David Beckham yupo Tanzania

Nadhani amekuja kutalii kama familia privately huwezi tena kwanza kufanya naye matangazo au sijui matamasha au makongamano.

Ila kwa waandishi watundu na wajanja wanaweza Hata kufanya naye appointment na Hata kufanya mahojiano na kituo kimoja cha TV akiwa ktk hotel yake alikofikia.

Ni nafasi pekee ya kuonyesha weledi wa taaluma ya uandishi na uwanahabari kwa ujio wa David Beckam
 
Kashafulia huyo!! wangekuja watu walio kwenye chati kama CR 7 au MESSI uone kama shuguli za uzalishaji uchumi sisingesimama kwa muda hapo bongo. Huyo ana tofauti gani na ile timu ya wazee ya real madrid iliyokuja bongo?
 
Habari wana JF, nimeona picha instagram David Beckham yupo na watoto wake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

Hapa ndiyo serikali yetu upande wa utalii inapofail, ingekua wenzetu Kenya mtu kama Beckham wangetangaza ujio wake kwa kiasi kikubwa.

Mwenye taarifa yoyote kuhusu ujio wake anaeza akatoa maelezo.
Anataka privacy ndo maana yeye pia hakutoa taarifa!
 
Nilimuona na nikampiga na ile sweet smile yake, na kumtajia jina alipachikwa enzi hizo. picha naona uvivu kurusha. Nilirushia wa karibu yangu hukoooo

Juu ya utaliiii, subirini Kenya waibe picha kutangaza yupo nchini kwao.

Hata siwasemi hao wa utaliii, wengi hawajui mengi. Wanabidi wajiongeze kijiditali pia hata kuwa na staff wanaofanya kazi fulani fulani...naona uvivu kuzitaja.
Nawe kila kitu unaona uvivu, sasa unatoa comment ya nini kama unaona uvivu?
 
Habari wana JF, nimeona picha instagram David Beckham yupo na watoto wake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

Hapa ndiyo serikali yetu upande wa utalii inapofail, ingekua wenzetu Kenya mtu kama Beckham wangetangaza ujio wake kwa kiasi kikubwa.

Mwenye taarifa yoyote kuhusu ujio wake anaeza akatoa maelezo.
Mkuu hebu fafanua kidogo.Kama wangetangaza ujio wake ni kitu gani kingefanyika?
 
Lakini bado ni celebrity mkubwa sana na mambo yakimwendea vizuri atakuwa owner wa timu USA muda si mrefu ujao.
Inawezekana yeye ni mzee kuliko Beckham kutokana na ugumu wa maisha....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nguli wa soka la Uingereza na familia yake wametua Bongo usiku huu Mwenye taarifa zaidi wa ujio wake na lengo lake tafadhari aongeze Nyama kwenye Uzi huu
 
hii habari ipo humu tangu jioni,huo usiku unaousema wewe ni upi,au aliondoka afu karudi tena saiv?
rudi kamalizie usingizi wako..
 
Kama kaja kutalii tu haina haja ya kumtangaza, acha ainjoi privacy na familia yake. Angekuja kwa madhumuni mengina kama vile kupromoti soka au ziara ya kikazi angetangazwa. kama kaja kimyakimya wacha akae kimyakimya na ataondoka kimyakimya. kwanza ni mtu wa kawaida tu, kuna wabongo wengi tu hawamjui wala hawajawahi sikia jina hili.

huyu si ndio alipokutana na JK pale santiago bernebeu wakati anacheza real mdrid JK alivyoenda kumsalimia na kumkaribisha bongo alisema haijui TZ mpaka alivyotajiwa mlima kilimanjaro....sasa nini kimemleta kama sio ufukunyuku na umbea...siku hizi hata hasikiki na mpira wake ulishaisha kitaaambo.....apite kushoto tu
 
Kasha kwisha huyo. Sana anashangaa kaja tz hakuna hata wa kumshobokea. Bora hata angekuja manamziki wabongo wangeshtuka
 
Back
Top Bottom