Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,034
- 7,590
Wakati mnaendelea kujadiri suala la nauli hebu tambueni umuhimu wa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi. Msisahau mradi huu ni mkubwa na unatakiwa kutunzwa ili udumu. Sasa ili malengo yaweze kufikiwa ni vyema mkaelewa namna watanzania tulivyo, wengi wetu si wasikivu na hatuelewi haraka, tunahitaji muda wa kutosha ili kuelewa. Zikiwa zimebaki siku 5 ifikie tarehe rasmi iliyotangazwa Jan 10 tunawasihi mtoe elimu mapema. Kuna vifaa, kuna vituo, kuna nauli na kuna magari yenyewe, haya yote yanahitaji kueleweka mapema kwa wananchi ili kusiwepo kulaumiana baina ya pande hizi kuu mbili. Ni hayo tu kwa leo.