David Kafulila ahamia NCCR Mageuzi akitokea CHADEMA

Remmy

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
4,701
1,799
David Kafulila kuhamia NCCR

Kuna nyepesinyepesi kuwa yule sisimizi wa CHADEMA kuhamia NCCR MAGEUZi kama alivyodai yeye kuwa anahitaji kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini.

Yule aliyekuwa Ofisa Habari wa Chadema, amekaribishwa muda mfupi uliopita ndani ya chama kingine cha upinzani cha NCCR-Mageuzi.

David Kafulila alikikimbia Chadema mapema wiki hii inayomalizika leo na kuwatuhumu viongozi wa chama hicho, Freeman Achikaeli Mbowe na katibu wake mkuu, Dk. Wilbroad Slaa, amepokewa na Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia jijini Dar es Salaam na kupewa kadi ya uanachama.

Kafulila amesema kuwa ameamua kujiunga na NCCR kwa kuwa huko anaamini ataendeleza jitihada zake za kuimarisha upinzani Tanzania, ingawapia nadhani anajipanga ili kutimiza ndoto yake ya kuwania ubunge Kigoma Kusini baada ya kunusa kuwa Chadema wasingempitisha.

Kafulila, hadi anapewa kadi hiyo, ni mwanachama wa kawaida tu, ingawa kuna tetesi kuwa ameandaliwa cheo fulani hapo makao makuu, hasa cha habari ili kuanza kazi ya 'kuipaisha' NCCR mbele ya umma wa Watanzania.

Tusubiri tuone mwisho wake
 
kuna nyepesinyepesi kuwa yule sisimizi wa CHADEMA kuhamia NCCR MAGEUZi kama alivyodai yeye kuwa anahitaji kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini.

Acha uzushi na chuki zisizo na hoja, thread ya chini hapo umeandika kuhusu huyuhuyu david nakusema atamwaga damu....acha hizo jiheshimu..mtu mwenyewe bado u kinda sana kilingeni hapa.
 
Yule aliyekuwa Ofisa Habari wa Chadema, amekaribishwa muda mfupi uliopita ndani ya chama kingine cha upinzani cha NCCR-Mageuzi.

David Kafulila alikikimbia Chadema mapema wiki hii inayomalizika leo na kuwatuhumu viongozi wa chama hicho, Freeman Achikaeli Mbowe na katibu wake mkuu, Dk. Wilbroad Slaa, amepokewa na Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia jijini Dar es Salaam na kupewa kadi ya uanachama.

Kafulila amesema kuwa ameamua kujiunga na NCCR kwa kuwa huko anaamini ataendeleza jitihada zake za kuimarisha upinzani Tanzania, ingawapia nadhani anajipanga ili kutimiza ndoto yake ya kuwania ubunge Kigoma Kusini baada ya kunusa kuwa Chadema wasingempitisha.

Kafulila, hadi anapewa kadi hiyo, ni mwanachama wa kawaida tu, ingawa kuna tetesi kuwa ameandaliwa cheo fulani hapo makao makuu, hasa cha habari ili kuanza kazi ya 'kuipaisha' NCCR mbele ya umma wa Watanzania.

Tusubiri tuone mwisho wake
 
Makosa yanaendelea

Umesema yote Mpita Njia.Kama wana siasa vijana wangejifunza kutofanya maamuzi wakati wa hasira, makosa kama haya yangeepukwa. Muda si mrefu, atajutia uamuzi huu. Nafuu angekaa bila chama kwa muda, hata thamani yake ingepanda. Angeanza kuposwa na vyama na kuwaringia kweli kweli.
 
Ni haki yake kikatiba kuwa mahali popote anapoona panamfaa kisiasa.
Kila la heri David Kafulila. Binafsi nakutakia heri na mafanikio katika maisha yako ya kisiasa. Usijali mabezo hiyo ndiyo si hasa.
 
bora tu na huko nccr asipewe wadhifa utakaomgonganisha
na mtu mwengine. kwani huko nccr inawezekana akawepo mtu ambaye
anaweza ona kafulila "anazuia ndoto zake za kuendeleza mageuzi" lol.

yangu macho masikio ya wenyewe
 
==

Yuko Ruhuza anapenda Microphone kama nini. Kafulila anapenda Mic pia.
Kuna showdown inakuja. Tujipe muda.
 
Mwacheni kijana apige siasa. Mambo ya kupeana mikosi haya ya nini kama sio fitina. Mtu unasafiri hata kabla ya kupanda chombo watu wameshaanza nafikiri hiki chombo kitapinduka ama kuwaka moto kabla hakijafika. Huu ni u roho ya korosho. Kumuombea mwezako madudu
 
Hongera Mkama
 
Mbona kwa Rwakatale kuhamia CHADEMA hamkuongea leo hii Kafulila kwenda NCCR tayari kmeongea,mpeni muda afanye kazi ni haki yake kikatiba, kumbukeni mawazo ya mtu ndio Serikali yake.
 
KILA siku nazungumzia siasa na uvumilivu,
hebu tuangalie hizi trend
Mrema alipotoka CCM kuja NCCR ilibidi mtu apigwe chini ili yeye achukue uenyekiti, lakini mwisho wa yote na yeye mwenyewe alikimbia NCCR, alipoingia TLP vilevile kuna mtu alitolewa uenyekiti ili apewe yeye(Mrema) na mambo tunayaona sasa hapo TLP,
Lwakatale alipotoka CUF, ili apewe cheo CHADEMA ni lazima mtu atolew hapo(Kafulila?), ili lwakatare apewe cheo, na hata KAfulila kupata cheo NCCR ni lazima mtu atolewe kwenye hiyo nafasi na mwisho wa yote hao wanaoamia hivyo vyama vipya, hawaendi kuimarisha vyama bali ni kuanzisha au kukza migogoro
maskini upinzani wa Tanzania unatia kinyaaa
 
Mbona wote wapinzani wametoka ccm ,nitajie mmoja ambaye hajahama chama??
NB: exclusive vijana.
 
Huyo ndo kwisha kazi kajimalza mwenyewe. Tatizo kubwa kwa sisi vijana tunapenda sana mabo faster, hatuna uvumilivu hata kidogo. tunapowaona wazee kama warioba, salim, ndesamburo, slaa na wengine hawakufikia mafanikio on the day walikubana na mambo mengi na magumu. Kama NCCR watakuwa wanaelewa wa wasimpatie uongozi ili uone kama hatatimuka tena.
 
mmmhh!! huyu mtu anataka ubunge tu kwani huku kwetu kaona hapati kitu akaamua kufungasha virago sasa tuone huko aliko je nini kitatokea. Upinzani wa Tz matata kweli kweli
 
Huyo ndo kwisha kazi kajimalza mwenyewe. Tatizo kubwa kwa sisi vijana tunapenda sana mabo faster, hatuna uvumilivu hata kidogo. tunapowaona wazee kama warioba, salim, ndesamburo, slaa na wengine hawakufikia mafanikio on the day walikubana na mambo mengi na magumu. Kama NCCR watakuwa wanaelewa wa wasimpatie uongozi ili uone kama hatatimuka tena.

Mbona Slaa naye alihama baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea ccm? mbona yeye hakusubiri kutafakri?? alihama mara moja baada ya kinyimwa nafasi ccm kugombea ubunge.

KAfulila yeye ni kosa kuhama kama alivyohama Slaa.

Humu JF bwana
 
Mkama, \
Mashine yenu kali, jipongeze tu.
 
NCCR ni chama mfu. Ni mzoga tu ambao tunauona. Kafulila alijengwa na Chadema. NCCR hakina uwezo wa kufanya hicho.

Je yeye atakifanyia nini NCCR? Remains to be seen...but no much hope
 
Back
Top Bottom