Ukitazama efforts zilizofanywa na "projects in hand" za umeme utakuta tunakos a umeme kwa ajili ya watendaji wachache tu na si kuwa hakuna efforts, wazembe wachache ama kwa matamanio yao ama kwa kutowajibika ipasavyo ndio wanaichafua "system" na hizo bugs lazima ziwe eliminated one way or the other.
Matatizo tulio nayo ya umeme sasa hivi, sio kuwa hatuna mitambo ya kutosha kuondosha mgao au kumaliza kabisa hili tatizo, la hasha. Tatizo ni watendaji wabovu kama huyu Jairo wa wizarani na wengine pale Tanesco. Kuna habari za kuaminika kabisa (ushahidi nnao) kuwa baada ya sheria mpya ua umeme,kuna watu wametaka kuja kuwekeza kwa fedha zao lakini wamewekewa vizingiti pale wizarani, na nani? huyo huyo Jairo. kuna wawekezaji wamemuandikia email kuhusu kuwa na nia kabisa ya kuwekeza kwenye umeme, lakini hata kuwajibu hakuwajibu na hao watu anawajua na wameshafanya kazi hapa Tanzania (in the past). Kwa nini hajawajibu? kwa sababu alikuwa anajuwa akianza mawasiliano nao atakosa ulaji. Ushahidi nnao.
Nimebaki najiuliza sana toka jana, hivi inawezekanaje Katibu mkuu aandike barua ambayo Waziri wake hana taarifa nayo?
Hivi anayesoma bajeti bungeni ni katibu mkuu au waziri? kama moto wa bungeni nani anaupata zaidi kama si waziri?
Majibu ya maswali yangu ni kwamba Katibu ni wajibu wake kutenda yale anayoagizwa na Bosi wake na kwamba si katibu pekee kaitenda hii dhambi bali na waziri kashiriki kikamilifu na lazima alikuwa anajua kuhusu huu mshiko.
Hatuna utamaduni wa kuwajibika, lakini kwa hili, Waziri husika, waziri mkuu walitakiwa kujipima wao wenyewe kisha waachie ngazi.
Au wanakuja na hadithi ndefu ya "tulikuwa tunamjua huyo, ushahidi ninao"Ulikuwa wapi usiweke hapa jamvini? Mbona GT aliweka huu uzi long time!FF acha cheap popularity! Kama una ushahidi peleka kwa Hosea TAKUKURU, si ndo utaratibu siku hizi?Halafu watu wanakuja na kukandia JamiiForums, au Mitandao inachafua watu nk!!
Au wanakuja na hadithi ndefu ya "tulikuwa tunamjua huyo, ushahidi ninao"Ulikuwa wapi usiweke hapa jamvini? Mbona GT aliweka huu uzi long time!FF acha cheap popularity! Kama una ushahidi peleka kwa Hosea TAKUKURU, si ndo utaratibu siku hizi?
Hata mm nilishangaa nilipoona Obama na blackbery!au ni FFalitaka kutupotezea?
Big up JF!hii issue ya Jairo niliisomaga humu humu longtime ago!nashukuru leo nime refresh my mind!
hivi yule mama sio shelukindo?Yule Mama (Mbunge) aliyesema kwamba JF inachafua watu, anatakiwa afute kauli yake.
hapana virus nisije ua my pc kama alivyo ua umemeGT,
hebu mtumie email Jairo akupe mtizamo wake anapatikana hapa: jairodk27@yahoo.com
Source:http://info.worldbank.org/etools/docs/library/96829/Tanz_0404/Ta_0404/Xtracking Participant List.doc.
Samahani kidogo, KTK hawa wawili kwenye picha, Jairo ni yupi!Hivi kwa nini hawa wawili hawana ushirikiano kwenye kazi zao...maana saa zingine huwa nawaona kama vile DUMB & DUMBER lakini mmoja na hasa Jairo kwa nini amekuwa mjinga kama Salva?
Na la muhimu zaidi kwa nini Jairo unamwongopea rais kuwa WEBSITE si kitu cha muhimu au ndio unaleta uhuni wako kama wa mzee LUHANJO?
Hivi hii aibu mtaendelea kuitia aibu Ikulu mpaka lini?
Aliyevaa miwani ndio Jairo mkono wa KushotoSamahani kidogo, KTK hawa wawili kwenye picha, Jairo ni yupi!
Hahahaha!!! Hapo sasaHalafu watu wanakuja na kukandia JamiiForums, au Mitandao inachafua watu nk!!
Aliyevaa miwani ndio Jairo mkono wa Kushoto
aliyekuwa katibu wa rais bwana david jairo ambaye wiki iliyopita amechaguliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini amekuwa akimtisha mbunge wa ilala mussa azzan maarufu kama zungu ambaye ni mwenyekiti wa kamati inayoshughulikia majengo ya machinga complex.
jairo anataka apewe kazi ya zabuni ya matangazo kwenye majengo hayo bila kufuata taratibu zinahusika.
david jairo alipotakiwa kufuata taratibu kwa kampuni yake kuomba tenda kama kampuni nyingine amekuwa mbishi na kumtisha zungu kuwa yeye(jairo) ni mtu wa karibu sana wa rais jk hivyo kama atakosa basi zungu ajue kuwa kakalia kuti kavu.
maswali kwa david jairo kwani hajui kuwa ikulu iko jimbo la ilala ambako zungu ni mbunge? zungu ni mbunge wa rais.
na kama rais ana jambo lake atawasiliana na zungu moja kwa moja sio wewe jairo.
zungu kachaguliwa na wananchi sio wewe jairo,lakini lazima uelewe kuwa majengo haya ni ya wamachinga wewe jairo unataka nini? Kwani wewe ni mmachinga?
mheshimiwa rais mtizame kwa macho mawili jairo anatumia vibaya jina lako.wewe ni rais wa watanzania wote wanaoweza kutuzidi kimapenzi kwako ni familia yako na watu wa jimbo lako la chalinze walitupa fursa ya kukupata.kwani bila wao kukuchagua kama mbunge wao sisi kama watanzania tusingeweza kufaidika na uwezo wako.
kama jairo anawatisha watu kwa vitangazo vya machinga complex na sasa umempeleka madini na nishati ikitokea dili za richmond anaweza kuwa na roho ngumu na kutenda haki?
shame on you jairo.