya kafulila na mapenzi yake kwa Chadema kama siri iliyofichika ni hoja dhaifu kujadiliwa na watu makini. Kwa bahati mbaya hizo kombati zao hata hawajaweka nembo za chama chao ili kuonesha utofauti na zile za migambo wa serikali za kijiji na vitongoji. Kafulila yupo sahihi alipo sema vazi lile ni la kwake kwa sababu anajua historia ya vazi hilo ndiyo maana hata lile analovaa mbowe mwenyewe halina nembo ya CHADEMA.
 
Kama kwa KIHA Kafulila maana yake kafulia, huyu dogo atakuwa kafulia kweli kwenda NNCR-MAGEUZI. Hiki chama kimebaki kwenye register ya Tendwa tu.
 
Tangu muda mrefu gazeti la Mwananchi limekuwa likiandika kuhusu kinachoitwa mgogoro ndani ya CHADEMA limekuwa likiandika mambo mengi sana ya uongo kuhusiana na mambo mbalimbali na haswa kuhusu Kafulila na CHADEMA Kigoma Kusini.

Soma hapa;


Date::11/22/2009
Swahiba wa Zitto akimbilia NCCR


clip_image001.jpg



Ramadhan Semtawa
DAVID Kafulila, aliyejitoa Chadema kutokana na kuondolewa kwenye sekretarieti ya chama hicho, amejiunga rasmi na NCCR Mageuzi ambayo ina ngome kubwa kisiasa kwenye jimbo la Kigoma Kusini, ambako amepanga kuwania ubunge mwakani.
Kafulila, ambaye hadi sasa bado ni mshirika mkubwa wa naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, alijitoa kwenye chama hicho wiki iliyopita kutokana na kile alichokieleza kuwa ni kunyimwa haki ya kuchaguliwa na mizengwe ya baadhi ya viongozi wa juu.
Jana Kafulila, ambaye alikuwa ofisa habari wa Chadema, alitangaza uamuzi wake akisema: "Nimejiunga NCCR kutokana na dhamira yangu binafsi, kupokea ushauri kwa watu ninaowaamini na kuwaheshimu pamoja na wapigakura wangu."
"Huu ni wakati wa kufanyakazi ya siasa, si kupiga kelele na malumbano. CCM imeshindwa kuongoza nchi kwa hiyo kazi iko kwetu ili tuweze kuingia kwa wingi bungeni."
Kafulila, akiwa na mwenyekiti wa NCCR, James Mbatia na mkuu wa idara ya haki za binadamu na sheria, Dk Sengodo Mvungi, alisema hata waliompa ushauri, walimweleza kuwa dhamira yake itatimia akijiunga na NCCR.
"Walionishauri ni watu ninaowaheshimu... nilijiridhisha na ushauri wao na walinihakikishia kuwa njia sahihi ya kutimiza ndoto ya kile ninachokiamini ni kuingia NCCR."
Takwimu za matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Oktoba, zinaonyesha kuwa NCCR ni chama chenye wafuasi wengi katika jimbo la Kigoma Kusini ikifuatiwa na Chadema.
NCCR inashikilia vijiji 11 ambavyo vingi viko katika tarafa ya Nguruka ambayo ina asilimia 40 ya wapigakura wote katika jimbo hilo huku Chadema ikiwa na vijiji 12 eneo la mwambao wa Ziwa Tanganyika likiwa na wakazi wachache, lakini nguvu hiyo pia ikielezwa kutokana na ushawishi na juhudi binafsi za Kafulila.
Kafulila alisema wapigakura wa jimbo hilo walimweleza kupitia viongozi mbalimbali kwamba maamuzi yaliyokuwa yakifanywa dhidi yake ni hujuma.
Alifafanua kwamba wapigakura hao walimuwekea bayana kwamba hata afanyiwe nini, hawatasita kumpa kura katika uchaguzi wa ubunge mwakani.
Kafulila aliongeza kwamba angependa ndoto yake itimie kwa vyama vya upinzani kujizolea viti vya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao ili viweze kufanya maamuzi mazito ndani ya Bunge.
"CCM imeshindwa kutuongoza, wengine wanasema afadhali ya mkoloni. Mwaka 1959 watu waliokuwa wameunganishwa na kupata umeme ilikuwa ni asilimia 15 sasa hivi imeshuka, mwaka 1974 takwimu za idadi ya watu wasiojua kusoma ilikuwa ni asilimia 10 mwaka 2007 ilifikia asilimia 30,"alifafanua Kafulila.
"Ndiyo maana, ningependa kuona siku NCCR inapata viti 30 vya ubunge, Chadema nayo labda viti 30, CUF nayo pia... hapo tutakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi bungeni."
Alisema mapungufu hayo yanaonyesha umuhimu mkubwa wa vyama kufanya kazi ya siasa na kuacha kupiga kelele na akaongeza: "Kukosoana ndani ya vyama ni jambo zuri kwani linalenga kutupa nafasi ya kujisahihisha."
Swahiba huyo wa Zitto alitumia fursa hiyo pia kutoa ufafanuzi kwamba alijiunga katika siasa akiwa kidato cha pili mwaka 1998, na kuweka sawa rekodi akisema hakuna mtu wa makao makuu ya Chadema aliyemwingiza kwenye siasa mwaka 2005.
"Sasa anapotokea mtu akisema aliniingiza kwenye siasa mwaka 2005, sijui anakuwa anamaanisha nini; kwamba au ili uwe mwanachama ni lazima uwe makao makuu Dar es Salaam," alihoji.
Naye Mbatia alisema umefika wakati sasa vijana wenye uwezo wa kuongoza wapewe nafasi na akataka wanasiasa watende yale ambayo wanahubiri na yaliyokubaliwa katika ilani na katiba zao.
Alisema mfumo uliopo sasa unamweka kijana katika nafasi ngumu kutokana na baadhi ya watu kukataa kuwapa fursa na kuhoji, :"Kila siku vijana ni taifa la kesho, tunao viongozi wakuu humu wana miaka hata 70."
Mbatia aliongeza kwamba mfumo huo mbovu ambao unanyima fursa vijana umehamia na kutafuna hadi kambi ya upinzani nchini ambayo ilipaswa kuwa chachu ya mageuzi.
Alisema NCCR imempokea Kafulila atakuwa na uhuru wa kukosoa kwa mujibu wa katiba na taratibu za chama, katika mambo ambayo yameanishwa katika nyaraka mbalimbali za chama hicho.
Dk Mvungi alisema vyama vingi ni njia ya kufikia malengo ya kulinda uhuru wa kiuchumi na kisiasa na kuongeza kwamba, endapo mtu ataona chama fulani kinajiendesha kwa mfumo wa chama dola kama CCM, yuko huru kuhamia kwingine ili kufanya mageuzi.
Dk Mvungi aliongeza kwamba huu si wakati wa kushambulia wanaohama chama kimoja kwenda kingine, bali ni wakati wa kuhakikisha vyama vinashiriki katika mageuzi yaliyokusudiwa wakati wa kuanzisha mfumo wa vyama vingi.
Alisema ndio maana NCCR imekuwa kimya licha ya baadhi ya wanachama wake kukimbilia vyama vingine kwa kuwa kazi kubwa imekuwa ni kufanya mageuzi.
Kafulila na mwenzake Danda Juju walifukuzwa na katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wiki moja iliyopita kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu na kuvujisha siri za chama.
Hata hivyo, Zitto ameonekana kupinga uamuzi huo, akiwataka viongozi wenzake kuwa waaangalifu katika maamuzi, hasa katika kipindi hiki ambacho Chadema imetikiswa kutokana na uchaguzi wa viongozi wake wa juu.

Na leo wameandika tena uongo mwingine ,
maswali ya kujiuliza ni kama yafuatayo;
1.Je? Gazeti la Mwananchi lina masilahi gani?
2.Wanaandika kwa masilahi ya nani?
3.Wametumwa na nani?
4.Waandishi wa habari hizi kila siku ni ama Ramadhani Semtawa au Fidelis Butahwe.
5.Gazeti la Mwananchi mara nyingi limekuwa likiandika kuwa CHADEMA wana nguvu kubwa Kigoma kusini , leo wanasema ni NCCR je? wanataka kutrupeleka wapi?

Nimekuwa nikijiuliza maswali haya sana kwani linaonekana linafanya kazi maalum na haswa linapokujua suala la CHADEMA .
Wanaojua watuelimishe hapa,.
 
hawa watu njaa tupu, sijui hata gazeti lipi lakuliamini sikuhizi...

ukionekana unamisimamo wanakurubuni unajiunga nao HOPELESS

hata huyo kafulila simkubali hata chonde, nae njaa tupu!
 
Wenyeviti 11 wa mikoa wa CHADEMA wamepinga uamuzi wa Dr Slaa wa kutengua uteuzi wa David Kafulila. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo tarehe 14 Novemba, ambalo halijataza majina wala mikoa ya wenyeviti hao, wenyeviti hao wanaelezwa kuutafsiri uamuzi huo kuwa ni kuendeleza kambi za uchaguzi wa chama hicho wa septemba 2009.

Habari hiyo inaeleza kuwa wenyeviti hao wanaamini kwamba David Kafulila alikuwa ndiye kinara wa kambi ya Zitto Kabwe. Habari inaeleza kwamba wenyeviti hao wanamsubiri Dr Slaa kwenye kikao cha Kamati kuu ya chama hicho kilichopangwa kufanyika Nov 27 na 28 waweze kumpinga.

Habari hiyo imemnukuu Katibu wa CHADEMA mkoa wa Kigoma akieleza kwamba wao bado wanamtambua David Kafulila kuwa ni Afisa wa chama kwa kuwa hajapewa barua rasmi na makao makuu kuelezwa kwamba uteuzi wake umetenguliwa.

Aidha katibu huyo, anayefahamika kwa jina la Msafiri Wamalwa amemueleza Kafulila kuwa ni Afisa anayetoka katika Mkoa wake Jimbo la Kigoma Kusini ambapo ni kati ya maeneo ambayo chama hicho kimefanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kwa upande wake David Kafulila ameeleza kuwa alipokea mwaliko wa kuhudhuria kikao kilichoitishwa na Mo Ibrahim hapa Tanzania chini ya Katibu wa zamani wa UN Koffi Annan.

Ukisoma habari hii ya Mwananchi walikuwa wanafanya sppining eti kuwa wenyeviti wa mikoa 11 wa CHADEMA walipinga uamuzi huo na wakaahidi kukutana na Dr.Slaa kwenye Kamati Kuu.

Ukitaka kujua ni sppining utagundua kuwa wenyeviti wa mikoa sio wajumbe wa kamati kuu kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA , sasa wao waliandika bila hata kusoma katiba ya CHADEMA.

Hili ni gazeti makini ila kwa sasa linaelekea kupoteza soko kwa sababu ya kutumika ama waandishi wake waandamizi kutumika .
 
Kombati si vazi la Chadema kama ilivyo green siyo rangi ya CCM. Green and Kombati was there before vyama hivyo. hoja ya msingi hapa ni aina gani ya green na kombati ndivyo tunaweza tukavilink na chama.... Kwa bahati mbaya hizo kombati zao hata hawajaweka nembo za chama chao ili kuonesha utofauti na zile za migambo wa serikali za kijiji na vitongoji. Kafulila yupo sahihi alipo sema vazi lile ni la kwake kwa sababu anajua historia ya vazi hilo ndiyo maana hata lile analovaa mbowe mwenyewe halina nembo ya CHADEMA.

nakubaliana na Albano kuhusu kombati.
ila Kafulila yuko wrong kwa kung'ang'ania kadi ya chadema, as najua kadi na vitambulisho sio mali ya mtu binafsi, ni mali ya organisation wanayotoa, na ndio maana wanaweza kukunyang'anya.
sasa kafulila kama ni mstaarabu (i doubt kama yuko hivyo) arudishe tu kadi ya chadema, yeye si kawahama? sasa anang'ang'ania kadi yao ya nini?
hapo anatufanya tuwe na shaka na nia yake!
 
Back
Top Bottom