Darasa la kupigilia pamba kijanja | Page 16 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Darasa la kupigilia pamba kijanja

Discussion in 'Urembo, Mitindo na Utanashati' started by Bitoz, Mar 17, 2016.

 1. Bitoz

  Bitoz JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2016
  Joined: Aug 27, 2015
  Messages: 23,330
  Likes Received: 91,620
  Trophy Points: 280
  Habari wakuu,

  Nimeona na mimi nitoe darasa kidogo kuhusu mavazi sababu na mimi ni kipaumbele changu katika maisha.

  1.Epuka kuvaa marangirangi
  Wakati unamatch mavazi jitahidi kupunguza idadi ya rangi,rangi 3 tu zinatosha kukutoa bomba.[​IMG]

  2. Vaa kulingana na mazingira/sehemu
  Mtu mjanja anajua kubadilika kulingana na mazingira,sio kuvaa jezi la Man utd lenye jina la Wazza kwenye sherehe [​IMG]

  3. Masharti ya kuchomekea;
  * Marufuku kuvaa oversize/undersize
  * Usivae mlegezo
  * Hakikisha singlet haionekani
  * Usivae mkanda mrefu
  * Usivae makubanzi/sandals
  * Hakikisha umemach rangi[​IMG]

  4. Kama umevaa pensi /kaptula...
  * Hakikisha unavaa soksi fupi zisizoonekana
  * Piga raba au makubanzi/sandals bila soksi
  * Haipendezi kuchemekea
  * Hakikisha miguu ni soft [​IMG]

  5. Usivae shati jeupe kama la mwanafunzi
  Shati nyeupe ni nzuri kama unaijulia wakati unanunua hakikisha ina urembo wa aina yoyote ile au ni ya kimtindo sio kuvaa shati la shule.[​IMG]

  6. Hakikisha una suruali nyeusi
  Mwanaume yoyote yule wa kijanja anajua umuhimu wa suruali nyeusi sababu inamatch mashati ya rangi nyingi.[​IMG]

  7. Saa
  *Kama umevaa jeans/kadet unaruhusiwa kuvaa saa ya aina yoyote
  *km umevaa suti/suruali ya kitambaa epuka kuvaa saa ya mkanda wa plastic. [​IMG]

  8. Miwani
  Duh hapa pagumu kidogo lakini cha msingi zingatia muundo wa kichwa chako pamoja na aina ya macho uliyonayo na aina ya pamba ulizovaa pia.Sio umepiga jeans kali,kichwa kama madenge na macho kama bundi kisha unapiga miwani ndogo ya njano,ni kituko [​IMG][​IMG]

  9/.Vaa kofia za kijanja
  Kofia pia huongeza mvuto,chagua kofia kulingana na aina ya kichwa na mavazi uliyovaa,haipendezi kuvaa suti na kapelo.Kanzu sharti ivaliwe na barakashia ndo utaeleweka la sivyo ni sawa na kuvaa dera tu [​IMG]

  10/Mkanda
  *Usivae mkanda mrefu km vile umefunga nyoka kiunoni
  *Mikanda ya vitambaa au madoidoi inafaa kuvaliwa na jeans/kadeti/kaptula
  *Jitahidi mkumatch rangi ya mkanda na viatu kama umevaa nguo za kuchomekea
  *Zingatia upana wamkanda na rux za nguo yako[​IMG]

  11/ Tupia cheni za ukweli
  Mikufu ya kiume pia huongeza mvuto
  * Kama umevaa nguo za kuchomekea au suti itapendeza ukivaa cheni nsogo ambayo haitokezi nje ya shati
  *Kama umepiga pamba za Joshua mfano T.shirt na jeans hapa tupia cheni kubwa lakini hata cheni ndogo zinakubali[​IMG]

  12/Uvaaji wa Tie
  *Vaa kulingana na urefu wako
  *Km wewe mwembamba inapendeza kuvaa tie nyembamba
  *Jitahidi kumatch tie na rangi ya shirt/suruali
  *Hakikisha tie yako imefungwa vizuri shingoni[​IMG]

  13/T.shirt na Jeans
  Wanaume wajanja wa mjini hupenda kupiga t shirt na jeans na chini kutupia raba Kali.....Vazi hili lina mvuto wa aina yake hasa limivaliwa kitaani na sehemu za mitoko km vile kwenye Club za starehe [​IMG]

  14/Vaa viatu kijanja
  Hapa pia Kuna changamoto
  *Usivaa suruali ya kitambaa na Raba
  *Usivae suruali ya kuchomekea na makubanzi
  *Ukipiga jeans unaweza kumatch t.shirt/shirt na rangi ya viatu
  *Ukivaa suti yakupasa upige kiatu kikali ....ulikosea itakuwa sawa na Toyota Mark X yenye matairi ya Fuso !!![​IMG][​IMG]


  ***Usipojua kuvaa utadharaurika***

  The Bitoz
   
 2. ukhuty

  ukhuty JF-Expert Member

  #301
  Dec 16, 2016
  Joined: Oct 9, 2016
  Messages: 5,151
  Likes Received: 5,371
  Trophy Points: 280
   
 3. Bitoz

  Bitoz JF-Expert Member

  #302
  Dec 26, 2016
  Joined: Aug 27, 2015
  Messages: 23,330
  Likes Received: 91,620
  Trophy Points: 280
  Jamaa hajui afanyalo
   
 4. usser

  usser JF-Expert Member

  #303
  Jan 8, 2017
  Joined: Sep 25, 2015
  Messages: 3,857
  Likes Received: 2,279
  Trophy Points: 280
  Aaaah me shart jiens plus mabut ndo fashion yang aseee
   
 5. Bitoz

  Bitoz JF-Expert Member

  #304
  Jan 20, 2017
  Joined: Aug 27, 2015
  Messages: 23,330
  Likes Received: 91,620
  Trophy Points: 280
  Imekaa poa
   
 6. Joseverest

  Joseverest Verified User

  #305
  Apr 15, 2017
  Joined: Sep 25, 2013
  Messages: 3,139
  Likes Received: 2,169
  Trophy Points: 280
  aiseee
   
Loading...