DART: Sio lengo letu kuuza kadi za Mwendokasi siku za 'weekend'

DART: Sio lengo letu kuuza kadi za Mwendokasi siku za 'weekend'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imetoa ufafanuzi kuhusiana na malalamiko yaliyoibuliwa na Mdau wa JamiiForums.com alidai kuwa wakati wa Siku za Jumamosi na Jumapili wahusika hawauzi kadi zinazowezesha abiria kupanda usafiri wa Mwendokasi.

Kusoma hoja ya Mdau kuhusu tiketi, bofya hapa ~ Mwendokasi kutouza kadi siku za Wikiendi siyo sawa, abiria wanapata changamoto
photo_2025-08-02_16-02-36 (1).jpg
Akitoa ufafanuzi huo Mtendaji Mkuu wa DART, Dkt. Athumani J. Kihamia, amesema sio lengo lao kuuza kadi wakati wa Siku za Jumamosi na Jumapili, ambapo amesema kwamba abiria anaweza kupata kadi kwa siku tano za wiki ambazo ni Jumatatu hadi Ijumaa.

Anasema "Sio lengo letu kuuza kadi siku za weekend (Jumamosi na Jumapili) kwa sababu sasa hivi tunaona karibia kila Mtu anayo kadi, kwahiyo tunauza kama akiba."

Amesema kuwa walitoa muda wa kutosha kwa ajili ya zoezi la Wananchi kusajili kadi, ambapo amesema kuwa awali walikusudia zoezi hilo lifanyike kwa miezi sita tangu Septemba 2024 lakini amedai hadi sasa bado ni zoezi endelevu.

Amesema kuwa wananchi wamehamasika sana kuchukua kadi hizo, hata hivyo amesema kadi hizo zinaongeza ufanisi wa kukusanya mapato na kuepusha ubadhirifu.
 
Back
Top Bottom