Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,327
- 24,209
Majuzi mto Mkondoa umepita juu ya daraja pale Dumila.
Hii si mara ya kwanza, kama sikosei ni karibia ya nne hivi.
Na mara zote tuta la barabara linachukuliwa.
Kina cha mto kwa sasa hivi ni mita moja na nusu hadi mbili hivi.
Nimepita hapo miaka ya 1990, kina cha juu cha maji nilikuona ni karibia mita 8 au zaidi.
Nini kimetokea?
EROSION au mmomonyoko wa ardhi unaleta udongo mwingi sana tokea sehemu za nyanda za juu kuliko na ukulima usio na weledi.
Sasa hivi pale darajani kuna mchanga wenye kina cha zaidi ya mita 6!
Kwa hiyo tatizo ni kubwa kuliko linanavyofikiriwa.
Solution yangu ni hii:
1. Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Tanga na Arusha inayopakana na mto Mkondoa ,wasimamie kwa karibu sana ukulima bora usioendeleza mmomonyoko wa ardhi.
2. Kwa karibia kilometa 4, toka Dumila kuelekea kale kapori karibu na Gereza, tuta la barabara linyanyuliwe si chini ya mita 4 ikiwa ni pamoja na kuongeza ma culvert ya kutosha.
3. Hili si tatizo la TANROADS peke yao, ni tatizo la kitaifa.
4. Mchanga pale mtoni ni mali. Mchangabunaweza kuvunwa kwa winhi sana nabkusagirishwa hadi Dar au Zanzibar , sehemu zenye uhaba mkubwa wa mali asili hiyo.
Nawasilisha.