Darasa la 7 kwa DSM watoto wanasoma balaa

bulabo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
620
759
Nina dogo anasoma shule hizi za kulipia std 7 ee bhana wanasoma kuanzia saa 12 asbh wanapumzika saa nne muda kidogo tu saa nne na nusu wanarudi darasani mpaka saa nane.

Wanaenda kula wakirudi wanasoma tena mpaka 12 jioni wanaenda kula wanarudi tena mpaka saa tatu usiku. Hivi hata shule zingine wanasoma hv maana nilimuuliza mkuu wa shule akaniambia mambo ni mengi kuliko muda uliopo.

Nikiwaza me nilivyosoma na nikapasua mpaka lakini kizazi hiki kinalishwa mpaka ubongo unakomaa akiwa mdogo..je shule zingine wanasoma hv kwa madarasa ya mitihani au ndio kuizinisha tu ulipaji aa ada kubwa.
 
Hao walimu huenda ni wachache na muda wa vpindi utakuta huwa wanafanya mambo mengine ya kuwaingizia kipato hivyo wanawapelekesha puta ili mladi Mada ziishe wao wafanye mambo yao.

Pia wanataka wafunzi wakose hata muda wa kuangalia etuguru

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna shule darasa la 4 wanasoma hivyo pia. Bora hata hao ni la 7 mkuu
 
Hao watoto wa dar wazuri sana wakifika sekondari hasa wakienda shule za huku vijijini (mbali na dar) wanakimbiza vibaya....

Elimu bora ipo majiji makubwa tu huku vijijini hali ni tete
 
Huo ni upuuzi nakusoma hivyo sio kufaulu... mtoto anatakiwa apate muda wa kurelax na kujisomea mwenyewe.

Mimi mpaka na maliza form six PCM na nikaweka 1 kali sijawahi soma tuition na shule nilikuwa natoka saa saba nafika nyumbani nampuzika lisaa limoja naanza self study mjengee mtoto mazingira ya kujisomea zaidi sio siku nzima yupo darasani.

Mkuu wewe mwenyewe nadhani umeenda shule je ulisoma kwa style hiyo?

Tusipokuwa makini tutatengeneza taifa la vilaza.
 
Nina dogo anasoma shule hizi za kulipia std 7 ee bhana wanasoma kuanzia saa 12 asbh wanapumzika saa nne muda kidogo tu saa nne na nusu wanarudi darasani mpaka saa nane.

Wanaenda kula wakirudi wanasoma tena mpaka 12 jioni wanaenda kula wanarudi tena mpaka saa tatu usiku. Hivi hata shule zingine wanasoma hv maana nilimuuliza mkuu wa shule akaniambia mambo ni mengi kuliko muda uliopo.

Nikiwaza me nilivyosoma na nikapasua mpaka lakini kizazi hiki kinalishwa mpaka ubongo unakomaa akiwa mdogo..je shule zingine wanasoma hv kwa madarasa ya mitihani au ndio kuizinisha tu ulipaji aa ada kubwa.
Ilo jibu la.mwalimu anaonyesha ni mwanasiasa tosha ...wanafundisha tu ku cover syllabus na kumaliza topics

Ila kama anatambua. Muda ni mchache kuliko mambo basi ajitahidi afanye vitu vya uweledi
 
Ukihitaji mtoto wako aje kusoma moshi shule za biarding za serekali unitafute
Ada ni 600k-750k per year

Call
0764616353
 
Back
Top Bottom