David Beckham yupo Tanzania

David Beckham yupo Tanzania

IMG-20170602-WA0019.jpg
 
Habari wana JF, nimeona picha instagram David Beckham yupo na watoto wake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

Hapa ndiyo serikali yetu upande wa utalii inapofail, ingekua wenzetu Kenya mtu kama Beckham wangetangaza ujio wake kwa kiasi kikubwa.

Mwenye taarifa yoyote kuhusu ujio wake anaeza akatoa maelezo.
Sio kila mtu maarufu anayekuja kutalii anatangazwa,mambo ya kutangazwa ni makubaliano ya mgeni kama atataka kutangazwa wengine hawapendi ,hata huko Kenya kuna maceleb kibao huingia na kutoka bila kutangazwa,hata mjukuu wa malikia wa uingereza kuna wakati aliweza kukaa hata mwezi huko Lewa bila watu kujua kama yupo Kenya
 
Wale mnasema kwamba watanzania Ni washamba kuliko wakenya kwenye mambo ya kutangaza utalii mnamatatizo..hivi mmejiuliza kwann becks kaamua kuja bango na sio Kenya!?au nyie ndo mlimueleza habari za Serengeti! Na tanzania?acheni kujidharau..!!
 
Si ajabu utajiri alionao beckam ukawa unawakaribia wakina Ronald na messi ukae ukijua kufuria kwa mchezaji aina ya beckam ni kuizalilisha uengereza.
 
Kama kaja kutalii tu haina haja ya kumtangaza, acha ainjoi privacy na familia yake. Angekuja kwa madhumuni mengina kama vile kupromoti soka au ziara ya kikazi angetangazwa. kama kaja kimyakimya wacha akae kimyakimya na ataondoka kimyakimya. kwanza ni mtu wa kawaida tu, kuna wabongo wengi tu hawamjui wala hawajawahi sikia jina hili.
we kweli pimbi
 
huyu si ndio alipokutana na JK pale santiago bernebeu wakati anacheza real mdrid JK alivyoenda kumsalimia na kumkaribisha bongo alisema haijui TZ mpaka alivyotajiwa mlima kilimanjaro....sasa nini kimemleta kama sio ufukunyuku na umbea...siku hizi hata hasikiki na mpira wake ulishaisha kitaaambo.....apite kushoto tu
Chekesha sana mzee baba
 
Itakuwa aliona matangazo ya vivutio vyetu katika michezo ya ligi ya uingereza,Kazi nzuri ya mkwele na waziri wa utalii enzi hizo mueshimiwa nyalandu Leo tunaona faida ya hayo matangazo.
 
Ma thread kama haya mi.huwa natamani mapicha tu
 
upload_2017-6-3_6-56-4.png

Nimependa hicho Ki-Englsih cha "enjoy your stay in a Tanzania" Hiki mbona kama cha Baba Bashite vile? Kazi yipoooooo!!!
 
Tatzo lako umezoea kingereza cha tense.
Kiingereza bila tense hicho siyo grammatical!! Hiki Kiingereza chenu cha akina Bashite ni tatizo!! Hiyo sentence ni broken English kwisha habari!!
 
Tupunguze kushoboka jamani, huenda anareasons zake za kutaka privacy
 
Back
Top Bottom