John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema mwaka huu utaongeza mabasi mengine mapya 95 ikiwa ni sehemu ya hatua za kupunguza msongamano wa abiria kwenye vituo vya mabasi hayo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Dk. Edwin Mhede alibainisha hayo jana wakati akifungua mafunzo kuhusu mipango ya mitaa kwa Jiji la Dar es Salaam.
Alisema wakala ulijitahidi kuongeza mabasi 70 hivi karibuni kwa ajili ya kupunguza msongamano huo lakini kutokana na wananchi wengi kuchangamkia usafiri huo, mahitaji yanaendelea kuongezeka.
Alisema zamani abiria alilazimika kusubiri basi kwa dakika 30 lakini walipoongeza mabasi 70, muda huo ulipungua na kufikia dakika tano na kwamba mpango uliopo unalenga kuondoa hata hizo dakika tano ili abiria akifika tu apande basi na kwenda anakotaka.
“Kabla ya mwisho wa mwaka huu tunakusudia kuongeza mabasi mengine mapya 95 na tunaamini kwa kufanya hivi tutaondoa kabisa muda wa kusubiri kwa sababu maana ya kuwapo kwa mabasi haya ni watu kuwahi makazini," alisema.
Dk. Mhede alisema ujio wa mabasi hayo pia utapunguza kawaida ya watu kukimbizana kupanda mabasi, hali ambayo imekuwa ikisababisha ajali kwenye vituo hivyo kutokana na watu kukanyagana au kugongwa na mabasi.
Aliwaomba wananchi kuacha tabia ya kukatisha kwenye njia za DART kwa kuwa si salama kwao na kwa mabasi, akionya kuwa wananchi wengi wamekuwa wakipata majeraha wanapokatisha kwenye njia hizo.
“Hakuna haja ya kukimbilia basi, ukakatisha njia ya UDART uwezekano wa kugongwa ni mkubwa. Sasa ni muhimu ukazingatia usalama wako kwanza kabla ya kuchukua uamuzi wa kukatisha kwenye njia hizo,” alionya Dk. Mhede.
Kiongozi huyo pia alisema wakazi wa Kigamboni wajiandae kupokea huduma hiyo kwa kuwa fedha za kujenga mradi huo kuelekea maeneo yao zimeshapatikana na kinachosubiriwa ni utekelezaji wa mradi.
Alisema ujenzi wa DART kuelekea Kigamboni utafanywa kwenye awamu ya tano, akidokeza kuwa ziara za Rais Samia Suluhu Hassan nje ya nchi zimefanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia mradi huo kwa awamu ya tano.
Alisema ujenzi wa mradi huo kuelekea Kigamboni utapitia kwenye Daraja la Nyerere na maandalizi kwa ajili ya utekelezaji wake yanaendelea vizuri.
DART kwa kushirikiana na Shirika la Makazi Duniani (UN- HABITAT) na Taasisi ya Usafiri na Maendeleo (ITDP), wameandaa mafunzo hayo ya siku mbili kwa ajili ya watumishi wanaohusika na mipango miji na mitaa ya Jiji la Dar es Salaam.
Source: Nipashe