Dark Day: Ajali ya Mbeya na Mtwara

Dark Day: Ajali ya Mbeya na Mtwara

Sizinga

Platinum Member
Joined
Oct 30, 2007
Posts
9,519
Reaction score
7,287
Ajali ya Juzi Mbeya iliyohusisha bus kuwagonga wanafunzi waliokuwa wanakimbia barabarani imeondoa vijana wetu 6 na wengine majeruhi. Ajali hii imetokea alfajiri tarehe 26.07.2025

Ajali kama hii ilitokea Mtwara ilihusisha school Bus kuingia mtaroni na kusababisha wanafunzi 8 kufariki na mwalimu 1 na dereva 1 kufariki. Ajali hii ilitokea siku kama hiyo alfajiri ya tarehe 26.07.2022

Itakumbukwa pia wanafunzi wa Sabodo January 2014 wakati wanakimbia mchakamchaka asubuhi waligongwa na gari na kusababisha vifo vya wanafunzi 4 hukohuko Mtwara.

Hizi ni tarehe mbaya kwa historia za ajali Tanzania. Tuendelee kuchukua hatua za tahadhali hasa kufanya mazoezi kwenye kingo za barabara.
 
Tuendelee kuchukua hatua za tahadhali hasa kufanya mazoezi kwenye kingo za barabara.
Hapa hujaeleweka vyema mkuu. Tuendelee kufanya mazoezi kwenye kingo za barabara au tuache kufanya mazoezi humo?
 
Wanafunzi hawana uwanja shuleni kwa ajili ya mazoezi !?
Anyway ajali ni kitu kibaya sana
 
Back
Top Bottom